Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Wewe nawe ondoa kauli za kipumbavu, mkataba utawekwa sign, uchaguzi wa serikali za mitaa CCM, uchaguzi ujao CCM, nadhani mmesahau JPM alichowafanyia piga chini mpaka mwenyekiti wenu ohhh sijui tuandamane hakutoka hata mmoja barabarani. Mama Samia kaja kamuonea huruma kamtoa sasa pembe zinakuwa dawa ipo karibu tu.
Mbona hoja zipo low Sana. Kwa hiyo Yale ndio upendayo wewe. Kweli tupo tofauti Sana. Wenzako wanaomba msamaha wewe unapongeza? Kweli

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Nani wenzangu wanaliomba msamaha? msamaha wa nini? kuna kitu lazima ujue hakuna hata siku moja nchi nzima ikakubaliana 100% hata liwe jambo zuri kiasi gani kuna mtu atalipinga ndio maana tuna uchaguzi na hizi chaguzi majority ndio anaendesha serikali na ndio wanaamua kwa niaba ya watu hata kwa wale minority sasa hatuwezi kuendesha serikali na maamuzi kila siku kwa kuomba maoni ya kila maamuzi subirini chaguzi anayeshinda anaunda serikali na kufanya maamuzi.
 
Walioelewa mtuambie mm sijaelewa lolote..Nilitegemea kama AG ungetambaa na ulalo wa Sheria ukichambua issues ambazo wananchi wana mashaka nazo mfano..Useme hii miaka sio milele wala sio mia ila iko hivi na vile..useme pia nchi itafaidika hivi na vile kuanzia mwaka huu mpaka huu...sasa ukianza kusema miradi inakwama kweli bandari ikiendeshwa na DP world ndio miradi haikwami??? miradi gani?? wewe toa majibu ya hoja za wananchi sio miradi imekwama...Nchi hii dah ni ya kuhurumia sana...
Achambue ibara za makubaliano.Ushirikiano udiotaja ukomo maana yake Nini? Nikisema ni ushirikano wa milele nimekosea wapi?Miradi kuendeshwa Kwa Sheria za Uingereza na za Tanzania haina shida? Tanzania ni dola lenye mamlaka kamili,je,Dubai ni dola kamili?
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.

"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.

Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.

"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.

Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.

"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.

Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.

"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.

Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.

"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.

Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Credit: Jambo TV
IBARA 4(2) Kwamba serikali inapopata mwekezaji eneo lingine sharti iende Dubai kuiomba DPW ili iridhie, hiyo imekaaje sawa? Kwamba Taifa la Tanzania liwe linaomba ridhaa kwa Waarabu, utafikiri ni nchi yao, bado mwanasheria anaona sawa tu?
 
Wewe nawe ondoa kauli za kipumbavu, mkataba utawekwa sign, uchaguzi wa serikali za mitaa CCM, uchaguzi ujao CCM, nadhani mmesahau JPM alichowafanyia piga chini mpaka mwenyekiti wenu ohhh sijui tuandamane hakutoka hata mmoja barabarani. Mama Samia kaja kamuonea huruma kamtoa sasa pembe zinakuwa dawa ipo karibu tu.
Wewe kweli kichwani zimo? IBARA 8 ya mkataba inampa haki DPW haki ya kumiliki ardhi maeneo ya bandari iwapo Kuna wakazi waondolewe bila fidia, wewe yote kwako ni sawa? Tena hakuna ukomo wa muda, wewe kwako ni sawa tu?
 
Hebu acha porojo za ku copy na kupaste wewe unadhani mimi ni mjinga kiasi hicho? nchi ina sheria zake hata wewe unaweza kuvunjiwa bila fidia kama umevamia eneo nje ya sheria unafidiwa kama umejenga kihalali maendeleo yamekufuata wewe sasa ni wapi wameandika hakuna kikomo? au unadandia kauli za hawa wanasiasa wenye kupinga kila kitu. Kuna mkataba gani duniani hauna muda labda useme wananunua hata ukinunua Tz ni lease tu. acheni kupotosha watu mbona mkataba wa LNG moja ya investment kubwa kuwahi kutokea Tz hakuna mtu ana ujadili.
 
1. Hakuna mkataba kuna nini?
2. Kwa hiyo hata mimi ninaruhusiwa kuusaini?
3. Mamjo mengine tumuachi mola ataamua ugomvi mwenyewe na wapiga kura 2025
Ohoooooo, unadhani CCM wanategemea sanduku la kura? Sanduku lao la kura ni TISS na jeshi la Polisi.
 
Hebu acha porojo za ku copy na kupaste wewe unadhani mimi ni mjinga kiasi hicho? nchi ina sheria zake hata wewe unaweza kuvunjiwa bila fidia kama umevamia eneo nje ya sheria unafidiwa kama umejenga kihalali maendeleo yamekufuata wewe sasa ni wapi wameandika hakuna kikomo? au unadandia kauli za hawa wanasiasa wenye kupinga kila kitu. Kuna mkataba gani duniani hauna muda labda useme wananunua hata ukinunua Tz ni lease tu. acheni kupotosha watu mbona mkataba wa LNG moja ya investment kubwa kuwahi kutokea Tz hakuna mtu ana ujadili.
Kwa hiyo Wewe ni mwanasheria? Tueleze Sasa kwa Nini Mwanasheria mkuu kaibuka mafichoni baada ya makelele, alikuwa wapi Mwanasheria mwenzio? Tueleze pia IBARA 4(2) inayoitaka serikali ya Tanzania kama itapata Mwekezaji mwingine iende Dubai kuiomba DPW ili iridhie, sisi ni watumwa wa Dubai mpaka tujidhalilishe kuomba?
 
Hiyo kazi ya JPM na sio kabambikiwa kuna ukweli na kama ni Mama basi heshima yake Mama maana jamaa mwenyekiti wao kasota ndani walibaki kwenda kumtembelea tu huko ndani. Rais ana huruma tu akija mtu kama JPM au Mungu angempe maisha marefu tu hawa jamaa wangeimba kila nyimbo..
Kwenye kesi ya Mbowe ya kubambikiwa ingekuwa ni mahakama huru tusingeona ule ushahidi wa kipuuzi wa serikali. Na hata jana Rostam Kalori kuwa mahakama zetu zinaagizwa kufanya mambo nje ya ushahidi. Samia ana huruma kwenye kesi za kubambikiwa? Huyo Magufuli unayemsifia kwetu ni mlevi wa madaraka kama walevi wengine. Ni mtu mjinga tu anaweza kusifia. matumizi mabaya ya madaraka.
 
Kwa hiyo Wewe ni mwanasheria? Tueleze Sasa kwa Nini Mwanasheria mkuu kaibuka mafichoni baada ya makelele, alikuwa wapi Mwanasheria mwenzio? Tueleze pia IBARA 4(2) inayoitaka serikali ya Tanzania kama itapata Mwekezaji mwingine iende Dubai kuiomba DPW ili iridhie, sisi ni watumwa wa Dubai mpaka tujidhalilishe kuomba?
Tazama upande chanya wa mkataba. Wanatoa mafunzo ya masuala ya bandari kwa wanafunzi wetu pale DMI pia wanakuja na mifumo ya kisasa ya upakuaji na upakiaji wa mizigo.

Hiyo ni IGA ni makubaliano ya jumla yaliyopita bungeni, huku kwenye mikataba ya kibiashara HGA wala haina nguvu yoyote kumbuka biashara hawatafanya bila ya kwanza kusajiliwa BRELA.
 
Wewe kweli kichwani zimo? IBARA 8 ya mkataba inampa haki DPW haki ya kumiliki ardhi maeneo ya bandari iwapo Kuna wakazi waondolewe bila fidia, wewe yote kwako ni sawa? Tena hakuna ukomo wa muda, wewe kwako ni sawa tu?
Mnapotoshwa na kina Mwabukusi na nyinyi mnaingia chaka mazima.
 
Mkataba uliingiwa na ushahidi huu hapa👇
 
Kwa hiyo Wewe ni mwanasheria? Tueleze Sasa kwa Nini Mwanasheria mkuu kaibuka mafichoni baada ya makelele, alikuwa wapi Mwanasheria mwenzio? Tueleze pia IBARA 4(2) inayoitaka serikali ya Tanzania kama itapata Mwekezaji mwingine iende Dubai kuiomba DPW ili iridhie, sisi ni watumwa wa Dubai mpaka tujidhalilishe kuomba?
Ondoa ujinga wako huo mnalishwa matango pori huko na unakuja na vi IBARA huko mnadanganyana unadhani serikalini kuna wehu huko. weka hicho kifungu nikutafsirie na kwanini usiweke hizo signature walio sign huo mkataba mnaambiwa bado mkataba nyinyi mmesharuka tunauza, kiti kinachouzwa si kina bei wekeni tumeuza bei gani?
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.

"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.

Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.

"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.

Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.

"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.

Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.

"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.

Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.

"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.

Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Credit: Jambo TV

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi ( PhD).
Soma hapa👇👇👇

Huu mkataba hauna hadhi ya intergovernmental yani IGA kwa sababu Dubai siyo nchi bali ni serikali ya mkoa kama serikali ya mkoa wa Simiyu.

Kama hutaelewa utakuwa umetumwa.
 
Attachments

  • 812FA4B3-C6BB-457F-83FD-467411BBCB99.jpeg
    812FA4B3-C6BB-457F-83FD-467411BBCB99.jpeg
    75.7 KB · Views: 3
Upuuzi mtupu.
Ngoja nikukumbushe, kama hukumbuki mwenyewe kuhusu hili jambo:
Hebu rudi nyuma tokea ujiunge humu JF, Aug. 2 2016 usome yoooote uliyokwishachangia humu jukwaani. Hapo utaona jibu sahihi kuhusu uwezo wako wa kifikra.

Nadhani hili linatosha kukupa maelezo kamili.
 
Back
Top Bottom