Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa

Hajajibu hata moja. Angesema ardhi gani inaongelewa? Bandari ipi? Vipi kuhusu air space? Angefafanua je ni miaka mingapi iliyotajwa?
 
Mbona huku binafsi nilishapita siku nyingi sana; kuna lipi jipya tena la kuelezwa amablo silijui.

Unachoniambia hapa ni kwamba hiyo "barua ya uchumba" hata ikiwa na matakataka mengi siyo neno?

Unakwenda kuchumbia, hapo hapo unaonyesha dalili zote za kuwa mme katili kwa huyo mchumba wako, utafanikiwa kweli?

Hao wazazi wenyewe watakuwa na upungufu mkubwa, kwa kudhani tu kwamba kwa kuwa "posa" inaletwa na mtu mwenye ukwasi mkubwa, hayo mapungufu yanayojionyesha kwenye barua ya "uchumba" siyo neno. Yapuuze tu?

Hao wazazi zitakuwa haziwatoshi kichwani, na huyo binti yao hawamthamini kabisa.
 
ACHANA NA NDOTO ZA NATIONALISM EAT YOUR PRIDE
hakuna kitu kama hicho.
Watu kama nyinyi kwenye jamii tunajua hamkosekani. Hii ni kawaida ya nyakati zote tokea enzi za utumwa hadi leo hii.

Watu mnaodhani utu wenu ni chini ya thamani ya hayo makombo mnayotupiwa chini.

Baadhi yetu hatuyakubali hayo; na tutaendelea kupoambana.

Na kama bado huelewi, hakuna mahali popote duniani, mapambano ya wenye kulinda hadhi ya utu wao iliposhindwa kufanikiwa.
 
Alitakiwa atoe ufafanuzi mwanzoni kabisa sasa kasubiri bajeti ipite ndiyo anaelezea. Nimemuona hapa kwenye newz domo zito km uji mmbichi.
 
Hiyo hatua haijafikiwa ikifikiwa tahadhari zipo kwa mjibu wa sheria za Tanzania
Nenda kawadanganye wapumbavu.
Watu kama wewe hapa uwepo huko TPA utakuwa na akili tena za kusaini chochote chenye maslahi ya Tanzania, tena makubaliano mtakayofanyia gizani?
 
Mambo yakijadiliwa kisheria watu wanasema hawaelewi
Watu wanataka mambo mazito kwa hoja nyepesi nyepesi maana ndio zinavutia
 
Anafanya watu wajinga! Hakuna mtu anapinga uhalali watu wanahoji na kushauri marekebisho wa vipengele vya MOU ili isije kutuletea matatizo kwenye mkataba huko baadae.
Huyu mwanasheria ni mkuu ndumilakuwili!..

Hivi anafanya watanzania ni mbumbumbu na mataahira kiasi hatuelewi nini Maana ya MoU!?

Hivi vipengele hakuna nchi inawezakubali kusaini huu ujinga zaidi ya Tanganyika tu!!!👇👇👇👇

So sad!!!👇👇👇
 

Attachments

  • Screenshot_20230621-201611.png
    37.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20230621-201742.png
    37.1 KB · Views: 3
  • Screenshot_20230621-201509.png
    39.5 KB · Views: 3
Hiv mwanasheria wetu mbna unatuchnganya, kwanza unagombeza ama unatueleimisha maana naona kama vile mm sikuelew kabisa Kwa sababu insu nzima ulitakiwa kuongelea mafanikio ya bandari ama hasala ya bandali kutokana na Sheria yako ama uwanasheria wako lakin hapa unategemea upande mmoja ambao ni upande WA mkataba WA maisha na lakin hujazungumzia upande WA mkataba WA miaka 100 WHY???
 
Mahakama ndiyo sehemu sahihi; wameshaenda tayari wataeewana huko
Mahakama za bongo hazitoshi kwani zinapokea maelekezo kutoka serikalini. Mashauri mengine hayana budi kufunguliwa mahakama za kikanda ambazo ziko huru zaidi.
 
Na usomi wake amekosa hata namna ya kujibu hoja tata, akaishia kunanga kama mswahili.
Dah! Labda ndio namna alivyoona ya kumridhisha 'mwajiri' wake.
 
Hapa kajibu kitu gani?

Kama AG alipaswa kujibu Kwa kutoa ufafanuzi wa ibara kwa ibara kwa kila hoja inayolalamikiwa kwa kuuchambua mkataba wenyewe..

Cha ajabu na yeye kajibu ki - Tulia Ackson na wabunge wenzake huko bungeni..

Kwa kifupi, he's too shallow. Likely kapigwa mkwara na kuambiwa huko kimeumana, toka na toa neno na neno lake ndo hili..!!

Kama ni alama, huyu angepaswa ku - supp hii paper..
 
Hawa jamaa ni blablaa tuu.
Alikuwa wapi wakati wa mjadala bungeni?
Leo kajitokeza kisa Mbowe kaongea jana?

Halafu nani kaongea kwamba ana pinga uwekezaji??? Wasi tuchanganye.
 
Kama amelazimishwa kujitokeza hadharani kutokea ufafanuzi.Mwanasheria Mkuu hajasema Kama ofisi yake ilishiriki kwenye timu ya majadiliano ,kwa nini Mwenasheria Mkuu wa Serikali hakuhudhuria/Kuwakilishwa kwenye tukio la kusaini MOU, Bandari/ Bahati masuala ya Muungano kwa nini tunaingia mikataba bila kushirikishs Tanzania Zanzibar, halafu tunajinasibu kuwa tutadumisha Muungano. Hamza Johari hayupo kwenye daftari la Mawakili wa Serikali, kanuni zinaruhusu kutoa legal opine,etc.Watanzania hawana Shida na ubinafusishaji au ukodishaji wa bandari zetu.Lakini Serikali ichukue tahadhari kuepusha migogoro siku za usoni,tumepigwa sana na Ticts Rights wa India (TRC),SAA(ATCL) nk
 
Mbowe ana nguvu sana kuongea kidogo , mwanasheria katoka mafichoni ...hata ivyo aje afafanue kwa nini mkataba una sahihi ya wapemba watatu
Hili nalo neno, maana hakuna sahihi hata moja ya mtanganyika........tukisema wamefanya conspiracy kujitajirisha kwa hila kwenye rasilimali za watanganyika tutakuwa tumekosea!!?
 
Ubaya hamko makini na madai yenu, watu wanasema wanapinga Makubaliano na wakatangaza kuandamana ila hakuna aliyejitokeza kuandamana.
Ukiwambia wanakasirika na kutoa matusi.


Binafsi naunga mkono uwekezaji wa Mwarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…