Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Feleshi ni muongo.Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.
"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.
Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.
"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.
Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.
"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.
"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.
Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.
"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.
Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.
"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.
Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Credit: Jambo TV
Ndio maana nakuambia ww ni bendera fuata upepo. Huna hoja zako zaidi ya hizi zinazowekwa huku jukwaani unazirudiarudia. Halafu wakati unaandika ujitahidi kuzingatia koma, nukta nk.Kama wewe tu hii ndio shida yenu wapinzani mnacholalamika kwa wengine ndio mnakifanya na hata ndani ya chama chenu nenda kajaribu kutaka kugombania nafasi ya juu ndio utajuwa true colour ya CDM, yalimkuta Zitto Kabwe
Tunashukuru TISS sana maana ingezikwa lakini baya zaidi sisi tungezikwa na chama cha VICOBACHAGUZI Tanzania hazitegemei sanduku la kura, zinategemea TISS na Polisi, zingetegemea sanduku la kura, CCM wangeshazikwa kitambo.
Huna hoja wewe umekariri tu umelishwa matango pori nisipoteze na mtu anayesikiliza sio kuchambuaYapo mambo 10 yasitokubalika likiwemo ukomo wa mkataba, tunapopata mwekezaji mwingine maeneo mengine tukaombe Dubai, Bandari ni suala la Muungano, kwa Nini bandari za Zanzibar zisiwemo?
Sawa mwalimu wa kiswahili. CCM wananiangusha hapa kuacha watu kama nyinyi kujificha nyuma ya computer. JPM tu angeishi miaka 10 tu shughuli yake mliiona mpaka mwenyekiti ubunge chali jelaaaaaNdio maana nakuambia ww ni bendera fuata upepo. Huna hoja zako zaidi ya hizi zinazowekwa huku jukwaani unazirudiarudia. Halafu wakati unaandika ujitahidi kuzingatia koma, nukta nk.
Unasifia ulevi wa madaraka badala ya utawala bora. Hapo ndio huwa nawaelewa sana wazungu kwanini huwa wanatuita manyani.Sawa mwalimu wa kiswahili. CCM wananiangusha hapa kuacha watu kama nyinyi kujificha nyuma ya computer. JPM tu angeishi miaka 10 tu shughuli yake mliiona mpaka mwenyekiti ubunge chali jelaaaaa
Nyani mama yako pia ungemwambia. Nenda tu kwa wazungu ukajiunge na ndugu zako kina LGBTQ sijui hao ndio wanakufaa. sisi huna adabu tunakupa ya shingo tu.Unasifia ulevi wa madaraka badala ya utawala bora. Hapo ndio huwa nawaelewa sana wazungu kwanini huwa wanatuita manyani.
Usingepanick ningeshangaa sana 😂Nyani mama yako pia ungemwambia. Nenda tu kwa wazungu ukajiunge na ndugu zako kina LGBTQ sijui hao ndio wanakufaa. sisi huna adabu tunakupa ya shingo tu.
Mimi sipanic na nakubali sisi manyani lakini manyani hata wewe wamekuzaa sasa tukiwa manyani wengi sawa tu. Uzungu wewe nenda sisi Tz yetu ni pepo yetu.Usingepanick ningeshangaa sana 😂
Mmesikia nyie wagalatia na parokia, haya nendeni sasa mkaimbe
Case closed
mwananchiSasa wewe mkuu unaongea kama nani na kwa niaba ya nani?
Hakuna mkataba ulioandikwa kuhusu uwekezaji lililopo ni azimio la makubaliano ya kuja kufanyika uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai.FAFANUA ukomo wa mkataba tukuelewe wewe usiyepotoshwa.
Naunga mkono wazo. Achague kati ya Dr. Slaa, Tundu Lissu ama Dr. Rugemereza Nshala. Mdahalo uwe mubashara kwenye Starrv, ITV na TBC wananchi tuchambue hoja.suala hili halitaaji madahalo.
ufafanuzi wa kutosha umesha tolewa na wananchi wameelewa vizuri,
ila wapo wachache wameamua kutokutaka kuelewa kwa maksudi, hao serikali iwapuuze, maana wanataka kupoteza muda bure.
Mtachambua 2025 kwenye uchaguzi, serikali ina mandate ya kufanya maamuzi sababu ndio wanaongoza nchi hatuwezi kama nchi kuwa na marais milion 61. Huyo sijui DR ni mpinzani kama wengine ndio maana kisha chukuwa upande wake na yeye ajadili kama nani nchi hii? yeye ni mwananchi kama wewe kama mimi. Anashida na huu uamuzi kama ulivyo wewe chaguzi zitakuja na siasa zitafanyika fanya kampeni mwisho wa siku wananchi watapiga kura. CCM wanatekeleza sera za chama 2020 to 2025 ndio sababu ya leo kuwepo hapo. Unashida subiri upige kura yako kwa Chadema.Naunga mkono wazo. Achague kati ya Dr. Slaa, Tundu Lissu ama Dr. Rugemereza Nshala. Mdahalo uwe mubashara kwenye Starrv, ITV na TBC wananchi tuchambue hoja.
Sent from my Infinix X689F using JamiiForums mobile app