Ukweli ni kwamba mwanaume hata ajitahidi vipi kukusamehe haitatokea kamwe, wanaume huwa wanadhani wanaweza lakini hawawezi.
Tutazungumzia hili kwa kutumia makundi matatu ya wanaume
KUNDI LA KWANZA
Hawa ni wanaume ambao tukijua tu wapenzi wetu wametusaliti huwa hatuna mjadala hata ulie, uombe msamaha sisi ni moja kwa moja tunapiga chini. Hatukupi muda hata wa kuzungumza.
KUNDI LA PILI
Hili ni kundi ambalo atajifanya kukusamehe lakini lazima kuna punishment utaipata mbele ya safari. Mojawapo ni kutoaminiwa. Kutakuwa na trust issues. Kwa mfano ukichelewa tu lazima atakumbushia, kwenye matumizi ya simu lazima atakufuatilia sana n.k Kidume anakuwa yupoyupo tu upendo sio kama zamani, hakuna msamaha hapo.
Kutokuaminiwa kwenye mahusiano huwa kunaondoa hisia za mahaba na upendo sana kwa mwanamke. Badala ya kufurahia ndoa utakuwa unavumilia ndoa. Shida yote ya nini kusanya virago ondoka.
KUNDI LA TATU
Hawa ni wanaume ambao anakuacha muendelee kwa sababu akutumie tu hasa kwa sex na akipata option ya mwanamke mwingine utaona tu unaachwa anafanya hivyo ili kulipiza kisasi au kama punishment.
Hapa nitawapa mfano; kuna demu alinipa stori walikuwa kwenye serious relationship penzi motomoto akamcheat jamaa yake akajua. Jamaa akafanya kama amemsamehe aendelee tu kumla, siku ya siku miezi imeenda alisikia jamaa anafunga ndoa, siku 3 alijifungia ndani analia. Angefanya maamuzi mapema hii trauma isingemkuta.
Binti unaingia kwenye serious relationship unacheat unaachwa unarudia tena kosa hilohilo kwa mwanaume mwingine na mwingine unaachwa. Unafikiri umri unakusubiri tukutane 30s.
Kila mwanamke msaliti akiulizwa ilikuwaje ukamsaliti mpenzi wako? Utamsikia anasema ilikuwa bahati mbaya. Sasa kama bahati mbaya ilikuwaje ukanyoa hadi mavuzi?
Learn or perish