Mwanaume anayepinga kuoa na ndoa halafu yupo magetoni anahangaika na masufuria kupika, ni masikini wa akili

Attachment yako mzazi ndio itaamua yote mzee

Child protection haimuhusu mwanamke peke yake ata wewe baba ndio maana watoto wanapenda sana mama zao kwasababu ya attachment yao walio wapa tangu utotoni

Believe mwanaume tangu mtoto anaandaliwa kuwa baba na mwanamke anaandaliwa kuwa mlezi wa familia hii ni ipmact of culture created

Siamini kwamba mwanamke pekee ndio mlezi bora wa familia naamin mtu yoyote anaweza kuwa bora kwenye familia ni the way utakavyo kuwa na familia yako

Nb uchaguzi utabaki kuwa wako unataka kuwa mtu wa aina gani katika familia yako?
 
Hakuna kitu kama hicho, hao Ke tunaishi nao na hakuna rangi iliyojificha linapokuja swala la masilahi ndipo utajua hujui.

Ke yuko radhi kushea na Me kila kitu ila si inshu ya pesa, ni big no "HAPANA".

Pia maisha hayanaga kanuni kabisa, Me wangapi wanasaidiwa majukumu ya kifedha na Ke ilihali hakuna hata utofauti kimafanikio kiuchumi kuliko Me ambao hawasaidiwi kabisa?

Wapaswa kuelewa inshu ya mafanikio kiuchumi maishani huendana na wakati na bahati (baraka za Mungu) wala si juhudi binafsi tu za kikazi, yani unakariri sana maisha ambapo huna tofauti na wale Wazazi wanaozaa Watoto wachache wakidhani ndipo patakuwa na unafuu wa maisha kwa maendeleo kiuchumi ilihali hujikuta kuwa hatua za kawaida sana miaka nenda rudi tena wengine huzidiwa mbali kabisa na waliozaa Watoto wengi kuliko wao.

Elewa maisha ni fumbo, ukiendelea kukaza fuvu lako kwa mtizamo wako uko sahihi kabisa maana naheshimu mawazo yako lakini ni heri ubaki kuamini unavyoamini life style yako nami niamini ninavyoamini maana maisha ni wewe mwenyewe na jinsi unavyoratibu kanuni zako kimaisha na kuziendesha upendezwavyo ilimradi tu usivunje katiba.
 
Wala sijasema children protection hainihusu la hasha! Tena basi hujajua jinsi gani nilivyo Gentleman kuhusu Watoto, si kwa urafiki, ukaribu na hata kufatilia maendeleo yao mara kwa mara ISIPOKUWA unapaswa utambue kwa asilimia kubwa sana Ke ndiye aliye na nafasi kubwa sana kimalezi kwa Watoto kuliko Me.

Mama walee Watoto wetu wazuri ila si inshu za kuwaachia house maids, HAPANA.
 
Ndio house maids ni special kwa kazi ndogo ndogo ila usimxuie mwanamke kufanya kazi ase ni kumnyima haki yake ya msingi
 
Hakuna kitu kama hicho, hao Ke tunaishi nao na hakuna rangi iliyojificha linapokuja swala la masilahi ndipo utajua hujui.

Ke yuko radhi kushea na Me kila kitu ila si inshu ya pesa, ni big no "HAPANA".
Unawaongelea vipi Cougars; Unaongelea vipi wale wanawake historically ambao waliacha Mali zao au kuwekeza kwa mwanaume; Unamuongelea vipi Michelle alivyom-support Obama wakati hana kazi na anaendeleza harakati zake..., au nikupe the really case study...


Au haujasikia wanawake wanawafadhili wanaume kuwapa mahari ili wapeleke kwao na wasiabike ?; Mkuu kama wewe pesa ni kigezo huo ni mtizamo wako wengine pesa ni makaratasi tu; na wewe ukiwa nazo nyingi utagundua kwamba pesa ni kiwezeshi tu na kile kinachokuwezesha kukipata ni more valuable kuliko hizo pesa
Pia maisha hayanaga kanuni kabisa, Me wangapi wanasaidiwa majukumu ya kifedha na Ke ilihali hakuna hata utofauti kimafanikio kiuchumi kuliko Me ambao hawasaidiwi kabisa?
Hivi nilikuwa nazumgumzia nini na wewe unazungumzia nini mbona kama hapa umepiga U-Turn; au umesahau ulichoandika paragraph ya kwanza ?
Mkuu huu ni mtizamo wako ambao nikaanza ku-argue naweza kujaza points mithili ya Bible kama ishirini; Mambo ya watoto kuja na Baraka yalikuwepo enzi za Child Labour (watoto walikuwa ndio wafanyakazi ukiwa nao wengi watakulimia, wanatunza mifugo n.k.) Karne hii ni kuwa nao kadri ya uwezo wako wewe ukiwa na watoto huwezi kuwalisha au kuwapa elimu hapo huwatendei haki hao watoto wala haujakamilisha majukumu yako na ndio hayo uliyosema mwanzo kwamba unaletea Jamii Panya Road; kwahio naweza kusema wewe ni liability katika jamii husika
Narudia tena hivi unasoma unachoandika na mimi ninachoandika naona kama unajipanga paragraph baada ya paragraph....
 
Sizani kama mwanaume anakataa kuoa bila sababu ya msingi
1.hali ya maisha
Kuna watu wanataka kuishi na mwanamke akiwa na kipato cha uhakika na sio waoga w maisha kama mnavozani bali ni hatki mpa shida mtoto wa watu
We kama huna aibu wengine wanazo tumeumbwa na hisia tofauti

2.kwa wenye ela kuna wanaotaka ku enjoy kwanza anaona akioa atamchezea mtoto wa watu ,na wengine wanaona wanawake anaowapata wanampendea hela zake

3.wengine tutaoa pale tukiona tunakata kuoa mda wako wa kuoa sio wetu [emoji2937]
 
Ubinafsi ni tatizo Kubwa sana kwa kizazi cha sasa.
Kila mmoja anajifikiria yeye tu, hakuna anayefikiri juu ya Wengine. Unahamasisha kuto kuoa, lakini unataka kuzalisha wanawake ambao wewe huna mpango wa kuwaoa Ili ulee watoto.
Je, wewe nae Baba ako alizalisha hivohivo?
Unafikiri kama ungezaliwa katika mazingira ya aina hiyo, Leo ungekuwa hivyo ilivyo leo?
Ubora wa wazazi wa Kesho, unategemea wazazi leo. Kuwa Mwaume sio Kazi nyepesi, Lazima ukubali kukutana na Matatizo na uyakabili.
Sio kukimbia Changamoto.
Kama haujiwezi Sawa, Wewe endelea kutafuta ujiweze Kwanza.
Ndoa ni Jukumu Kubwa tu, unapaswa kuwa na uwezo wa kutatua Shida ndogondogo
Wanawake wenye sifa zakuwa akina Mama kwenye Familia bado wapo.
Ni Wengi tu.
Matatizo yenu mnakwenda kuwatafuta wamama wa Watoto wenu kwenye Vilabu vya Pombe.
Mtanyooshwa tu.
 
Dinia ina package zote,ukitaka oa,usipotaka usioe.Usingo una raha zake na karaha zake pia,halikadhalika kuoa pia,kuna raha zake na karaha zake pia.All in all,kama mtu hutaki kuoa,Hakikisha unakua na watoto au mtoto.
Ngoja waje Kukuambia Kataa NDOA

Mimi huwa najiuliza hivi mwanaume kamili utasema Kataa ndoa [emoji1][emoji1]

Kuna shida mahali
 
Mke wa Nick wa Pili alikutwa kwenye vilabu vya pombe?
Mkuu we komaa na mkeo,kama umekubali kupambana na hizo changamoto,niwewe,ndomaana Kuna wanaume wanawafumania wake zao,na wanasuluhisha,maisha yanasonga,lakini wengine wanaachana,wengine hadi vifo vinatokea.Chamuhimu kila mtu aishi anavyoona inafaa.
 
Ngoja waje Kukuambia Kataa NDOA

Mimi huwa najiuliza hivi mwanaume kamili utasema Kataa ndoa [emoji1][emoji1]

Kuna shida mahali
Kuna jamaa Iringa kapigwa rungu na mke wake mpk umauti umempata.
Jamaa asingeoa, angekuwepo mpk sasa hivi
 
Issue yako ni ya kimtazamo.

Hujaonesha kwanini kukaa gheto ni ujinga
 
Shit gets outrageous

Kumbe wengi mmeoa kwasababu ya uvivu wa kupika?
Wengi wanaoa kwa kuwa kazi za nyumbani hawawezi.
Kuhusu ngono mbna hata kabla ya kuoa wanapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…