Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Leo ni yeye anapiga kelele kasahau ujinga huu kaanzisha yeye mwenye alifungua Radio inaitwa Sports FM. Radio yake ilikuwa 24hrs ni michezo. Aache unafiki.
 
Huyo mzee anasumbuliwa na mazoea.
Nyakati zimebadilika, Sasa redio zipo nyingi ni suala la kuchagua usikilize ipi au nini?
Akitaka za siasa, kilmo na ufugaji aende Uhuru, TBC, n.k.
Akitaka za dini zipo masaa 24.
Wakati wao michezo haikuwa shughuli rasmi ya kukupatia kipato. Siyo full time job. Michezo ilikuwa jioni baada ya kazi rasmi za kujipatia kipato.

Sasa michezo hasa soka ni ajira rasmi ya kipato kikubwa, kuanzia waalimu, wachezaji, wachambuzi hadi wana habari za michezo. Hivyo lazima wanye ajira yao sekta hiyo wawekeze muda wao siku nzima kufuatilia na kushughulika na mchezo husika.
 
Asiwapangie nini cha kufanya kama hataki kusikiliza habari za michezo Asubuhi azime redio yake na aendelee na shughuli zake
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
 
Nilijua ni mimi tu nnayeboreka na hayo matangazo yampira
tumekuwa Nchi ya Mazezeta, hatuwezi Kuchambua Vitabu vya Fasihi... Literatures... Mbinu bora za Kilimo... Ufugaji... kukicha tupo busy na Simba na Yanga
 
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
Anayeboreka afungulie TBC.
 
Akili za vijana zinatakiwa kufanyiwa rehabilitation juu ya hii michezo 24hrs.
Sio vijana ni wazee tembelea vijiwe vyote vya kahawa vya wazee wanajadili Simba na yanga Hadi wananuniana
 
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
Mfumo ndiyo unataka hivyo,watu wajadili mipira wakitoka hapo udaku umbea stori za wasanii
Inapigwa singeli mziki
Wakitoka hapo betting,wanajadili mipira tenaa mpaka usikuu

Ova
 
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
Halafu kujadili kwenye pumba tupu!
 
tumekuwa Nchi ya Mazezeta, hatuwezi Kuchambua Vitabu vya Fasihi... Literatures... Mbinu bora za Kilimo... Ufugaji... kukicha tupo busy na Simba na Yanga
Happy Valentine's dogolasi!😛 Endeleeni kuchambua mpira .Kenya wameshatupita
 
Kuanzia saa 3 mpaka 6 michezo, kuanzia saa 6 mpaka saa nane au tisa unapata mambo ya umbea ukiwa na mchanganyiko wa taarabu, mapisho na dondoo za Simba na yanga. Radio zingine huo muda utapata mambo ya bongo fleva.
Balaa zito kuanzia saa saa tisa au kumi, huu muda radio nyingi watangazaji wake ni walevi. Hapa Sasa omba Mungu asiwe ameamka nazo. Hapa ndo pale waswahili tunasema limtokalo mtu, ulimi hauna mfupa, makosa ya kibinadam. Yan huu ndo muda mtangazaji anajadili mambo ya Sheria na hiyo Sheria haijui, atajadili uchumi wakati yeye ni empty kichwani.
Ukimaliza, mida ya saa moja unazugwa na kitaarifa Cha habari Cha dkk 5, na radio zingine wanakurudisha kwny simba na yanga mpaka saa nne usiku.
Saa nne usiku sasa unambiwa kaa kwa kutulia upate ushauri wa mapenz. Hapa unashauriwa na mtu ambae ukiamka asubuhi unakuta amepost wanaume wote ni mbwa, wanawake kwanin mnataka nini, siku hizi hakuna mapenzi, nk.
 
Kusema kweli inasikitisha sana,jamii yetu inachangamoto nyingi sana, lakini kuanzia asubuhi mabishano ni mipira tu
 
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
Hata TBC, JUMAMOSI masaa 3 ni blaablaa za michezo na wachambuzi uchwara. Ni aibu kwa TV ya Taifa. Ni nchi ya wavivu ndio maana unaona hayo mambo.
 
Kijiweni kwetu tulipiga marufuku mijadala ya simba vs yanga, sijui kama tulikosea lakini binafsi naona ilisaidia. Ilikuwa kila watu wakiwa free ni Chasambi chasambiii hadi wengine tunaona hii ni kero, akatokea "ring leader" na kuwapa vijana muongozo. Sasa hivi stories zao wanapiga wakiwa nje ya mazingira, it's very boring watu wazima na akili zenu mnajadili na kubishana vitu visivyo na msingi tena mda wote.
 
Kweli ww chenga kabisa sasa ndo umeuliza swali gani hili la kipuuzi?
Unajua ni maelfu yawatz wangapi walio jiajiri kupitia vibanda umiza vilivyoko ndani ya nchi hii?
Unajua ni maelfu ya wachezaji wangapi walijio ajiriwa na mpira ndani ya nchii?

Unajua pesa wanazo ingiza wamiliki wa vyombo vya usafiri ,mahotel,mama ntilie,wauza vinywaji, wauza jezi, kwa sababu ya mpira?
Unajua kingamuzi cha Azam kinacho rusha mpira kinaingiza pesa ngapi kwenye mapato ya serikali?
Unajua ni wachambuzi wangapi walio ajiliwa kwenye maredio kwa sababu ya mpira?
Vibanda umiza navyo ajira? 😂😂😂
Hao wenye vyombo vya usafiri, mama ntilie na mahotel wangepata tu riziki bila pumbazo la simba na yanga
Ni sekta ya kidwanzi balaa na hata Kodi zake inazoingiza huwezi compare na hasara ya funza zinazojaa vichwani mwa watu siku kwenda siku; chasambi anajadiliwa kuliko hata kukatwa misaada ya USAID, we are not a serious people and it shows
 
Back
Top Bottom