Mwanza hapajabadilika kwa miaka 13, bado nyumba zinachungulia kutoka milimani

Mwanza hapajabadilika kwa miaka 13, bado nyumba zinachungulia kutoka milimani

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Mwaka 2010 nilikaa mwanza kwa mwezi mmoja nikifanya kazi pale TPA. Niliwahi kuja mara kadhaa kwenye mikutano ya siku moja moja hivyo sikuwa nazunguka sana.

Sasa nimeingia jana napita mjini pako vilevile, nyakato, miti mirefu, nyegezi, kirumba, capripoint, airport hamna chochote kipya. Gold crest ipo vilevile.

Ina maana miaka yote hii hakuna maendeleo yoyote mji huu? Rock city mall ipo kama vi-mall vya kawaida kule nyerere road Dar es Salaam.

Nyumba bado zinachungulia milimani kusikokuwa na miundombinu ya barabara.

20231028_094420.jpg
 
Kwani Mwendazake ndio alikuwa na Uchumi wa Mwanza mfukoni mwake? Achaga ujinga
Mkuu mzee alisaidia sana mzunguko na uchumi wa mwanza kuwa juu haswa kwa miradi yake, kwa kipindi cha miaka 6 mwanza iliinuka sana kiuchumi haswa mzunguko wa fedha, mirad mikubwa ilifanyikia kanda hii na pembezon mwa ziwa so matumiz yalikuwa mwanza kwa ukanda wote so nachokiandika nimekiona na nimekiishi so acha kutukana watu, binafsi na declaire interest kwamba mzee alisaidia uchum wangu kukua mara dufu… now mwnz n kama dead city mzunguko uko chini sana
 
Mfn soko kuu la mwanza rwagasole limesimama na njia kuu imefungwa ikapelekea masoko na maduka kugawanywa na pasionekane sehem ya biashara na soko limekuwa kiungo muhimu kwa watu wa mwanza kwa wafanyabiashara lkn mpaka sasa hv hali n tete na ujenzi wake uko slow sana
 
Na kwa habar za ndani zaidi uchumi wa mwanza umeporomoka sana tangu mwenda zake afukiwe! Yaani hakuna mzunguko wwt wa pesa kwa muda wa 2years now ni kama dead city now

Mkuu mwanza ilikuwepo kabla ya mwendazake na ilikua inaendelea vyema,cha kumshukuru mwendazake ni daraja la kigongo-busisi.
 
Mfn soko kuu la mwanza rwagasole limesimama na njia kuu imefungwa ikapelekea masoko na maduka kugawanywa na pasionekane sehem ya biashara na soko limekuwa kiungo muhimu kwa watu wa mwanza kwa wafanyabiashara lkn mpaka sasa hv hali n tete na ujenzi wake uko slow sana

Mkuu usihofu miradi ya tactic soon kuanza,mwanza haijawahi kufeli.
 
Nyumba za milimani haziwezi kubadilika labda mpaka huo mradi wa wawekezaji wa Brazil ufike. Pia maeneo uliyoyataja yote ni makazi ya zamani hatutegemei yabadilike maana wamiliki ni either wastaafu au marehemu.
Ukitaka kuona mabadiliko mkoa wa Mwanza nenda mji unako expand kama Ilemela wilayani, Ilemela ya Malaika, Kiseke , Buhongwa majengo mapya, usagara, Fela, nk. Kiukweli Mwanza imeendelea sana hasa kipindi cha mwendazake. Imeipita mikoa mingine mingi tu
 
Hivi unaposema nyumba zinachungilia kutoka milimani, ulitaka wazibomoe alaf wajenge tambarare?
Lini uliskia mwanza watu wamekufa kwa kukaa milimani?
Haya wewe daslam, sio nyie kila.siku mnalalamika mafuriko?
Shida unapita kwenye basi ukiwa unaenda kazuramimba huko halaf unawahi JF kuongea bila ushahidi.
All u said is just vague shyt, ungetembea ukaona in deep whats going on. Huko milimani, watu ndo wameporomosha majengo ya hatari wanakula upepo n.k
 
Back
Top Bottom