Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Hayo mambo ya % ya mizigo acha nayo, mzee ali taka SGR ikatoe ushamba huko kwao
 
Kwani SGR ni mizigo tu hakuna huduma ya abiria? kwa hoja hii unasema kama mkoa una mchango mdogo kiuchumi basi hawastahili kujengewa barabara ya lami kwa kuwa haichangii kiasi kikubwa. Hoja nadhani dhaifu SGR ni huduma na ikianza itafungua fursa nyingi na kama mizigo ilikuwa 10% unaweza kuvutia 40% kikubwa itaunganisha nchi kama tunavyounganishwa na barabara mikoa yote bila kujali ukubwa wa mkoa. Sio kila jambo kupinga tu huu mradi haukuanza awamu ya 5 huko nyuma ulifanyiwa kazi ni hali ya kifedha tu serikali haifanyi biashara ila inajenga miundombinu kutoa huduma na kuchochea fursa za kiuchumi. SGR na perfect service. Ndio maana wakoloni walijenga reli miaka hiyo sisi tunajenga ya kisasa.
 
Wewe biashara ya reli Ili iwe na faida lazima mizigo iwe mingi,kwa abiria inakuwa ni huduma
 
Hujui kitu wewe utopolo kwani unajua Kanda za Ziwa inachagia kiasi gani katika uchumi wa TZ?
Baada ya kilimo cha Pamba kufifia, na Wafugaji wa Ng'ombe kuhamia Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya baada ya kukosa malisho kutokana na Uharibifu mkubwa sana wa Mazingira, mchango wa Kanda ya Ziwa katika Uchumi wa TZ ni mdogo.
Kilichobakia huko ni Dhahabu ambayo HAISAFIRISHWI KWA TRENI.
Ujenzi wa SGR kwenda Mwanza ulichochewa na kukosa uzalendo na ukabila, kwa Kisukuma "primitive nonsense", kwa maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
 
Wewe biashara ya reli Ili iwe na faida lazima mizigo iwe mingi,kwa abiria inakuwa ni huduma
Sasa mizigo itakuja bila kuweka miundombinu kwanza? unaweka miundombinu halafu unawavutia wateja utaanzaje kuvuta wateja miundombinu huna. Unaweka Reli ya kisasa wateja watakuja kufuata huduma bora kama alikuwa anatumia gari siku 4 atatumia SGR siku moja. Siku za nyuma ilikuwa ukitoka mfano Iringa kwenda Arusha ilikuwa unakata njia mpaka Chalinze mbali leo baada ya kujengwa Dom to Arusha watu wanakata Iringa-Dom-Arusha mizigo inafika haraka. Weka SGR wateja watakuja kwa wingi hiyo 10% itakuwa 40%.
 
Saizi wanapigwa tafu na migodi 3 tuu huko ikishafungasha kama Buzwagi wanarudi kwenye umaskini wao waliouzoea.
 
Kwingine ambako kuna mizigo kama njia ya Kigoma na Mbeya kuna miundombinu gani?

Inaanza uhitaji ndio miundombinu inafuata
 
Hahaaaa
Mzee wa kuteseka na mwanza
Yani hapo ndo mwanzo jifunge mkanda kiunoni kazi ndo imeanza
 
Kwingine ambako kuna mizigo kama njia ya Kigoma na Mbeya kuna miundombinu gani?

Inaanza uhitaji ndio miundombinu inafuata
Serikali imefanya feasibility study kote wameshasema hii SGR itafika mpaka Songea huko mikoa ya kusini mwisho wa siku nia ni kuunganisha East, west, north na south kwa SGR kama barabara ni suala la kutafuta pesa ila SGR itakuja kufika kote na hili waziri mkuu alishasema bungeni. Feasibility study imefanyika.
 
Alikuwa anataka akaiunganishe na daraja la mke wake la busisi kule ukweni.

Ila Mungu anaIpenda sana TZ.
 
Huduma ya Abiria kwa Treni, inachangia chini ya Asilimia 20 ya mapato ya Reli.
Bila kubeba mizigo, SGR haiwezi kujiendesha.
Shirika la Reli linabebwa na mizigo ya kwenda Kongo kwa zaidi ya Asilimia 50.
Katika hali hiyo, busara ya kawaida inaonyesha kuwa SGR ilitakiwa iende Kigoma kwanza, ili iboreshe mapato ambayo yangetumika kukamilisha kipande cha Tabora-Isaka-Mwanza.
Mkulima mwenye busara, analima shamba lenye rutuba kwanza, na baadaye ndipo analima lile lenye upungufu wa rutuba.
Mwendazake aliamua kuanza na Shamba lisilo na rutuba.
Hakika, uamuzi huu wa kuanza na shamba lisilo na rutuba umechochewa na Ukabila wa Mwendazake.
 
Huyu ni poyoyo tu
Kazi yake ni kuiponda mwanza
 
Hoja yako ni hafifu kwa sabau SGR haina maana ya kutoa mizgo dar es Salaam kwenye huko mikoni bali pia kutoa mizigo mikoani kwenda Dar es Salaam. Sasa hivi mizigo ya kutokea kanda ya ziwa inapitia kwenye maroli kwa vile hamna njia nyingine mbadala. Usishahau kuwa kanda ya ziwa ina economic activities nyingi kuliko mikoa mingi sana, halafu reli inayokwenda mwanza pia itakuwa inahudumia Rwanda kutokea Isaka. Sijui uambiweje uweze kujua kuona maana ya strategic investment; SGR ni strategic investiment.
 
Mabandiko yako yote huwa ya kipumbavu tu. Huna lolote endelea kuota ndoto huku miradi ya daraja la Busisi, sgr ikikamilishwa. Ama sivyo kajinyonge.
Akili zake huwa ni fupi sana huyu mtu aisee kazi yake ni kuponda vyote vinavyofanyika kanda ya ziwa
 
Safi mkuu hongera kwa ufafanuzi Kunawatanzania akili ziko mndukuni kupinga kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…