Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Na ambayo inashuka moro, Dodoma,Tabora,Kahama,Shinyanga,Simiyu,Mara ni asilimia ngapi?hizi akili za kilaza Zitto zishindwe
Kwani moro, dodoma tabora ziko mbele ya mwanza?
Kumbe tu ukiwa mjambaji sana na akili zinapungu!!
Soma vizuri bandiko.

Unajua nilikuwa najiuliza Sana ni mantiki ya sgr kuelekezwa mwanza badala ya kigoma?
Na kwanini waliojenga centre Raiway walilenga Nini!
 
 
Safi mkuu hongera kwa ufafanuzi Kunawatanzania akili ziko mndukuni kupinga kila kitu
Kupaka rangi jumba bovu hakuongezi uimara..Takwimu ndio hizo hapo juu 10% kwa Mwanza route vs 41% for Kigoma route.

Sasa sijui unadhani hiyo Isaka itabadili kitu gani..passanger transit ni huduma sio biashara but kwa hali ilivyo Serikali itakuwa imefukia matilioni kutoa huduma na tutaendelea kutozwa kodi kila mwaka ya kuendeshea matreni yenu.

Je hizo pesa zingewekezwa else where au kwa model nyingine ya usafiri kama express way return yake si ingekuwa bora? Na kule kwenye tija ya biashara ndio sgr ingeenda
 
Tuseme ulichosema ni kweli je hujiulizi kwanini mpaka leo miaka 60 Kigoma ni mkoa pekee michache iliyobaki haina barabara za uhakika? juzi umesikia Mwanza BOT wamefungua branch pale sababu mikoa ya kule inachangia 25%. kama nilivyosema itakuja kufika kote huko kwa sasa wenye malory ya mizigo au bidhaa za Congo badala ya kuchukulia Dar watakuja hapo Isaka tu na kupeleka Congo hizi ndio fursa zitaletwa na SGR kama dry port mambo mengi yatakuja kwa fursa. feasibility study imefanyika inaweza kuwa ni rahisi mizigo kuchukuliwa Isaka to Congo badala ya kupeleka reli Kigoma lazima tuwaamini waliofanya study na zaidi hata watoa mikopo wanapitia study hizi ili kupitisha mikopo yao kwa kujuwa unafungua fursa katika uchumi. Tuipeni nafasi SGR mimi naamini ni kitu bora kabisa na itapunguza gharama za kurekebisha barabara zetu. Kama tunahoji hili la SGR kwenda Mwanza tungehoji barabara pia kwenda Mwanza kwanza kabla ya Kigoma hapo ingeleta logic.
 
Sgr kwenda mwanza iko kimkakati zaid ukizingatia biashara inayofanyika katika ziwa victoria na ushidani wa soko la uganda kati yetu na kenya. Kuiwin Uganda tulihitaji kupeleka sgr mpaka bandari ya mwanza ilikurahisisha biashara katiyetu na wao, ivi umewahi fikiria kwanini mradi wa sgr ya kenya kwenda uganda ulikufa?
Pili kwa upande jirani zetu kule kigoma asilimia kubwa soko ni letu na hapakua na haja ya kuharakisha kupeleka SGR. Nimalizie kwa kusema uamuzi wa kupeleka SGR Mwanza ni sahihi kabisa hasa ukizingatia na namna wapinzani wetu (kenya) wanavojipambanua.
 
Ni vizuri kufanya analysis ya Takwimu unazotoa.

Kuna uwezekano hiyo ndio GDP ya eneo tajwa lakini huo uchumi ukawa unazunguka mikoa ya jirani na ndani ya mkoa ila ukawa hauhusiani na maeneo mengine ya mbali.

Ukichambua vizuri utakuta volume ya biashara Kati ya Dar na Mwanza ni ndogo kuliko Mwanza na mikoa jirani,hata mizigo mingi ya ku export na ku import kuja lake zone inapitia Bandari ya Tanga na Mombasa kuliko Dar ndio maana figures zinasomeka 10%

Kwa mantiki hiyo kulikuwa hakuna haja ya connectivity ya sgr kwa sasa badala yake ingeenda kule ambako ingeleta tija.Ningekuwa mimi ndio naamua ningejenga express way Kati ya Mwanza-Singida-Tanga,Mwanza-Singida-Dar alafu sgr ningeipeleka Kigoma au njia Mbeya
 
Hakuna feasibility study imefanyika hiyo ni politics za Mwendazake tuu
 
Weka link ya bbc ikimuhoji huyo mtaaalam...Tuanzie hapo kwanza
 
Hakuna feasibility study imefanyika hiyo ni politics za Mwendazake tuu
Sasa unaenda personal, kamsikilize JK katika mahojiano na Salama aliongelea hili lilianza awamu yake. Mimi sijawahi kuwa mpenzi wa JPM lakini katika sio jambo lake binafsi hili lilikuwa ilani ya CCM feasibility study ilifanywa awamu ya 4 wala sio ya 5 ndio maana alipoingia yeye tu miradi ikaanza sababu ilishafanyiwa upembuzi,
 
Na lile liuwanja la kimataifa la Chattle kule kitovuni lilikua na maana gani katika uchumi wa nchi hii? muwe na akili wakati mwingine, mwendazake alikua hana vision yoyote ni mabavu tu na ukizingatia lililkua gonjwa basi balaa tupu, hii nchi ifike mahala wagombea wote wa nafasi nyeti wawe wanapimwa afya kwanza tena ya akili na mwili
 
Lawama zote kwa Magufuli kwa kuwa na upendeleo na ubinafsi! Alidhani kwa upendeleo huo atapendwa na wasukuma matokeo yake wanashangilia kutoweka kwake kuzimu!
Pumbavu wewe ndo mwakilishi wa wasukuma? Huko kigoma machakani kunakotegemea mizigo ya Congo kunanini zaid ya mizigo tu? Uache kupeleka mwanza ambapo utapata mizigo na a abiria ukimbilie sehemu ambayo usalama mpaka ukae sawa ndo uwe na uhakika wa mizigo
 
Kwa heshima na taadhima, ninaamini kabisa wewe unaitakia mema Nchi yetu.
Pamoja na nia yako njema, naomba nikuambie kuwa zipo njia (route) mbili za kupeleka mizigo Kongo.
Moja ni kupitia Mbeya, kwa njia ya Barabara, na ya pili ni kupitia Kigoma kwa njia ya Maji (Ziwa Tanganyika).
Kwa hali hiyo, hakuna Malori yatakayokuja Isaka kuchukua mizigo ya Kongo.
Jiografia ya Nchi ya Kongo iko hivyo.
Labda ungesema kuwa kwa kuwa Reli ya Kati ipo na inafanya kazi, mizigo ya kwenda Kongo itaendelea kwenda kwa kutumia Reli ya zamani (Metre Gauge) wakati Standard Gauge Railway ya Isaka-Mwanza inakula kodi za Watanzania.
Ukweli ni kwamba, SGR ya kwenda Mwanza imeingia kwenye kapu moja na Chato International Airport!
 
Nadhani mimi na wewe sote nia yetu nzuri katika hili na hoja kutofautiana mimi napenda tu. Nilivyosema mizigo ya Congo waje wachukulie Isaka sikuwa na maana gari zitatoka Congo hapana ni kama tungejenga reli mpaka Kigoma SGR kwa hoja uliyotoa kuwa 41% mizigo inaenda Congo kupitia Kigoma haina tofauti na kuchukuwa Isaka kwa maana haya malory yangefanya route fupi kutoka Isaka mpaka Kigoma halafu hapo usafiri wa majini. hata SGR inegefika Kigoma ni bado usafiri wa majini ungetumika.
 
FIKRA FINYU za Mwendazake Waziri wa Fedha,Uchumi na Mipango ndio huyu huyu Alishindwa Kumshauri
 
Tatizo una upungufu wa akili ungepungukiwa damu tungekuchangia!
 
Very unfortunate. #katiba mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…