Aliandika
PseudoDar186 mwaka 2019 namnukuu:
Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.
Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.
Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.
Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.