Hivi ni kweli mwenge wa uhuru utakimbizwa tena mwaka huu 2016 ?
 
Kwa nini usikimbizwe..........Kwani umefutwa.......?...
 
Pesa za kukimbizia Mwenge zitumike kwenye mambo ya maendeleo.
Mwenge uwashwe mlima Kilimanjaro. Ukishamulika kila upande wa Tanzania( kutoka mlima Kilimanjaro) uzimwe na watu warudi kwao wakafanye mambo mengine.
 
au uncl magu anasubiri wapange bajeti alafu azi-divert kwenye madawati
 
Utakimbizwa ila tunapunguza idadi ya wakimbizaji,magari, posho na ukubwa wa mwenge wenyewe ili usitumie mafuta mengi
 
Utakimbizwa ila tunapunguza idadi ya wakimbizaji,magari, posho na ukubwa wa mwenge wenyewe ili usitumie mafuta mengi
LENGO LAKE HASA NI NINI HUO MWENGE HASA KWA ZAMA HIZI...
 
Usipokimbizwa watu watapigaje hela, lazima ukimbizwe ili watu wapate sababu ya kupigia hela
 
Itakumbukwa kuwa mwezi wa 12 mwaka 2015 sherehe za Uhuru zilitishwa kwa kile kilichosemwa ni kubana matumizi, pia itakumbukwa kuwa sherehe za muungano nazo hazitaazimishwa kwa kile kilichosemwa kuwa ni kubana matumizi, shughuli zote za serikali kwa sasa zinaendeshwa kwa kuangalia hasa mpango kubana matumizi, wengi walitegemea kuwa hata Mbio za Mwenge nazo zitazingatia dhana hiyo hiyo ya kubana matumizi, lakini hali imekuwa tofauti kabisa ikiwa leo hii mbio za mwenge zimeaanzishwa huko Morogoro.

Swali la kujiuliza inakuwaje mbio za mwenge hazijawekwa katika mpango wa kubana matumizi? nini kinachofanya mbio za mwenge kuwa na nguvu kuliko siku ya uhuru na siku ya muungano?
 
Mimi najua hasara pekee

1.michango isiyona umuhimu inayoumiza wananchi

2. Kodi inatumika vibaya hii ni nje ya michango

3. Kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI

4. Kuongezeka kwa watoto wasio na baba

5. Sehemu ya wapiga deal(mafisadi)

Hebu na weww weka zako ziwe faida au hasara me sion faida ndo maana sijaweka
 
hakuna mradi wowote uliozinduliwa na mwenge wa uhuru uliodumu , hii ni kwa sababu ya laana ya Mwenyezi Mungu kutokana na machukizo yanayofanywa kwenye mikesha .
 

Mwenge hauna faida hata moja zaidi ya kusambaza ukimwi na kutumia pesa kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…