Mzee wa Ufipa katika ubora wake. Yeye kila kitu kinachofanywa na Serikali na chama tawala anakipinga. Huyu jamaa ataugua vidonda vya tumbo soon maana siku hizi anaandika kwa jazba na mihemko
huy jamaa huwa hana jazba
 
Mzee Tupatupa, huo mwenge si ndiyo umebatizwa jina na sasa umepewa jina la chama chenu yaani Mwenge wa CCM...kulikoni sasa unajitenga nao?
 
Kwa nyakati zile Mwenge ulijenga sana hisia za uzalendo na utaifa. Ulijenga hisia za upendo katika jamii na hata kitaifa. Ulijenga hisia za umoja na kusaidiana kama watanzania. Kwa kweli ulituunganisha sana japo inawezekana kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale.

Lakini yote mazuri ya Mwenge hayakuja hivi hivi tu! Hapana, yalikuja kutokana na aina ya viongozi na uongozi wa nchi uliokuwapo wakati ule - uongozi uliojali umma na maslahi ya umma. Viongozi tuliowaona kama ndugu na hata wakitambulishwa kwa title ya "Ndugu". Nyakati hizi za kila aina ya uchafu na ubinafsi Mwenge sio lolote tena; ni kukimbiza tu moto usio na faida badala ya dhana na falsafa vilivyokuwemo ndani ya tukio lenyewe.
 
Mwenge wa sasa ni chochoro la ulaji wa wachache, sio Mwenge wa Uhuru tena! Mbio zake zisitishwe na Mwenge uwekwe jumba la Makumbusho Butiama.
 
Haya haya mazungusha mikono yanaponda mwenge wa Uhuru ,lakini ukija mwenge wa Olympic yanaenda kukimbiza!!!!!

Nyumbu wanaomba wapewe nchi lakini hawana uzaraendo hata kiasi ya punje ya mchele
 
Mzee wa Ufipa katika ubora wake. Yeye kila kitu kinachofanywa na Serikali na chama tawala anakipinga. Huyu jamaa ataugua vidonda vya tumbo soon maana siku hizi anaandika kwa jazba na mihemko
Acha kudanganya vidonda vya tumbo vinasasabishwa na helicobacter pylori.Utawashika maskio wajinga wenzio.
 
Mzee tupa tupa unamkana mungu mwenge.Huoni chama pendwa kitakufa.
 
DHANA mwenge zamani ilitumika kuwaunganisha watu katika melengo ya kimaendeleo sasa dhana hiyo imepitwa na wakati. iwekwe katika kumbukumbu za taifa. Itumike dhana nyingine kuwaunganisha watu
 
Una akili sana.lile niliibada lakishetani.usishiriki kwa namna yoyote ile.
 
uwepo sana tena sana, lakini usikatishe mjini, upite kijiji kwa kijiji pembeni pembeni na kuzindua miradi iliyoko vijijini tu. mjini usipite kabisa na iwe marufuku bin makufuru kukatiza mji wa aina yoyote mkubwa kwa mdogo.
 
Una point. Kama ni kumbukumbu labda uwashwe siku ile 9/12 na kuzungushwa kiwanja husika na kupachikwa kwenye kilima bandia? Au ndio hutaki kabisa hata mawazo mbadala Mkuu?
 
Na hii misheria ya mitandao hii soon utasikia mzee tupatupa yupo mahakamani kwa "kukashifu" Mwenge!
 
Hivi wanajamvi ikulu imeshindwaje kuufutilia mbali mwenge wa Uhuru ukawekwa makumbusho kuna siri gani kuusu huo mwenge ??

Toka nimeanza kufatilia mbio za mwenge sijawai ona faida yake zaidi ya hasara kibao tunazopata kama nchi ndo maana nasisitiza mwenge ni janga la taifa

Unasafirisha watu wengi kwa wakati mmoja magari zaidi ya 100 nchi nzima
Alafu watu wanafika sehemu eti wanaweka jiwe la msingi kwenye darasa la milion 7 harafu wanalala eneo lile lile kwa garama za ajabu kweli

wako na wasanii wa Kuimba!
wako na madakitari wa kuwatibu !!
Wanakula!
Wanakunywa!

Yaani unazindua mladi wa million 7 alafu unatumia million 30 within the day
Alafu kama nchi mnakuja kusema mpo silius ?
Nyerere aliruhusu mwenge kipindi kile watu walikuwa awajaanza kujua matumizi kama sasa na matumizi ya wakati ule yalikuwa chini kwasababu ya kutokuwepo kwa inflation kama ilivyo sasa !!

ni haibu kwa nchi inayobana matumizi kuruhusu mwenge uendelee kukumbizwa nchi nzima kila mwaka!!

Niaibu kuzindua mladi wa million 7 wa jengo la dalasa arafu ukala pale pale
Kwa million 30!!!**********"*

Kama taifa tumepotea sana kwa kufanya mambo bila kushirikisha wananchi
'"Mwenge ni janga la taifa kila mtu anatakiwa kuupinga kwa nguvu na uwezi wake!!

"”"""Yaani unazuia umiseta arafu unaluusu mwenge""!!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…