Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Mwanakijiji,

Ningewaona watu wa CCM kuwa ni watu wa maana kama wangeahirisha kuuwasha mwenge mwaka huu mpaka hapo wangemalizana na ma-scandal yote yanayoumiza vichwa vya watu. Kuuwasha mwenge hakuna maana yoyote kwa sababu tumesha-prove kwamba other means za kuwamulika wahujumu uchumi ni more effective zaidi ya hili useless gimmick.

Let's be realistic; Pesa ya kugharamia mafuta ya mwenge ingeweza kutumika kujaza mafuta ya magari ya hospitali ili kuwapeleka waja wazito hospitalini. This is a waste of resources. Wake up - CCM people!!!
I totally agree with you. Lakini Kama mwenge unaondoa chuki palipo na chuki na heshima palipo na dharau basi hakuna mahali pazuri pa kuweka huu mwenge zaidi ya lumumba
 
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)

Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?

huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?

Katika vitu nilivyotaraji vingelifutwa mara moja ni huu mwenge maana sioni faida yake kiuchumi wala kijamii, maana kama mambo yenyewe yanakuwaga hivi kuna haja ya kuwa nao kweli?

upload_2016-10-15_7-12-23.png
 
Habari wadau!

Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.

Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.

Nini faida yake?

Kimsingi, Mwenge unatumia gharama kubwa mno, kiasi kwamba fedha hizo zingetumika kufanya shughuli za maendeleo, baadhi ya kero kwa wananchi ama zingekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.

Inashangaza kuona kuwa Mwenge ule ulikabidhiwa katika eneo la shule ambayo haikuwa na madawati.

Njia nzima katika Wilaya ya Manyoni, Singida, tangu tumepokea Mwenge, shule zote njiani wanafunzi walikuwa wamejipanga barabarani, hawakusoma siku hiyo. Lakini hata Mwenge haukusimama njiani.

Wananchi wa Lusilile na vijiji jirani waliniambia kuwa kulikuwa na msako maalumu kwa wananchi watakaokiuka kuhudhuria mbio za Mwenge, hivyo walilazimika kujipanga barabarani tangu asubuhi na baadaye kupigwa na jua kali, njaa na kiu zao hadi Mwenge ulipopita.

Wapo waliolazimishwa kucheza ngoma ili ionekane wanaufurahia Mwenge. Kifupi, wapo wananchi ambao hawakufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuheshimu amri ya kuhudhuria mbio za Mwenge

Hata hivyo, katika mbio za Mwenge, Mwenyekiti wa CCM na katibu wake, pamoja na viongozi wa Umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) ni watu wa kuheshimiwa kuliko hata askari wa cheo cha juu.

Kuna bajeti ya kuweka mafuta gari ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa CCM, wa UWT, na UVCCM, japo wanahadaa kuwa Mwenge ni wa kitaifa. Ni uongo, kuthibitisha hili, huwezi kuona popote risiti ya mafuta kwa magari ya wenyeviti wa mikoa wa TLP, NCCR, CUF, CHADEMA, NLD.

Kichefuchefu kingine ni kwamba kuna fungu la kununua nguo za mapokezi ya Mwenge, zipo tofauti kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya katibu tawala wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya Ofisi ya TAKUKURU, ofisi ya Usalama wa Taifa na viongozi wengine.

Pia unakuta kuna sare za mapokezi ya Mwenge zingine za kimbizia Mwenge. Fungu la suti hizo zilitosha kununua madawati kwa ajili ya darasa moja la shule waliyoenda kukabidhiana Mwenge ambayo haikuwa na madawati.

Mwenge unatembezwa na kaulimbiu za “kumulika wezi na wala rushwa,” nilishtuka zaidi tulipokuwa Manyoni Mjini, ukarabati wa mnara wa Mwenge, mnara ambao umejengwa miaka mingi huko nyuma, mnara ulipigwa rangi na kuandikwa kaulimbiu ya “Tumethubutu, tumeweza, na Tunasonga mbele” kwa gharama ya Sh. 2.5 milioni. Haiingii akilini. Watanzania tuache kuhalalisha wizi wa kimachomacho kama huu.

Mwenge ni nini? Kwanini unatumika kama alama katika mavazi na kadi za UVCCM? Mwenge una msafara mrefu kuliko hata msafara wa rais?

Katika msafara wa Mwenge, kuna kundi kubwa la askari polisi, sijui wote hao wanalinda nini? Hivi katika Tanzania nani anaweza kuwa na wazo la kuiba Mwenge? Na akiuiba ataufanyia nini?. Polisi wanaolinda Mwenge wapo makini zaidi kuliko hata wale wanaolinda benki.

Tunaambiwa wanaangalia usalama wa Mwenge, je Mwenge huwa unaugua? Mwenge unaweza kuwekewa sumu? Mwenge na TAKUKURU au uhamiaji zina uhusiano gani? Mwenge na mkuu wa Magereza, vina uhusiano gani? Mkuu wa gereza anahusika na wafungwa, je kwenye Mwenge kuna wafungwa? Mwenge na Uhamiaji lini na wapi? Mwenge na Jeshi la Wananchi ambalo jukumu lake ni kulinda mipaka, lini na wapi na kwa nini? Wote hawa wanalipwa pesa kuhalalisha mbio hizi.

Hivi hatuwezi kufungua shule mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kupanda miti mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kuzindua majengo mpaka Mwenge upite. Miaka zaidi 50 ya Uhuru tumegandamizwa kiakili na Mwenge, kwanini?

Hakika Mwenge sasa unaunguza wazalendo, unanyonya wanyonge, unanyanyasa walipakodi. Unamaliza fedha lukuki bila kuwa na tija. Rais anayebana matumizi ya hovyo amebariki ukimbizwe. Ajabu.

Ni vyema Mwenge nao ukafutwa na kuzikwa kabisa, kwani nalo ni jibu, tena limekomaa, tayari kwa kutumbuliwa
 
hata ukizuiliwa bado watu mtalalama tu.
oooh kulikua kuna watu wamejiajiri kupitia mbio za mwenge. na mambo mengine kedekede

Waswahili sisi tuna jema.
 
Hauna faida yoyote bali kuwaonea wafanyakazi wa Serikali hasa walimu ambao nchi nzima wanakatwa pesa zao chungu nzima tena bila ridhaa yao eti kwa mafuta ya mengi. Ni wizi mtupu wa mabilioni ya pesa za walipa kodi na kwa kujua kumejaa wizi kwenye pesa hizo hawataki CAG azikague.
 
Habari wadau!

Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.

Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.

Nini faida yake?
Ni milioni au bilioni 400 ? Lile daraja la kigamboni (Nyerere Bridge) liligharimu bilioni 254!

In any case, sikubaliani na kukimbiza mwenge
 
Mwenge ni nuru y Taifa......unawamulika waovu wote wenye nia mbaya kwa Taifa washindwe na walegee.....ni muhimu sana kwa Taifa
 
Back
Top Bottom