Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Hiyo chuki au ukweli? bisha kama si ukweli na ushahidi nimeuweka, ni ibada ya Kikatoliki na Makanisani mwenu haukosi huo mwenge.

Achana na mimi jadili hoja yangu yenye ushahidi na uipinge kwa ushahidi.

sometimes unavuta bange wewe sio bure,ushatembelea madhehebu yote ukakuta hilo likitu?acha ufala,kama vipi tembea mitaani utangaze udini wako...nilikuwa nakuheshimu kumbe adabu yako inakoma ukivuliwa pichu?
 
Kutoka 20: Na Mungu akaanza kunena maneno haya yote, na kusema: ?Mimi ni Yehova Mungu wako, ambaye nimekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya watumwa. Usiwe na miungu mingine yoyote dhidi ya uso wangu. ?Usijifanyie sanamu ya kuchongwa wala umbo lililo kama kitu chochote kilicho juu mbinguni wala kilicho chini duniani wala kilicho ndani ya maji chini ya dunia. Usiviinamie wala kushawishiwa kuvitumikia, kwa sababu mimi Yehova Mungu wako ni Mungu anayetaka watu wajitoe kikamili, na ambaye huleta adhabu juu ya wana kwa sababu ya kosa la akina baba, juu ya kizazi cha tatu na juu ya kizazi cha nne, kwa wale wanaonichukia;
 
Pitieni kwenye jukwaa la historia Kuna simulizi za aliyetoa wazo la kuanzisha mwenge
 
Kwani na hizo nembo mfano jogoo mwewe na makorongoshungi uliyoyataja hukimbizwa nchi nzima kama huku. CCM imekuwa ikihakikisha zoezi la kukimbiza hilo dude nchi nzima linafanikiwa kwa 100% lakini si kumaliza hata tatizo la madawati shule za msingi , poor strategies kabisa
 
Jana sikupata nafasi ya kusikiliza hotuba ya rais bungeni nilikua safarini huku kusini mwa Afrika, na kuna jamaa yangu alinijulisha kuwa ameongelea mambo mazuri kweli kweli ikiwa ni pamoja na kubana matumizi kwa mambo yasiyokua na lazima, sasa nauliza habari ya mwenge nayo ameikata?

kwa kuwa kwa maoni yangu nayo naona kuizungusha nchi nzima kwa kutumia kodi za wananchi ni kama kupoteza pesa ukizingatia miradi ambayo mwenge inazindua inaweza kuzinduliwa hata na mkuu wa Wilaya.

pia itapunguza maabukizi ya virusi vya ukimwi.
 
Mwenge ni laana kwa Taifa. Mwenge upigwe marufuku. Pesa nyingi zinapotea kwasababu ya Mwenge. Mwenge ubaki Makumbusho ya Taifa.

kuna miradi hata wenyewe wana uwezo wa kuzindua mfano bar na nyumba za watu binafsi.
 
Wanajamvi habari,
Mimi kama mwananchiwa Tanzania napendekeza pia kwa Rais wetu JPM afute mbio za mwenge wa uhuru na fedha zitakazookolewa zikalipe madeni ya watumishi wa umma wote ili kuongeza tija na morali ya kazi.
Naomba kutoa hoja
Toa maoni na mtazamo wako, matusi hapana.
 
Huo ndo mtihani mwingine kwa JPM.Kimsingi mbio za mwenge hazina tija na maslahi mapana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa hiyo naunga mkono hoja kuwa zifutwe mara moja....
 
Mh umeanza vizuri, sasa nakuomba utufutie mbio za mwenge kwani pamoja kuwa tunatumia fedha nyingi katika kuukimbiza mwenge huo lakini pia ni chanzo kikubwa cha uenezaji w magonjwa ya zinaa.
Wapinzani wamekuwa wakilalamikia sana swala hili, na walisema waziwazi kuwa wao watafuta mbio za mwenge na kuuweka mwenge huo makumbusho.
Kwa kuwa umeshakua sera za wapinzani kama kubana matumizi ya serikali na kupunguza safari za nje basi nakuomba uliangalie swala hili.
Nahofu waliopita watakwambia vingi vya kukutishia kuhusu mwenge lakini wewe ndiye rais wa nchi hii wao zama zao zimeshapita.
Akhsante
 
Tatizo la viongozi wetu wanaendekeza mambo fulani kama mwenge kwa kisingizio cha kujenga umoja na amani kwa kisingizio tu kwamba Mwl Nyerere alisema. Lakini ni mambo mangapi mazuri ambayo Mwalimu katika kipindi cha uhai wake aliyaasisi ambayo wameyafuta? Miiko ya uongozi, rushwa, ufisadi nk ni vitu Mwalimu alivipiga vita kwa nguvu zake zote lakini ni Kiongozi gani leo anayeweza kusimama kwa ujasiri kabisa akawaumbua hata viongozi waandamizi walioshiriki kwenye huu mchezo mchafu? Mwenge si msahafu, kila kitu kina wakati wake, wakati wa mwenge kukimbizwa nchi nzima umepita. Viongozi wanang'ang'ania mbio za mwenge ili kijinufaisha tu. Ikiwa bajeti ya mwenge inafikia hadi shs bilioni 20, hivi ni kweli hatuoni kama huu ni ufisadi mtupu?
 
Yani mwenge ufutwe tuu maana sioni umuhim wa hii kitu
 
Ndio maana tunamuomba mh atumbue hili jipu, imetosha sasa asisikilize wa awamu zilizopita,anakazi ya kujihakikishia ushindi 2020, waliopita wameshindwa kwenye kila kitu, asiwasikilize amani yetu haitaondoka kwa kufuta mbio za mwenge. Pesa nyingi zapotea kwa ujinga ujinga wa mbio za mwenge
 
Dhana ya mwenge na umuhimu wake iendelezwe. Ila haya mambio mbio yake yanayoambatana na gharama full stop
 
Tatizo la viongozi wetu wanaendekeza mambo fulani kama mwenge kwa kisingizio cha kujenga umoja na amani kwa kisingizio tu kwamba Mwl Nyerere alisema. Lakini ni mambo mangapi mazuri ambayo Mwalimu katika kipindi cha uhai wake aliyaasisi ambayo wameyafuta? Miiko ya uongozi, rushwa, ufisadi nk ni vitu Mwalimu alivipiga vita kwa nguvu zake zote lakini ni Kiongozi gani leo anayeweza kusimama kwa ujasiri kabisa akawaumbua hata viongozi waandamizi walioshiriki kwenye huu mchezo mchafu? Mwenge si msahafu, kila kitu kina wakati wake, wakati wa mwenge kukimbizwa nchi nzima umepita. Viongozi wanang'ang'ania mbio za mwenge ili kijinufaisha tu. Ikiwa bajeti ya mwenge inafikia hadi shs bilioni 20, hivi ni kweli hatuoni kama huu ni ufisadi mtupu?

na hiyo bilion 20 ni badjet ikiyotengwa serikali kuu..ila kila halimashauri hutumia si chini ya milion 80 kwa maandalizi ya mwenge
 
Back
Top Bottom