Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Hizo shughuli za Mwenge mi zinanikera sana, huo ni mtaji tu wa watu
 
Tupige kura nchi nzima. Tuukatae.

Maana ni ofisi ya watu ile, ma mia ya family yanaishi.

Raisi hataweza uzima mwenyewe.
 
Huu hauna manufaa yoyote kwa nchi zaidi ya kupoteza kodi zetu na kulazimisha wafanyakazi wa halmashauri kuchanga pesa, pia kupelekea vitendo vya ngono pale unapokesha.
 
tangu nipate akili nimekuta mwenge unakimbizwa kwa kaulimbiu mbalimbali ila binafsi sijawahi kujua manufaa ya mwenge zaidi ya kutumia pesa ambazo tumezipata kwa kuvuja jasho sana je kuna uhalali wa hizo pesa kuendelea kutengwa kila mwaka huku watu wakiacha kufanya kazi za kuleta maendeleo bali kuteketeza pesa ya umma??
 
Kwa muda mrefu kumekuwa na manung'uniko juu ya mwenge wetu hapa TZ, kwa nilivyopitia kurasa mbalimbali na kusikia maoni mbalimbali wengi hawaungi mkono swala la mwenge kuendelea kuwashwa na kukimbizwa nchi nzima!

Sina sababu ya kuanza kuelezea faida na hasara za mwenge . Kwa mliopitia mkajua habari za mwenge naomba tupige kura hapa ili tuone wepi wengi kat ya UWEPO au UFUTWE!!!

Piga kura yako kwa uhai wa NCHI yako.
Swali ni je mwenge wa uhuru uendelee KUWEPO AU UFUTWE??
Jibu ufutwe au uwepo tutahesabu na kujua nan kashinda!!
 
Ufutwe hauna maana yeyote, kwanza mwenge unasababisha watanzania wasijielewe, unafaya wawe watu wa ndio tu iwe kwa baya au zuri, kwa haki au dhuluma, ule moshi sio mzuri hata kidogo
 
Wajuzi wa mambo tuelezeni faida na hasara za mwenge wa Uhuru kwa maana na kukimbizwa nchi nzima je kuna sababu bado ya umuhimu wa kuendelea kuwepo na mbio za mwenge au nao ni JIPU.
 
Wajuzi wa mambo tuelezeni faida na hasara za mwenge wa Uhuru kwa maana na kukimbizwa nchi nzima je kuna sababu bado ya umuhimu wa kuendelea kuwepo na mbio za mwenge au nao ni JIPU.
uacheni mwenge wa uhuru uendelee kuliangaza taifa.
 
Kwa sababu mwanadiwani sasa ni manyota, tunamuomba aje humu atusaidie kutoa maelezo ili tusipotoshane.
 
Back
Top Bottom