Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakin kiujumla kwa sasa mwenge hauna faida mwana namtumbo mwenzangu, iz9 ulizomention hapo ni faida za zaman
kama umezaliwa Kinondoni, ukakulia kinondoni umesomea Bunge, sekondari mzizima chuo IFM kazi umepata crdb tawi la millenium tower
wikiend bata mlimani city sijui bahari beach kamwe huwezi jua thamani ya Mwenge
mwenge tuulize sie tunaokaa wilayani Namtumbo
Kwa miaka kumi ya utawala wa JK kitu ambacho kimem boost sana JK angalau kuna sehemu ambazo ameonekana kafanya kazi ni MWENGE
kwa sababu mwenge unaharakisha sana miradi VIJIJINI ... mkisikia mradi fulani MWENGE unakuja kufungua utawaona ma dc, ded, na viongozi wa halmashauri na wilaya wanavyokimbizana kufanikisha mradi ule ili mwenge unavyokuja kufungua uwe tayari umekamilika
atlest viongozi walikuwa wanazionea haya pesa za miradi ambayo mwenge ulikuwa unakuja kuzindua
SOMWENGE UWEPO MIAKA 1000 na rais Magufuli aupe sana nguvu huu mwenge
Mkuu unaongelea Mwenge ya Dar au Mwenge huu wa Uhuru.Mwenge iachwe kama ilivyo. Mambo mengine si lazima kujua.
Ulishawahi kufikiria kwani nini mkuu wa Wilaya, Mkoa, Waziri ama Rais anazindua mradi?kwani mkuu hiyo miradi lazima izunduliwe na mwenge?! hatuwezi kufanya na kuzindua miradi mpaka mwenge ufike?
Unaongelea mradi wa kuuza vitumbua au mradi gani?Nikuulize wewe unayesema umeishi Namtumbo, Ruvuma.....hivi hapo Namtumbo ukiwa na milioni 2, wewe binafsi hakuna mradi unaweza ukafanya?! Milioni 2 mkoani, tena Namtumbo ambaye nimepata kukaa, ni pesa ndefu mno, mno😱
Umesoma post #9,Miradi ya maendeleo, tuanzie hapa!!
Sasa huo Mwenge utafunguaje miradi bila kuzunguka/ kukimbizwa?Itafutwe Tu Namna Ya Kuuenzi Huu Mwenge Na Si Hii Tulonayo.
Mwenge Ufungue Miradi Hata Ukiwa Dar Then Mwaka Unaofuata Arusha, Kigoma Na Kwingineko.
Lengo Ufungue Miradi Sio Lazma Ukimbizwe Nchi Nzima, Unaweza Tu Kuazimishwa Hapa Kisha Kule Wakafungua Miradi.
Kuwe Na Mwenge Wa Mkoa Mkuu Au Hata Huu Mmoja Uazimishwe May Be Arusha Kisha Miradi Yote Tz Hufunguliwa Na Wakuu Wa Mikoa Au Wengineo.Sasa huo Mwenge utafunguaje miradi bila kuzunguka/ kukimbizwa?
Mwenge ukimbizwe dadoma tu inatosha mikoa mingine wakitaka kuuona waangalie taarifa za habar.
Hapana mkuu, barafu itaisha...dom ndio pazuri, mji mkuu wa nchi yetu[emoji2]Uwashwe na kuzimwa kulekule kileleni kwani kuna Shida yoyote si unamulika mipaka kisha unapumzika me naona mwenge usisumbuliwe tens uwake tuu kule kule kileleni tu
Hapana mkuu, barafu itaisha...dom ndio pazuri, mji mkuu wa nchi yetu[emoji2]
Kwanza unafahamu dhana ya Mwenge? Ukifahamu dhana ya Mwenge basi haiwezekani kabisa kufanyika hivyo unavyodhani.Kuwe Na Mwenge Wa Mkoa Mkuu Au Hata Huu Mmoja Uazimishwe May Be Arusha Kisha Miradi Yote Tz Hufunguliwa Na Wakuu Wa Mikoa Au Wengineo.
sio mwaka huu tu, bali kusiwe na mbio za mwenge kabisaaa, mbio za mwenge ni katika matumizi makubwa yasiyo na maana kabisa, nini maana halisi ya kukimbiza mwenge baada 45 ya uhuru na hali duni ya maisha. Hivyo vijisenti ya kugharamia mbio za mwenge si zingetumika kujenga maabara na kuziequip fully katika mshule ya msingi na sekondari. Kukimbiza mwenge 1962 na sana sana 1963 kulimake sense, baada ya hapo ni ufujaji tu.
Ni kiasi gani cha fedha kinafujwa?hili nalo jipu linahitaji kutumbuliwa...hakika mzee magu angeanza na hilo kwanza maana mm binfsi sijaona faida za huo mwenge zaidi ya ufujaji tu wa pesa za wananchi walipa kodi..