Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Sio tu kufunga siku arobain, Ile ratiba ya YESU ya maombi ni funga kazi most of time alikua anakesha akiomba alone zile nguvu za YESU hazikuja kwa granted

Kabla Mungu hajakupa nguvu zake anaangalia moyo wako, usiwe na kiburi hakuna kitu kigumu kama Mungu kukupa nguvu zake, shetani anakupa tu hajali
 
Hapa umeprove kabisa kwamba Mwamposa ni nabii wa kweli maana aliona shida yako
 
We kweli unamjua maana kipande kimojawapo ulichokiongelea na mm nakifahamu na sio kuhadithiwa
 
UONGO UNAKUSAIDIA NINI?
 
Moj
Moja ya kanisa Kongwe mnasema ni Cathoric? Unaweza tuambia lile chetezo ndani ya Kanisa nini? Je Maji ya Baraka ambayo kila mkatolik anayo kwenye nyumba yake nini?? Ulishawahi kuona Mkatolik akizindua Nyumba yake na akamualika Padre huwa ananyunyiza nini Kuzunguka nyumba yake? Kila kitu ni Imani Brother.. Kama vitu vingine huvijui ni bora kuacha ila elewa Watu wanteswa sana na hasa na watu kama ninyi kwa kuwa usiku mnakumbana na vizuizi vingi kama hivyo pale mnapokuta Nyumba imekingwa na Uwepo wa Nguvu za Kiungu ndiyo Maana Mnapinga sana
 
Minafuata biblia na sio mapokeo ya kanisa katoliki, mim natumia damu ya YESU au damu ya mwanakondoo na jina la YESU sio kitu kingine

Mim kutumia hivyo vitu vya upako kulikua na faida gani YESU kufa msalabani sababu hivyo vitu vya upako vimetumika sana agano la kale kumbuka sasahivi tupo agano jipya
 
ni Lini tuliambiwa Agano la Kale limefutwa na halipashwi kutumika tena kwenye mafundisho? Tupe muongo Mkuu
 
ni Lini tuliambiwa Agano la Kale limefutwa na halipashwi kutumika tena kwenye mafundisho? Tupe muongo Mkuu
Uelewa wako wa biblia ni mdogo na finyu hakuna sehemu nimesema agano la kale limefutwa Bali ni kuukuu na hii kauli aliitoa YESU, na huwez elewa tofauti ya agano jipya na kale sababu hujui somo la damu ya YESU, tunatakiwa tulisome agano la kale na kulielewa kupitia mtizamo wa damu ya YESU kumbuka damu ya YESU ilipomwagika pale msalabani ndo tulipata uhalali wa kutumia jina la YESU

Agano la kale limefungwa kwenye damu za mafahali nikimaanisha wanyama, na vitu vingine kama mafuta ya upako, chumvi na maji ya upako, huku agano jipya limefungwa kwenye damu ya YESU ambao kwa jina lingine ni damu ya mwanakondoo

Nikusaidie watumishi wa kisasa walio wengi hawawez promote matumizi ya Damu ya YESU na jina la YESU sababu hakuna money involve, Kwa hiyo lazima wapromote hivyo vitu vinavyoitwa vya upako sababu Kuna money involved
 
Ha ha ha ignorance is eating Africa my friend.
 
tunatakiwa tulisome agano la kale na kulielewa kupitia mtizamo wa damu ya YESU kumbuka damu ya YESU ilipomwagika pale msalabani ndo tulipata uhalali wa kutumia jina la YESU
Yesu mwenyewe alisema tazama ya kale yamepita. Hatupaswi kufuata missingi ya agano la kale ktk kuutafuta wokovu.

Yaani baada ya Yesu kufa pale msalabani na damu yake kumwagikw hatupaswi kuchinja wanyama tena ili kumtafuta Yeye.

Yesu ndiye maji, na damu yake iliyomwagika pale msalabani ndiyo jibu la wokovu wetu
 
Tatizo hivyo vitu havihushishi ela ndo sababu ya kuraise kwa hivyo vitu vinavyoitwa vya upako
 
Mtumishi unahudumu dhehebu Gani? Je unahudumu chini ya mti? kama unahudumu kwenye Jengo je mumelijengaje? nisaidie chanzo chenu cha mapato ni Damu ya Yesu? tunafundishana na kuelimishana tu.
 
Biblia ipi haina hivo vitabu?
 
Mtumishi unahudumu dhehebu Gani? Je unahudumu chini ya mti? kama unahudumu kwenye Jengo je mumelijengaje? nisaidie chanzo chenu cha mapato ni Damu ya Yesu? tunafundishana na kuelimishana tu.
Sadaka zimeorodheshwa kwenye biblia, kuuza mafuta ya upako, maji ya upako, chumvi ya upako hakuna mstari biblia unasema waumin wauziwe mfano samwel alitumia mafuta ya upako kama kuwaweka wakfu wafalme sauli na daudi, same kwa Elisha alimtuma mtu akampake yehu mafuta hajawa mfalme lakin hawakuyatumia kama mtaji wa biashara kama wafanyavyo watumishi wa mungu wa sahivi

Ukienda kwa baadhi ya watumishi wa Leo wanauza maji ya upako sh 1000 neema ya Mungu haiuzwi, assume zile nguvu za YESU wangekua nazo watumishi wa Leo wangezitumia vibaya sana
 
Vipi ushapata kazi lakini??

#MaendeleoHayanaChama
 
Acha roho mbaya yani kwa maisha haya ya usasa afanyie bure..unadhani hiyo ministry ingesimama..mngemlipa hela ya kukodi hapo tanganyika pekaz...ungemlipia bili za umeme..unhemlipia vyombo vya miziki..usafi..usafirishaji..na mahubiri kwa njia za redio na tv.??

Ebu tumia akili kidogo..Yesu mwenyewe alihitaji fedha hadi akawepo mtunza fedha mzee yuda.

#MaendeleoHayanaChama
 
Samwel na elisha walitumia tu mafuta ya upako pale walipokua wanataka kuwapaka mafuta wafalme huwez ona sehemu nyingine wakitumia, ni tofauti leo Kuna huduma ya kutumia zana za upako kama mafuta ya upako ambazo kwenye huwez Kuta kitu kama hicho
 
Me sijui kama jamaa ni mkweli au vipi na wala sitaki kujua ila Tu nachojua Mie ata kabla yake tuliwahi kuona watu na namna yake

Alitokea babu wa Loliondo, watu walisafiri umbali mrefu Kwa ajili ya kwenda kutatua shida zao, na wengine ilisadikika walifanikiwa na wengine hawakufanikiwa

Alikuwepo Kakobe, enzi zake walitoka mikoani na kulipia pesa nyingi sana ili tu waonane nae na kuwatatulia shida zao, na wengine walitatuliwa na wengine hawakufanikiwa

Akaja mwakasege nayeye akawa hodari kwa njia zake na namna zake na wengi wakamwamini na kuambatana nae hadi pale walipoona mambo hayaendi tena

Sasa hivi yupo bwana Bulldozer, nayeye yupo kwenye ubora wake kabisa kama waliomtangulia walivokuwa, wapo wanaosema amewasaidia na wapo ambao wanasema bado labda zamu yao bado haijafika

Hao ni wachache ambao karibia kila mtu anawajua, ila wapo wengi ambao walivuma na kupotea

Kwahiyo kuliko leo kukaa kuwa mtetezi kama wale waliokuwa enzi za Kakobe ni kheri ukaupa muda useme ukweli, kama Una shida zako nenda kasaidiwe ubakie na ushuuda wako moyoni na sio kufata mkumbo wa kwenye TV/maredio na magazeti

Kama nawewe ni mpondaji kama walivokuwa wale wa Enzi za Mzee wa Loliondo basi nawewe inatosha, uliyosema tumeyaskia na tutakusifu endapo utaonekana ulikuwa sahihi siku za usoni

Habari za watu kutapika viwembe,kujisaidia hirizi,kutoa paka juu ya dari,kumwaga maji na nyoka kutoka ndani,kumwaga maji na Panya kufa na mengine mengi kama hayo,Kwa Akili ya bila kushikiwa hiki hakiwezi kuwa kipimo cha unabii wa mtu

wote tulikuwa mashuuda wa kipindi kile mganga wa kujiita Dr manyau manyau anapita nyumba Kwa nyumba kutoa uchawi na alikuwa anayafanya haya Live mbele ya chaneli ya EATV mchana kweupe watu wamejaa, kwahiyo katika hayo na yafananayo na hilo hakuna jipya tushaona hadi waganga na wafanya mazingaombwe wanafanya

Kwahiyo kama kuna mtu atasimama na kumtetea kwamba jamaa atakuwa mtumishi wa kweli kwakuwa anafanya Mambo kama hayo ya kutoa kutapisha hirizi basi Akili zake zitakuwa haziko sawa sawa maana huku mitaani tumeyaona sana kwenye mazingaombwe

Una shida zako unaamini mwamposa anaweza kukusaidia we nenda tu mkuu Acha kuwa chawa wake mwache ajitetee mwenyewe Kwa Mungu wake na kupitia Mungu ata waliomkataa watamkubali

maana uchawa wako hamsaidii chochote mwamposa Kwa alipofikia hivi sasa, mwenzio kafikia hatua ya kuingiza Zaidi ya 50M Kwa siku ambayo haina ata Kodi za TRA mwenzangu namie unategemea ukakanyage mafuta ndio upate Ajira ya Mama Samia uambulie laki 5 Kwa Mwezi

Na wewe kama Huamini kuhusu huduma za Mwamposa we piga kimya endelea na mishe zako na nenda zako Kwa unaowaamini sio kumponda tu kijana wa watu alieamua kutumia fursa vizuri, mwisho wa siku utaonekana una chuki na mafanikio yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…