Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?
Sent from my SM-J700H using
JamiiForums mobile app