Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Nakubaliana na wewe mtumishi kwa Hilo. Kanisa limekosa watu wenye nguvu ya kutoa pepo. Nadhani hili tatizo linatokana na malezi ya kiroho au Nani aliwapa msingi wa kiroho walipookoka. Wengi hawajajua principles za Mungu za kupata nguvu ya kutoa pepo wachafu.

Ukisoma Marko 9:19 Hata wanafunzi wa Yesu walishindwa kutoa pepo Yesu akawafokea. Na kuwaambia mambo mengine hayawezekani Bali kwa kufunga na kuomba. Hii inamaanisha kwamba nguvu za Mungu aliye hai zinapatikana kwa kufunga na kuomba ambacho watumishi wengi hawawezi.

Pia, ili kutoa pepo inategemea nguvu ulizonazo na nguvu za pepo. Kama pepo lina nguvu kukuzidi basi huwezi kulitoa. Wengi tunakemea pepo wakati nguvu zetu kwenye ulimwenguni wa roho ni kidogo Sana. Yesu alikuwa na nguvu nyingi ndio maana Pepo walikuwa wanatii na kukimbia au mengine kuomba sehemu ya kukimbilia, maana alifunga siku 40 hivyo alipata nguvu kubwa Sana kuliko yeyote yule.
Sio tu kufunga siku arobain, Ile ratiba ya YESU ya maombi ni funga kazi most of time alikua anakesha akiomba alone zile nguvu za YESU hazikuja kwa granted

Kabla Mungu hajakupa nguvu zake anaangalia moyo wako, usiwe na kiburi hakuna kitu kigumu kama Mungu kukupa nguvu zake, shetani anakupa tu hajali
 
Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Hapa umeprove kabisa kwamba Mwamposa ni nabii wa kweli maana aliona shida yako
 
huyu ndugu ninamfahamu tangia akiwa kijana alipotoka tukuyu safari yake ya huduma kabla hajafahamika ilianzia tunduma akiwa na sambamba na mchungaji efraim mwaitebele wa kanisa la restoration bible church tunduma ,alikuwa mpenda maombi sana hasa ya kwenda milimani, alikuwa anafanyabiashara pale soko la black tunduma amewahi kuuza viatu pia, kwa sisi vijana wa kipindi kile maombi mengi tulikuwa tunafanyia milimani,mwamposa alikuwa kiongozi wa maombi nawakumbuka vijana kama pasta mwankenja ambae kwa sasa ni mchungaji kitunda tulikuwa nao pamoja .badae alipata wito akawa anaalikwa sehemu mbalimbali kanisa lake kubwa na mahali watu walianza kumjua ni moshi ,pale jamaa alipiga kazi sana na alikuwa na waumini wengi mno sikuwahi fikiria kama angehama moshi.inasemekana badae ilitokea migogoro flani ya kifamilia kati yake na mke wake,mwamposa aliamua kuondoka moshi kwa hasira na kuamua kwenda dar kuanza huduma upya.haikuwa kazi rahisi maana alikuwa hana hata mahali pakufanyia huduma,alianzia sebulen kwa mtu akiwa n
We kweli unamjua maana kipande kimojawapo ulichokiongelea na mm nakifahamu na sio kuhadithiwa
 
Basi yule jamaa ni mshirikina kwa taarifa yako. Anapopanda gari baada ya ibada huwa anavua nguo zote na kubaki na boksa tu huku wapambe na walinzi wake wakiwa wamemzunguka.

Ndiyo maana ninyi waumini wake hamjawahi kumuona akipanda gari lake baada ya ibada. Uliza kila mmoja atakuambia hajawahi kumuona

Na wakati wa kushuka anapoingia ibadani huwa mikonoo yakoe inakuwa mfukoni alikoweka hirizi.
UONGO UNAKUSAIDIA NINI?
 
Moj
Kuna Mzee kila usiku saa nne sio Mara zote ni baadhi ya siku utamkuta na maji ya upako ya mwamposa anamwaga kwenye ukuta wake swali ambalo najiuliza kwanin asitumie jina la YESU au damu ya YESU kukilinda nyumba, inamaana anaamin maji ya upako kuliko damu ya YESU ukishaona hivyo uju Kuna shida mahali kubwa sana

Lengo la shetani ni kuhakikisha wakristo hawatumii either jina la YESU au damu ya YESU na watumia vitu vingine, kwa shetani hakuna vitu ambavyo ni tishio kama jina la YESU au damu ya YESU na mpaka sahivi ameshafanikiwa pakubwa sana

Mafuta ya upako na vitu vingine vyote vyenye jina la upako havina tofauti na mtu anayeabudu sanamu
Moja ya kanisa Kongwe mnasema ni Cathoric? Unaweza tuambia lile chetezo ndani ya Kanisa nini? Je Maji ya Baraka ambayo kila mkatolik anayo kwenye nyumba yake nini?? Ulishawahi kuona Mkatolik akizindua Nyumba yake na akamualika Padre huwa ananyunyiza nini Kuzunguka nyumba yake? Kila kitu ni Imani Brother.. Kama vitu vingine huvijui ni bora kuacha ila elewa Watu wanteswa sana na hasa na watu kama ninyi kwa kuwa usiku mnakumbana na vizuizi vingi kama hivyo pale mnapokuta Nyumba imekingwa na Uwepo wa Nguvu za Kiungu ndiyo Maana Mnapinga sana
 
Minafuata biblia na sio mapokeo ya kanisa katoliki, mim natumia damu ya YESU au damu ya mwanakondoo na jina la YESU sio kitu kingine

Mim kutumia hivyo vitu vya upako kulikua na faida gani YESU kufa msalabani sababu hivyo vitu vya upako vimetumika sana agano la kale kumbuka sasahivi tupo agano jipya
 
ni Lini tuliambiwa Agano la Kale limefutwa na halipashwi kutumika tena kwenye mafundisho? Tupe muongo Mkuu
 
ni Lini tuliambiwa Agano la Kale limefutwa na halipashwi kutumika tena kwenye mafundisho? Tupe muongo Mkuu
Uelewa wako wa biblia ni mdogo na finyu hakuna sehemu nimesema agano la kale limefutwa Bali ni kuukuu na hii kauli aliitoa YESU, na huwez elewa tofauti ya agano jipya na kale sababu hujui somo la damu ya YESU, tunatakiwa tulisome agano la kale na kulielewa kupitia mtizamo wa damu ya YESU kumbuka damu ya YESU ilipomwagika pale msalabani ndo tulipata uhalali wa kutumia jina la YESU

Agano la kale limefungwa kwenye damu za mafahali nikimaanisha wanyama, na vitu vingine kama mafuta ya upako, chumvi na maji ya upako, huku agano jipya limefungwa kwenye damu ya YESU ambao kwa jina lingine ni damu ya mwanakondoo

Nikusaidie watumishi wa kisasa walio wengi hawawez promote matumizi ya Damu ya YESU na jina la YESU sababu hakuna money involve, Kwa hiyo lazima wapromote hivyo vitu vinavyoitwa vya upako sababu Kuna money involved
 
Nilianza kumsikia akiwa Vatican sinza bar, hii ni maarufu kipindi enzi zetu tunasoma,
Siku moja nimetoka arusha nikasema ngoja nikapate biere baridi moja nikashangaa hakuna bar kuna Injili inapigwa kuulizia somebody Mwamposa nikasema haleluya.

Ila Aache mazingaombe kutapika nyembe na mende,kunya hirizi na shanga
Ha ha ha ignorance is eating Africa my friend.
 
tunatakiwa tulisome agano la kale na kulielewa kupitia mtizamo wa damu ya YESU kumbuka damu ya YESU ilipomwagika pale msalabani ndo tulipata uhalali wa kutumia jina la YESU
Yesu mwenyewe alisema tazama ya kale yamepita. Hatupaswi kufuata missingi ya agano la kale ktk kuutafuta wokovu.

Yaani baada ya Yesu kufa pale msalabani na damu yake kumwagikw hatupaswi kuchinja wanyama tena ili kumtafuta Yeye.

Yesu ndiye maji, na damu yake iliyomwagika pale msalabani ndiyo jibu la wokovu wetu
 
Tatizo hivyo vitu havihushishi ela ndo sababu ya kuraise kwa hivyo vitu vinavyoitwa vya upako
 
Uelewa wako wa biblia ni mdogo na finyu hakuna sehemu nimesema agano la kale limefutwa Bali ni kuukuu na hii kauli aliitoa YESU, na huwez elewa tofauti ya agano jipya na kale sababu hujui somo la damu ya YESU, tunatakiwa tulisome agano la kale na kulielewa kupitia mtizamo wa damu ya YESU kumbuka damu ya YESU ilipomwagika pale msalabani ndo tulipata uhalali wa kutumia jina la YESU

Agano la kale limefungwa kwenye damu za mafahali nikimaanisha wanyama, na vitu vingine kama mafuta ya upako, chumvi na maji ya upako, huku agano jipya limefungwa kwenye damu ya YESU ambao kwa jina lingine ni damu ya mwanakondoo

Nikusaidie watumishi wa kisasa walio wengi hawawez promote matumizi ya Damu ya YESU na jina la YESU sababu hakuna money involve, Kwa hiyo lazima wapromote hivyo vitu vinavyoitwa vya upako sababu Kuna money involved
Mtumishi unahudumu dhehebu Gani? Je unahudumu chini ya mti? kama unahudumu kwenye Jengo je mumelijengaje? nisaidie chanzo chenu cha mapato ni Damu ya Yesu? tunafundishana na kuelimishana tu.
 
Mkuu huwa kila Mwaka ukianza naweka nadhiri ya Kusoma Biblia kuanzia Kitabu cha Mwanzo hadi Kitabu cha Mwisho cha Agano Jipya tena sisomi Hizi Biblia ambazo zimetoholewa ambapo vitabu kama Ezra, Esta,Yobu,Yoeli,Amosi, Obadia, Nahumu,Zephania,Haggai na Malachi havina....

Kwa hiyo usiseme tupo shallow.....
Biblia ipi haina hivo vitabu?
 
Mtumishi unahudumu dhehebu Gani? Je unahudumu chini ya mti? kama unahudumu kwenye Jengo je mumelijengaje? nisaidie chanzo chenu cha mapato ni Damu ya Yesu? tunafundishana na kuelimishana tu.
Sadaka zimeorodheshwa kwenye biblia, kuuza mafuta ya upako, maji ya upako, chumvi ya upako hakuna mstari biblia unasema waumin wauziwe mfano samwel alitumia mafuta ya upako kama kuwaweka wakfu wafalme sauli na daudi, same kwa Elisha alimtuma mtu akampake yehu mafuta hajawa mfalme lakin hawakuyatumia kama mtaji wa biashara kama wafanyavyo watumishi wa mungu wa sahivi

Ukienda kwa baadhi ya watumishi wa Leo wanauza maji ya upako sh 1000 neema ya Mungu haiuzwi, assume zile nguvu za YESU wangekua nazo watumishi wa Leo wangezitumia vibaya sana
 
Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Vipi ushapata kazi lakini??

#MaendeleoHayanaChama
 
Nabii wa KWELI wa MUNGU hutenda miujiza kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU aliyepewa na MUNGU na siyo kwa uwezo wa "mafuta" au "keki" au kitu chochote kile. Tena siyo yeye anayetenda bali ni YULE ROHO wa MUNGU akaaye ndani yake.

Na huduma hiyo hutolewa bure kabisa bila malipo yoyote. YESU KRISTO alisema : "mmepewa bure, toeni bure". Na ndivyo akina Petro na mitume wengine walifanya zamani zile.

Huyo Mwamposa hana ROHO MTAKATIFU. Mwamposa ni mfanyaMAZINGAOMBWE anayetumia jina la YESU KRISTO kama kivuli.
Acha roho mbaya yani kwa maisha haya ya usasa afanyie bure..unadhani hiyo ministry ingesimama..mngemlipa hela ya kukodi hapo tanganyika pekaz...ungemlipia bili za umeme..unhemlipia vyombo vya miziki..usafi..usafirishaji..na mahubiri kwa njia za redio na tv.??

Ebu tumia akili kidogo..Yesu mwenyewe alihitaji fedha hadi akawepo mtunza fedha mzee yuda.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu kiongozi wa Mkristo ni biblia.
Hakuna mahali chumvi ilirudiwa kutumia mara kwa mara au mafuta.

Kila kitu huwa ni ufunuo na hutumika mara moja tu.

Unapotumia mara kwa mara au kusisitiza matumizi yake tayari hiyo ni imani potofu uliyoijengea imani.

Wakristo tuweni na akili na tuwe makini kujifunza neno kwani tunapoteza muda kwa vitu visivyo vya imani sahihi.

Haya maigizo ni upepo wa muda hautusaidii kitu.

Lengo kuu la Mungu ni mwanadamu kukombolewa dhambini na sio muujiza.

Muujiza ni msaada wa dharura lakini ukristo ni maisha ya mwamini kuuendea uzima wa milele.

Hadi lini tutakuwa watoto tukichukuliwa na kila upepo?

Maigizo haya yalianza kitambo enzi za biblia walikuwepo akina Simioni mchawi
Samwel na elisha walitumia tu mafuta ya upako pale walipokua wanataka kuwapaka mafuta wafalme huwez ona sehemu nyingine wakitumia, ni tofauti leo Kuna huduma ya kutumia zana za upako kama mafuta ya upako ambazo kwenye huwez Kuta kitu kama hicho
 
Me sijui kama jamaa ni mkweli au vipi na wala sitaki kujua ila Tu nachojua Mie ata kabla yake tuliwahi kuona watu na namna yake

Alitokea babu wa Loliondo, watu walisafiri umbali mrefu Kwa ajili ya kwenda kutatua shida zao, na wengine ilisadikika walifanikiwa na wengine hawakufanikiwa

Alikuwepo Kakobe, enzi zake walitoka mikoani na kulipia pesa nyingi sana ili tu waonane nae na kuwatatulia shida zao, na wengine walitatuliwa na wengine hawakufanikiwa

Akaja mwakasege nayeye akawa hodari kwa njia zake na namna zake na wengi wakamwamini na kuambatana nae hadi pale walipoona mambo hayaendi tena

Sasa hivi yupo bwana Bulldozer, nayeye yupo kwenye ubora wake kabisa kama waliomtangulia walivokuwa, wapo wanaosema amewasaidia na wapo ambao wanasema bado labda zamu yao bado haijafika

Hao ni wachache ambao karibia kila mtu anawajua, ila wapo wengi ambao walivuma na kupotea

Kwahiyo kuliko leo kukaa kuwa mtetezi kama wale waliokuwa enzi za Kakobe ni kheri ukaupa muda useme ukweli, kama Una shida zako nenda kasaidiwe ubakie na ushuuda wako moyoni na sio kufata mkumbo wa kwenye TV/maredio na magazeti

Kama nawewe ni mpondaji kama walivokuwa wale wa Enzi za Mzee wa Loliondo basi nawewe inatosha, uliyosema tumeyaskia na tutakusifu endapo utaonekana ulikuwa sahihi siku za usoni

Habari za watu kutapika viwembe,kujisaidia hirizi,kutoa paka juu ya dari,kumwaga maji na nyoka kutoka ndani,kumwaga maji na Panya kufa na mengine mengi kama hayo,Kwa Akili ya bila kushikiwa hiki hakiwezi kuwa kipimo cha unabii wa mtu

wote tulikuwa mashuuda wa kipindi kile mganga wa kujiita Dr manyau manyau anapita nyumba Kwa nyumba kutoa uchawi na alikuwa anayafanya haya Live mbele ya chaneli ya EATV mchana kweupe watu wamejaa, kwahiyo katika hayo na yafananayo na hilo hakuna jipya tushaona hadi waganga na wafanya mazingaombwe wanafanya

Kwahiyo kama kuna mtu atasimama na kumtetea kwamba jamaa atakuwa mtumishi wa kweli kwakuwa anafanya Mambo kama hayo ya kutoa kutapisha hirizi basi Akili zake zitakuwa haziko sawa sawa maana huku mitaani tumeyaona sana kwenye mazingaombwe

Una shida zako unaamini mwamposa anaweza kukusaidia we nenda tu mkuu Acha kuwa chawa wake mwache ajitetee mwenyewe Kwa Mungu wake na kupitia Mungu ata waliomkataa watamkubali

maana uchawa wako hamsaidii chochote mwamposa Kwa alipofikia hivi sasa, mwenzio kafikia hatua ya kuingiza Zaidi ya 50M Kwa siku ambayo haina ata Kodi za TRA mwenzangu namie unategemea ukakanyage mafuta ndio upate Ajira ya Mama Samia uambulie laki 5 Kwa Mwezi

Na wewe kama Huamini kuhusu huduma za Mwamposa we piga kimya endelea na mishe zako na nenda zako Kwa unaowaamini sio kumponda tu kijana wa watu alieamua kutumia fursa vizuri, mwisho wa siku utaonekana una chuki na mafanikio yake
 
Back
Top Bottom