Hayo ni kweli lakini Yale SIO mafuta ya upako ni mafuta yanayotengenezwa kwa formula za kushirikina.
Na zinajukana . MTU yeyote anaweza kuyanunua Kwa maustadhi na yanafanya KAZI Kwa Hiyo SIO upako Wa Kikristo Bali ni mchanganyiko Wa mitishamba kama Dawa nyingine za kisuna. KUWADANGANYA watu Kuwa ni upako Wa Roho Wa MUNGU ni kupotosha na kumwandolea MUNGU sifa za Upekee.
Natamani kuwaambia ukweli Wakristo wenzangu mana wamepotoka sana. Uliona Mashekhena ubwabwa wameenda kumuunga mkono Nabii Mkuu . Ni Muislam Gani anayekubali Kuwa kuna Nabii mwingine baada ya Nabii Mohamad (SAW)? Wale ni wataalam Wa Dawa za Kisuna wanajua Kuwa zipo Dawa za Kisuna na za majini zinazotumiwa kutibu Kwa uwezo Wa Allah MTU akapona mana Kila kitu alikiumba yeye na akaumba Dawa za Kila Ugonjwa Katika miti aliyoiumba ?
Nikuulize Swali ?
Hiví Unaonaje kama Madaktari Wa Muhimbili wangesema Kuwa tunatibu Kwa Jina la Yesu ! Njooni Juma Pili mlete wagonjwa wenu WOTE waliovuniika miguu ,wenye matatizo ya macho tuna macho ya KIROHO,macho ya upako Yaani miwani. Wakati huo binadam wawe hawajapata elimu Juu ya sayansi rasmi ya tiba ? Je, watu wasingefurika Muhimbili nakujua Kuwa ni Imani ya Kikristo kutibu Kumbe ni sayansi ya Kigiriki na Kirumi ?
Kwa Sasa Imani zimegubikwa na Sayansi ya Kale ya MISRI .
Wayahudi wamegubikwa na Sayansi ya Kimisri ikiwemo Mussa Aliyekulia Kwa Faraoh kama Mtoto Wa Mfalme. Mussa alijua sayansi na ushirikina WOTE mana alikulia NDANI ya Ikulu ya Faraónh Lakini aliuacha akamwamini MUNGU Mmoja na Kupinga Imani za kishirikina . Waisraeli wengi walijua mbinu za wamisri za kishirikina lakini walikua wanaamrishwa waepukane nazo na wakawa wanatungiwa Sheria Kali sana kuachana nazo.
Musa alichelewa kurudi Toka mlimani Siku 40 tu Waisraeli wakaanza ibada za Sanamu Kwa kuchonga Sanamu ya Ng'ombe na kuiabudu.
MANABII WENGI WANATAMANI MIUJIZA LAKINI HAWATAIPEWA KAMWE NA MUNGU ANAACHA MAKUSUDI ILI KUWAJUA WATU WAKE HALISI. SASA WENGI WANAPOONA MUNGU ANACHELEWA KUJIBU MAOMBI YAO YA MIUJIZA WANAAMUA KUCHONGA SANAMU ZA NG'OMBE YAANI VITAMBAA ,MAFUTA ,KEKI, CHUMBI N.K. HIZI NI IBADA ZA WAMISRI. NA MPAKA LEO KULE MISRI KUNAVYUO VYA KICHAWI LAKINI KWA SABABU WANAFUNDISHA KWA KIARABU BASI WATU WANAJUA KUWA NI VYA KIDINI HIVYO KUNA WATU WENGI WANASOMEA KULE NA WANAJUA FOMRULA NYINGI ZA DAWA ZA KUONA ,KUFUGA NA KUTOA MAJINI. NDIZO WANAZOWAPA MANABII NA MAKRISTO WA UONGO WALIOCHOKA KUOMBEA KWA JINA LA YESU BILA MAFUTA NA KUONA KUWA WANATUMIA NGUVU KUBWA SANA KUOMBA NA HAKUNA MUUJUZA WALA NINI.
MAFUTA ni Ibada ya Sanamu.
YESU alimpaka MTU matope machoni kama Dawa lakini na kumwambia Kuwa Imani yake imemponya. Ile ilikuwa ni Dawa tu kama Panadol . Hakusema Kuwa ni matope ya upako.
Someni Vitabu .