Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

Jamaa huyu ana PhD ya kiburi na majivuno!! Mama toa hii jamaa kabla hajakuumiza mwenyewe!! Sidhani kama anakuheshimu!! Ukifuga nyoka ukaona anauma wengine usidhani kuwa wewe uko salama!! Ni suala la muda tu, akipata nafasi atakung'ata!!
 
Dah, haya maneno si dharau tu kwa wananchi bali hata rais wetu alizuru Burundi. Hivyo kauli hii Mwigulu anamaanisha rais wetu atokomeee uko huko Burundi kwa vile tu nae ameungana na wananchi kwa kusema tozo hizo ziangaliwe upya kwa maana ya kwamba hajakubaliana nazo pi.
Haya ni maneno ya dharau na kiburi kikubwa sana sijui wapiga kura wake hayo mafuta wanauziwa tsh. Ngapi maana alivyo ongea utadhani ubunge wake ni wakuteuliwa hivyo hajali, au hana mpango wa kugombea tena maana anaamini 2025 atakuwa Rais
 
watu wamepunguza kufanya miamala na hivyo alichotarajia kukikusanya hatakipata - bado anasema uchumi hautaathirika. Haoni kama kodi alizokuwa akipata kutoka kwenye faida ya kampuni za simu inaenda kupungua - Musukuma chapa sana hawa wasomi wa ajabu ajabu! (huu ni u dr. wa makaratasi tu)

Na hii kauli ya kuhamia Burundi, haina tofauti na ile ya kula majani lakini ndege ya rais inunuliwe -Basil Mramba

Kama kuna mtu alisikiliza mchango wa Kimei kwenye bajeti ataelewa kwa nini uchumi utaathirika, Huyu ni mtu ambaye practically amekuza CRDB kwa vitendo, msikilize na alichokisema juu ya tozo za simu ndicho kinatokea sasa!

Usiwe kenge wewe ,kabla ya kuweka makisio ya fedha analysis ilifanywa yote haya yalitarajiwa.

Kwa mfano hata watu wapungue kwa asilimia 30% still hiyo 70% inayobakia inaweza kuipa serikali zaidi ya Tilioni 1..

Wale watakao pungua nusu yao wataenda benki na kwa hiyo kodi iyakayotokana na faida ya benki na gawio itafidia kiwango cha VAT kitakachopungua kutokana na ile 30% .

Hali hii pia ni ya mda mfupi maana wateja wanaongezeka,kwa hiyo Mwigulu yuko sahihi kwenye tozo.

Hayo mawazo ya huyo mbunge uliyemuweka hapo juu yataishia kuwa mawazo lakini hayaathiri mwenendo wa uchumi.Tatizo lenu hamjui uchumi na mnaishi kwa hisia.

Mwigulu na Mpango ni wataalamu wa uchumi na Kimei na mtaalam wa usimamizi wa biashara.

Kuna sera za mda mfupi na sera za mda mrefu,as per Kimei anapendelea kukopa zaidi.
 
Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

Tulikubaliana sisi siyo wanyonge. Hii kulalamika inatoka wapi?
 
Usiwe kenge wewe ,kabla ya kuweka makisio ya fedha analysis ilifanywa yote haya yalitarajiwa.

Kwa mfano hata watu wapungue kwa asilimia 30% still hiyo 70% inayobakia inaweza kuipa serikali zaidi ya Tilioni 1..

Wale watakao pungua nusu yao wataenda benki na kwa hiyo kodi iyakayotokana na faida ya benki na gawio itafidia kiwango cha VAT kitakachopungua kutokana na ile 30% .

Hali hii pia ni ya mda mfupi maana wateja wanaongezeka,kwa hiyo Mwigulu yuko sahihi kwenye tozo.

Hayo mawazo ya huyo mbunge uliyemuweka hapo juu yataishia kuwa mawazo lakini hayaathiri mwenendo wa uchumi.Tatizo lenu hamjui uchumi na mnaishi kwa hisia.

Mwigulu na Mpango ni wataalamu wa uchumi na Kimei na mtaalam wa usimamizi wa biashara.

Kuna sera za mda mfupi na sera za mda mrefu,as per Kimei anapendelea kukopa zaidi.
Huyu maza mnampotosha wapuuzi nyie
 
Mimi namuelewa sana Mwigulu, huu ni mpango maalumu wa kuizika ccm endapo SSH hatolitambua hili! Na Mimi naomba Mwigulu aongeze zaidi ujinga ili kila mtanzania tukimwambia tunahitaji mabadiliko ya kimfumo katika utawala iwe rahisi kueleweka! Mwigulu hayupo kabisa upande wa Mama na yeye mwenyewe anahitaji CCM ifikie ukomo!
 
Sasahivi wataamka hakuna namna
 
....
IMG-20210720-WA0017.jpg
 
Haya ni maneno ya dharau na kiburi kikubwa sana sijui wapiga kura wake hayo mafuta wanauziwa tsh. Ngapi maana alivyo ongea utadhani ubunge wake ni wakuteuliwa hivyo hajali, au hana mpango wa kugombea tena maana anaamini 2025 atakuwa Rais
Nani alimpigia kura? huyu alipitishwa na tume ya Mahera
 
Jamaa huyu ana PhD ya kiburi na majivuno!! Mama toa hii jamaa kabla hajakuumiza mwenyewe!! Sidhani kama anakuheshimu!! Ukifuga nyoka ukaona anauma wengine usidhani kuwa wewe uko salama!! Ni suala la muda tu, akipata nafasi atakung'ata!!
Ndiyo mshauri wake eti
 
Huyu Waziri Amejizila Kabisa
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Mfute Kazi Haraka
UVCCM Chali!! Yaani Anatudharau Waajiri
 
Back
Top Bottom