Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!hata hivo hii ya Mwigulu ni kuanguka na si kuteleza.Ieleweke kwamba mbinu zinazofanywa na Mwigulu na chama chake hayana tija kuwakomaza kisiasa na kuwapa uhalali wa kuongoza nchi hii kamwe.CHADEMA iuwe watu kwa lipi hasa?CHADEMA inamaslahi gani na kuua watu na kwa kutumia nini?Hayo mafunzo waliyafuzia wapi na slaha hizo wanazitoa wapi au na wenyewe hutengewa bajeti kuingiza slaha nchini?
haswaaaa huyo spka namchukia mbaya
Mwigulu na CCM wako tayari kuivuruga hii nchi ili waendelee kutawala!Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo.
Watanzania wanaangalia Bunge, wanajua Bunge linavyoendeshwa. Wanajua Spika unavyofanya, wanaona Unavyopendelea. CCM mmeshangilia sana, hongereni. Mlianza na Udini wa CUF na sasa wa CHADEMA, Mkaja Ukatoliki wa Slaa, na Uchaga wa CHADEMA.
Mlijaribu Udini suala la Kuchinja limepata busara ya Mwinyi tumepata nafuu ya siku moja. Sasa la Kuchakachua Katiba kunakoendelea mtaani sasa, na kuruhusu ujinga Bungeni kuipendelea CCM kutukana........... mnaharakisha kupeleka nchi kusikovutia wengi.
Wabunge wa TZ wanapoteza muda mwingi kujibizana kuliko kujadiri hoja.. Mh Nchemba amenisikitisha sana maana ameidharau mahakama na amevunja kanuni za bunge huku spika akisema "mkuki kwa nguruwe"😡
Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale iwe polisi, mahakamani bungeni hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, na kwamba kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari kuthibitisha mahali popote. Amewataka viongozi wa chadema wasitafute mchawi kwa kusingizia vyombo vya dola hasa polisi na usalama wa taifa kwamba vinahusika.
Amesema ni vyema viongozi wa chadema popote pale walipo waende kwenye nyumba za ibada zilizopo karibu nao wakatubu na kuungama kujisafisha na matendo maovu ya kigaidi na mauaji wanayoyafanya. amewashangaa kutaka madaraka huku wanawaua wananchi wanaotaka kuwaongoza...awaambia shame on you, look at you chadema!!!!!
Amesema ile ya chadema iliyowasilishwa na mbowe ilikuwa ni malalamiko ya kambi ya upinzani na sio hotuba ya kambi ya upinzani kwa kuwa haina mapendekezo wala solution ya matatizo pamoja na kwamba ina urefu wa kurasa 70.
Amelitaka jeshi la polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE kwa kuwa ni mkurugenzi wao wa ulinzi na usalama, kufuatia maelezo ya mbowe jana kwamba anayewasiliana na gaidi naye ni gaidi pia hivyo akamatwe..
Huyu Mwigulu anajitafutia mwisho mbaya kisiasa.
Nimemsikia Nchemba alivyokuwa akiongea, katika hali ya kawaida, Nilitegemea Lukuvi angasemama na kusema kuhusu utaratibu, sikumsikia. Mbaya zaid Spika akanogewa na utamu wa mada aliyokuwa akiiwakilisha Mwigulu akaruhusu Mwigulu akamaliza matusi yote tena kwa kutaja jina-Lukuvi anasemaga kanuni zinakataza kabisa, kutaja jina la mtu kwa dhihaka.
Spika ameombwa atoe utaratibu kuhusu kitendo hicho cha kumruhusu Mwigulu kuvunja kanuni, Spika kasema kwa kuwa jana alimruhusu Mbowe asome na amalize speech yake iliyojaa lugha kama alizotumia Mwigulu ndo mana leo kamruhusu Mwigulu, ila baada ya tukio hili la Mwigulu, wabunge wote sasa waobserve kanuni. Huu ni upuuzi kabisa!
Kama Spika aliona Mbowe anapotoka kwanini hakumzuia na kumtaka afute kauli??? Inaleta tija gani kuona mbunge anaenda nje ya mstari then unamuacha ili uruhusu baadaye mbunge mwingine aje kuvunja kanuni ili kurevenge?? Uendeshaji huu wa bunge hautatufikisha mahali.
Mwigulu na CCM wako tayari kuivuruga hii nchi ili waendelee kutawala!