Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

We Mwanamke una matatizo sana kwa kweli
Utakuwa na Stress tu
I am fine thank you for your concern.
Tunaweza kuendelea na hoja hii?
Au tuendelee kwanza kuongelea stress zetu?
 
Is the screw on Mwigulu(caught in this Lwakatare Video saga) becoming tighter or is he just a reckless talker? If at all you have evidence that can condemn some CHADEMA leaders to imprisonment for the so called "acts terrorism" why shout? Why not let the court do its work? By politicising this thing Mwigulu makes yet another mistake is the Court of Public Opinion. He has breached the delicate wall between the judiciary and the bunge. He has failed the test of infidelity to the constitution of the United Republic of Tanzania that provides for separation of powers. In whom should the shame be on now? If the likes of Mwigulu is what comprise the CCM top brass, then this qualifies the prophets of doom opinion that CCM is hastening its way to bury itself. I am amazed of what has become of our leaders. How can you politicise such as "acts of terrorism".Do we really have leaders these days or just a bunch of cronies meant to serve the interests of the few? I really appreciate the "gusto" that Mwigulu Nchemba displays when making a presentation. That is so untill you hear the words come from his mouth. He really does a good job to discredit the audience appreciation of his zest and what he says. The disconect is between them like day and night. And you ask yourself was all that energy meant to put accross this kind of rubbish! I have nothing personal against Mwigulu Nchemba it is just that there are certain responbilities and a code of conduct that come with holding a public office. And Mwingulu being as vibrant and educated(not learned) as he is, seems to ignore that. That seems to pass above his head. Whether that is by design or deliberate,it is really appalling and distateful by any good governance standards.
 
mwigulu ndio njia yake pekee ya kutafuta usuper star!ila kumbuka kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho!
u super star unatafutwa kwa kutumia akili, sasa jemba linatumia nguvu nyingi busara kidogo lini utaupata u-super star katika siasa? tunawajua vijana waliotulia na wanafanya siasa kwa kujenga hoja za msingi na si kukurupuka kila siku mara livalishe mbwa bendera za chama pinzani, siasa za ki-analogue sana.
 
Jamani Great Thinkers kwanini Zitto Zitto asifunguke zaidi? unajua CCM inawapatia CDM maana wapo "fragmented sana" Leo kina Slaa, Mbowe, Lissu, Lema, Mnyika, etc wanakosa nguvu na nini cha kusema mbele ya Raia maana hawamwamini tena Zitto. Zitto ni mjenga hoja, ni mzungumzaji aliejaliwa na MUNGU. Ila anatulia wakati anafahamu fika waTz wanahisi nini kuhusu yeye....(mimi nikiwa miongoni mwao) . Kwamba; huenda akawa ni Ngazi yawabaya wa CDM kukifuatilia juu kilipo......AMEN ALELUYA.....TAKBIR_-_-_ALAH AKBAR
 
Mwigulu utakuja kungolewa meno bila ganzi, we endelea???
 
Hivi unajua kutoka na maelezo ya mwingulu nchemba si yeye aliyefichua huo anao huita mpango?

"nilipewa mkanda huo na kiongozi wa chadema anaye chukia maovu yanayo fanywa na chama chake- mwingulu" nani amefichua kati ya mwingulu na huyo kiongozi? Mbona hamtaki kumsifu huyo kiongozi mnamsifu mwingulu? Wakati mwingulu hajui chochote zaidi ya yeye alipewa mkanda(kutokana na maelezo ya mwingulu)

unajua kinachofanya watu wamjadili na kupatwa wasi wasi na mwingulu ni yeye kujivika jukumu kuwa yeye amefichua wakati alishasema amepewa huo mkanda na ndio hapo swali lina kuja kwa nini alipewa yeye mkanda na si kova?

Atongwele kwenye maelezo ya mwingulu alisema ana ushahidi wa finger print na barua ya maelekezo ya lwakatare! Umewai kujiuliza mwingulu alimpima saa ngapi lwakatare? Je hii issue ya finger print ameijulia wapi? Je polisi wanashirikiana na mwingulu na wanampa taarifa?

Watanzania tukae chini na kutumia bongo zetu. Haya Mahaba ya vyama vya siasa yataibomoa nchi. Huwezi kumlaumu mtu anayeharibu mipango ya Watu wa Giza.
 
Last edited by a moderator:
Nimemsikia Nchemba alivyokuwa akiongea, katika hali ya kawaida, Nilitegemea Lukuvi angasemama na kusema kuhusu utaratibu, sikumsikia. Mbaya zaid Spika akanogewa na utamu wa mada aliyokuwa akiiwakilisha Mwigulu akaruhusu Mwigulu akamaliza matusi yote tena kwa kutaja jina-Lukuvi anasemaga kanuni zinakataza kabisa, kutaja jina la mtu kwa dhihaka.

Spika ameombwa atoe utaratibu kuhusu kitendo hicho cha kumruhusu Mwigulu kuvunja kanuni, Spika kasema kwa kuwa jana alimruhusu Mbowe asome na amalize speech yake iliyojaa lugha kama alizotumia Mwigulu ndo mana leo kamruhusu Mwigulu, ila baada ya tukio hili la Mwigulu, wabunge wote sasa waobserve kanuni. Huu ni upuuzi kabisa!

Kama Spika aliona Mbowe anapotoka kwanini hakumzuia na kumtaka afute kauli??? Inaleta tija gani kuona mbunge anaenda nje ya mstari then unamuacha ili uruhusu baadaye mbunge mwingine aje kuvunja kanuni ili kurevenge?? Uendeshaji huu wa bunge hautatufikisha mahali.

Mkuu hivi unajua speaker ni mwanamke? kaamua kutuletea maamuzi yanayoshabihiana na jinsia yake tehetehe ......wakiwezeshwa wanaweza.
 
Mwigulu anasema atatoa ushahidi kwamba cdm inahusika na kupanga mauwaji....
Ana mpaka maandishi ya huyo alierekodi..
anasema CHADEMA iko kama mchawi..! kwamba inaloga alafu inakuwa wa kwanza kulia kilioni
Kwa nini Polisi hawajamkamata huyu anayetamba kuwa na ushahidi wa kila kitu kuhusu shauri hilo? Halafu anawapakazia kwelikweli polisi kuwa aliwapa huo mkanda mapema, na wao badala ya kuufanyia kazi wakasubiri hadi Kibanda alipoteswa ndo wakauweka youtube. Polisi,je ni hivyo? Kwa nini mlisubiri hadi Kibanda ateswe kwanza? Na kwa nini mlitumia njia ya kuuweka mtandaoni badala ya utaratibu wenu wa kukamata watuhumiwa na kuendesha upelelezi kwa kanuni zenu? Bila kumkamata jamaa huyu na kumhoji, tutaamini kuwa hata ninyi mlishiriki njama hiyo hatari!
 
Sasa kama yuko tayari kutoa ushahidi,tatizo likwapi?
Mwacheni akatoe popote anapotaka kama ni fake itajulikana tu.

ushahidi muhimu juu ya ugaidi afu autoe "anapopenda mwenyewe"...mbona unaleta mahaba ktk mambo mazito.
 
Ila jamaa ana maneno ya kuudhi, anamwambia mbowe unashangaa 0 kwani wewe mbowe ulipata div ngapi
 
hili jamaa uwelewa wake ni mdogo sana, atachukiwa sana na jamii kwa siasa zake za kipuuzi na kwa kwendo huu hatafika mbali kisiasa.

Wazee mkeemeeni kijana huyu maana ameivamia siasa kwa pupa.

Mbona Mwigulu ametoa challenge ya kutoa ushahidi na pia kumtaja kiongozo mmoja musicians wa CDM, ambaye pia yuko tayari kutoa ushahidi. Sasa hapo sioni ujinga wowote na sioni sababu za Mwigula ku huchukiwa na Watu Kama anaukweli wowote Utakao tuletea kujua hali halisi ya hi video. Ndugu hapa kina Mbowe na Slaa wane challengiwa so they have to counter challenge and come clean, au Kama hawawezi watafute namna ya kumyamazisha, otherwise atawaaibisha sana.
 
Bocho naomba utoe facts za tatizo la hiyo hotuba!

Nakupa kichekesho kimoja kwenye hotuba ya mwenyekiti wako Mbowe jana:

Anasema watanzania waliotoa maoni kwenye tume ya katiba ni asilimia 0.7% ya watanzania wote! Hiyo asilimia imekokotolewa na wasomi wa CHADEMA kwa kuchukua idadi ya watanzania wote milioni 45.

Swali la msingi: CHADEMA ilitegemea mpaka watoto watoe maoni kwenye katiba mpya?

Ukiweza unaweza kumsaidia mwenyekiti wako kujibu mantiki ya hiyo asilimia.

Kwangu mimi ni kichekesho kitupu kwa wasomi wa CHADEMA kuweka pumba kama hizi kwenye hotuba zao.
 
ushahidi muhimu juu ya ugaidi afu autoe "anapopenda mwenyewe"...mbona unaleta mahaba ktk mambo mazito.
ushahidi muhimu si ndio hiyo video,sasa unataka autoe mara ngapi?au unataka atafsiri kinachoongelea katika video hiyo kejeremani?.

Kama kuna ziada atatoa ushahidi mahakamani.
 
Jinsi wananchi tulivyo na shida nyingi,halafu tunavyosikia viongozi wanavyofisadi nchi,ripoti zinatolewa,hakuna hatua zinazochukuliwa,halafu badala ya kuzungumzia haya,mtu anaingia bungeni na kutumia muda mwingi kuzungumzia upuuzi huu,na spika anamshangilia na watz mnaendelea kusapoti ujinga huu!iko siku tutachinjana nawaambia kiukweli kabisaa!
 
Back
Top Bottom