Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Tatizo sio wabunge bali spika kuruhusu hoja zisizo na mashiko kwa taifa huku akizizima hoja zenye mashiko kwa taifa. wanataka kusikia tu mipasho ya mwigulu

Unakumbuka mipasho ya mbowe Jana..Hilo ndio chanzo cha hotuba Kali ya mwigulu leo
 
Hotuba ya mbowe Jana ndio imechokoza haya ya Leo ya mwigulu mana Alimsema mwigulu na mwigulu ametoa ya facts alizonazo
 
Amesha fikisha kile alichonacho mahakamani (tape, notes)
Mi nashangaa sana CHADEMA kuwasilisha hoja hili bungeni
Hata kama wanataka kumsaidia, wamsaidie tu, bunge la nini?
We Mwanamke una matatizo sana kwa kweli
Utakuwa na Stress tu
 
Bocho naomba utoe facts za tatizo la hiyo hotuba!

Hivi Mbowe hana washauri wa kupitia hotuba yake kabla ya kuipeleka bungeni? Kama ile hotuba ni ya kwake peke yake, CHADEMA mtakuwa na ahueni.

Lakini kama uongozi wa chama ndio umeandaa ile taarifa ya budget, CHADEMA hamna kitu, ni domo kaya tu.
 
Last edited by a moderator:
kama mwigulu yupo tayari kutoa ushahidi popote polisi wanachelewa nini kumkamata na kumhoji?l
 
kama mwigulu yupo tayari kutoa ushahidi popote polisi wanachelewa nini kumkamata na kumhoji?l
Sheria ya wapi hiyo mtoa ushahidi anakamatwa,utaratibu ufuatwe mbona wanaotuhumiwa nao wamekaa kimya?
 
Hivi huyu jamaa ana shida gani? Mbona anakua na kauli na vitendo vya kijinga kiasi hiki?

Sijasikiliza mchango wake huo alioutoa hapo bungeni lakini kwa jinsi ninavyomjua sina shaka ni yeye ndo aliyechangia hivyo katika hoja hiyo. Sasa anasema hotuba ya Mbowe ni malalamiko kwa kuwa haina mapendekezo yoyote, vipi kuhusu hotuba za Mwenyekiti wake wa Chama?

Juzi tu tumesikia Rais mzima analalamika kuhusiana na vurugu walizotengeneza wao na kuziita za kidini, na kuweka mstakabali wa Taifa letu mikononi mwa viongozi wa dini, kwanini hakumueleza mwenyekiti wake kuwa analalamika? Waziri Mkuu nae kwenye hotuba yake hivyo hivyo kama bosi wake, kwenye hotuba ya bajeti nae analalamika tu. Ipi afadhali kulalamika kwa kiongozi wa upinzani (kama ni kweli) ambaye hana serikali na dola au kulalamika viongozi walioko madarakani ambao kila kitu wanacho pamoja na kodi zetu. Ama kweli nyani ni mnyama mbaya sana.

Ujinga mwingine wa huyu mtu ni kwamba anadhani siasa ni kuisema CDM tu. Yaani kila anapopata nafasi ya kuongea au kuchangia, yeye ni kuwashambulia CDM tu. Sijui kwanini hakui huyu bwana. Kweli CCM imekua kama kokolo kwa kusomba hata ambao walipaswa kuwa hospitali za wagonjwa wa akili kama wagonjwa lakini wamechukuliwa kama ndo MAJEMBE ya chama.

LAKINI HATA HIVYO ASIPOWAZUNGUMZIA CDM ATATOA HOJA GANI NYINGINE ILI ASIKILIZWE!!!!?
 
Watanzania tukae chini na kutumia bongo zetu. Haya Mahaba ya vyama vya siasa yataibomoa nchi. Huwezi kumlaumu mtu anayeharibu mipango ya Watu wa Giza.
 
Mwigulu kwetu ni juu ya dali huwa tunaweka mahindi yapigwe na moshi yasiharibike!! Sasa nashangaa kusikia ni jina la mtu tena fytu kichwani
 
Back
Top Bottom