Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Karibu watu wote wenye kuona Mbali tulifahamu kwamba Mwigulu Nchemba ni lazima atayasema haya anayoyasema , maana ndiyo Move ilivyopangwa , kujua tu kwamba angeropoka uongo hata kabla hajaropoka , Ni ushindi mkubwa ! Siku za Mwigulu kwenye Siasa zinahesabika .

Huyu gaidi ni lazima aropoke maana movie yake imeenda alijojo hakuna anayetaka kuiangalia sasa ameingiwa na wasiwasi mkubwa kwamba uongo na ugaidi wake umeshawekwa wazi.
 
Kiongozi huyu ni mfano wa kuigwa kwani anajiamini, hapendi dhulma na pia namuomba mungu aonyeshe na kuwadhalilisha waovu wote wanaochonganisha serikali na wananchi,
viongozi gani hawaamini jeshi la polisi, mahakama bunge n.k?
 
director: Mw'gulu Nchemba
location: Mw'gulu Nchemba
promoter:Mw'gulu Nchemba
marketing: Mw'gulu Nchemba


THE END
 
Kwa hili mimi napingana kabisa na wewe ki msingi spika hana makosa kwani hata jana kwenye hotuba ya Mbowe kama ulifuatilia vizuri alizungumza maneno makali sana na kwa suala hili alimlenga Mwigulu moja kwa moja na Mwigulu alikuwepo alitulia tuli sasa tatizo nini Mwigulu kujibu hoja leo. Mimi nadhani paia Mwigulu kasaidia kasema yupo tayari kutoa ushahidi popote tatizo ni nini? Kama CHADEMA kitaendeshwa kwa kila kitu kuona kuwa kinaonewa ni ngumu sana kukijenga chama na kwa utaratibu huu nina wasiwasi mkubwa kama wakipewa madaraka ya nchi watakuwa ma dictator kwani siku zote dictator hapendi kukosolewa

well said.
 
Nadhani tatizo sio Mwigulu tatizo kubwa ni Spika wa Bunge kuruhusu hayo yote yaendelee bungeni ili hali suala zima lipo mahakamani. Ikiwa shutuma zinaihusu vyombo vya dola zipo mahakamani spika huwa makini sana kuzuia wabunge wasilijadili kwa madai kuwa hilo suala lipo mahakamani. Leo kwa vile shutuma ni dhidi ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA basi ni sawa tu mtu kuongea lolote bila kujali kuingilia uhuru wa mahakama.
 
mwingula yukokwenye hatamu kwa hiyo anayo haki ya kuyasema hayo lakini akumbuke kila enzi inaomwisho cjui wakati huo atakuwa mwingula yupi
A%20S-heart-2.gif
 
Only in Tz Natamani mabunge ya wenzetu pale wangezipanga halafu ndio mwigulu angejua Kuwa matusi na uzushi bungeni si mabali pake. Hawa ndio wanaokiharibu chama na kuiharibia serikali kwa kujifanya wao ni wasemaji wakuu wa serikali na chama Wakati busara zero kabisa. Wamezoea kusutana CCM Kutwa kutwangana.lol!
 
Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo].

MAKINDA JAMANI!:nono: MUNGU AMSAMEHE NAJUA ANAMLINDA BOSI,ILA AJUE WATANZANIA WANAUMIA KWA AFANYAYO. MKUU NIMEKUNUKUU KWAN UMEONGEA POINT.
 
Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale iwe polisi, mahakamani bungeni hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, na kwamba kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari kuthibitisha mahali popote. Amewataka viongozi wa chadema wasitafute mchawi kwa kusingizia vyombo vya dola hasa polisi na usalama wa taifa kwamba vinahusika.
Amesema ni vyema viongozi wa chadema popote pale walipo waende kwenye nyumba za ibada zilizopo karibu nao wakatubu na kuungama kujisafisha na matendo maovu ya kigaidi na mauaji wanayoyafanya. amewashangaa kutaka madaraka huku wanawaua wananchi wanaotaka kuwaongoza...awaambia shame on you, look at you chadema!!!!!

Amesema ile ya chadema iliyowasilishwa na mbowe ilikuwa ni malalamiko ya kambi ya upinzani na sio hotuba ya kambi ya upinzani kwa kuwa haina mapendekezo wala solution ya matatizo pamoja na kwamba ina urefu wa kurasa 70.

Amelitaka jeshi la polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE kwa kuwa ni mkurugenzi wao wa ulinzi na usalama, kufuatia maelezo ya mbowe jana kwamba anayewasiliana na gaidi naye ni gaidi pia hivyo akamatwe..

Nahisi tanzania hakuna seperation of power and effective supervision with implementation of laws,principle n policies accordingly!!!
Bungeni tunajadili taifa la jana,leo na kesho au siasa!?
Bungeni ni jukwaa la kutamba na kutafuta jina kwa maneno au kwa hoja zinazohusu maendeleo??!!...ningefurahi sana kama converstion hiyo ingehusu ile mikataba ua uchina!!
genuine patriotics ot this stata are shedding off their tears!!
 
mwingula yukokwenye hatamu kwa hiyo anayo haki ya kuyasema hayo lakini akumbuke kila enzi inaomwisho cjui wakati huo atakuwa mwingula yupi
A%20S-heart-2.gif
Sijui wamekumbwa na upofu gani kushindwa kuona kuwa mwisho wao ni 2015.
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!hata hivo hii ya Mwigulu ni kuanguka na si kuteleza.Ieleweke kwamba mbinu zinazofanywa na Mwigulu na chama chake hayana tija kuwakomaza kisiasa na kuwapa uhalali wa kuongoza nchi hii kamwe.CHADEMA iuwe watu kwa lipi hasa?CHADEMA inamaslahi gani na kuua watu na kwa kutumia nini?Hayo mafunzo waliyafuzia wapi na slaha hizo wanazitoa wapi au na wenyewe hutengewa bajeti kuingiza slaha nchini?
 
Tatizo cyo mwigulu ni ugonjwa mlio uleta ninyi cdm na bado kuna mengi mliyopanda mtavuna, Mnaposimama majukwaani na kusema maneno yasiyofaa mbele ya wananchi mlitegemea nn? Taifa mnalipeleka kubaya na kurithisha kizazi kisichokuwa na maadIli. nasema mtavuna mlichopanda, kutukanwa na Mwigulu ni matokeo ya matendo yenu.
 
Huyu mwehu huyu ...eti Ma engineer wakafundishe shule za kata...alaf walipwe acccordingly...wakati hao tu walimu wameshindwa kuwalipa...

Ati Viongozi wa CHADEMA ndio Magaidi na wauaji ...na yupo tayri kutoa ushahidi na pia aliyerecord video ile yupo na yupo tayari kusema chochote..
Ati "You look Messless,shameless...look at you "
Hivi huyu jamaa anajua mziki wa engineers au keshalewa madaraka, lets wait and see 2015 is coming.....!!!
 
Mwenzenu nashindwa kumwelewa huyu kijana mwenzetu Mwigulu Nchemba ana matatizo gani kwani hayo maamuzi yake ya kujitoa kafara kwa ajili ya CCM yatamfikisha mahali pabaya sana na asipopatarajia, akumbuke kuwa ACHIMBAE SHIMO ATATUMBUKIA MWENYEWE, nawasihi sana wapenda mabadiliko wenzangu tusitishwe na kelele za GOLIATI/CCM kwani tunae DAUDI/CHADEMA ambaye amekuja kuzima kelele zote za Goliati na kuzifanya kuwa historia kwa kizazi kijacho...... MABADILIKO NI LAZIMA
 
Kiongozi huyu ni mfano wa kuigwa kwani anajiamini, hapendi dhulma na pia namuomba mungu aonyeshe na kuwadhalilisha waovu wote wanaochonganisha serikali na wananchi,
viongozi gani hawaamini jeshi la polisi, mahakama bunge n.k?

MWIGULU KAOKOKA?HUJUI ALICHOFANYA IGUNGA NA ARUMELU,ANA MDOMO MCHAFU KAMA LUSINDE,KWA MWENYE MPANGO WA KUWA NA WATOTO,AOMBE MUNGU WASIPATE CD ZILE.WAAMINI SANA POLIS KWAN SIKU YAJA UTABAMBIKIKIWA BANGI,AU KUITWA KUTOA USHAIDI UHOJIWE KWA UMEME.MAHAKAMAN UTAAMBIWA UPELELEZI BADO,MAHABUSU KUNA PAPASI NA UNA PUMU,UTAIPENDA TU POLISI.BUNGEN SPIKA AKIULIZA MNAUNGA MKONO HOJA YA WIZARA ....KUHUSU USHOGA WASEME NDIYOO.UFURAHI,NA UJIANDAE MWANAO KUOLEWA.UTAPENDA TU HOJA YA WENGI WAPE!...BADILIKENI.TUWAPENDE POLIS,MAHAKAMA,BUNGE WAKIFATA SHERIA NA KUWA KWA MANUFAA YA WATANZANIA NA SI WACHACHE,:A S-heart-2:
 
Kwa kukiri wazi hadharani kuwa anahusika na ile video, nitawashangaa Polisi kama hawamhoji Mwigulu kutokana na source ya mkanda huo. Atoe ushahidi mahakamani na huyo aliyerekodi na kumpa mkanda huo aitwe atoe ushahidi ili kitendawili kiteguliwe. Mwigulu nimmoja kati ya wahusika WAKUU KATIKA SUALA HILI. Lakini mawasiliano na pesa alizomtumia Ludo lazima vihojiwe.
 
Haya yote yanatokea kwa sababu hatuna upinzani makini.

CHADEMA sio chama makini, baada ya kumaliza hoja za ufisadi miaka miwili nyuma, hawana jipya la kushauri serikali.

Matokeo yake, mkuu wa kambi ya upinzani badala ya kupeleka mapendekezo ya budget, anaanza kulalamika bungeni!

Badala ya kujadili maendeleo, wanaanza kujadili kesi zilizopo mahakamani! Tutafika kweli?
 
Back
Top Bottom