Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Hivi Mbowe hana washauri wa kupitia hotuba yake kabla ya kuipeleka bungeni? Kama ile hotuba ni ya kwake peke yake, CHADEMA mtakuwa na ahueni.

Lakini kama uongozi wa chama ndio umeandaa ile taarifa ya budget, CHADEMA hamna kitu, ni domo kaya tu.
 

Nilikuwa najiuliza, hivi yale MAPESA ya Sabodo yanatumika kwa ajili ya nini???
 
Kwahiyo kutukana ndio jibu? yapi mabaya kati ya kakako mwigulu na Lusinde na ya chadema? kwa taarifa yako mwigul na shem wako Lusy...nde hawarud bungen,bora huku lusinde kaanza kujiandaa kusepa anajua ccm yenu haitampitisha tena.Alias cdm hatarudi tena labda aanzishe chama au awe mabaki ya uozo wa ccm.
 
Juzi nilimuuliza Mwigulu Nchemba kama hafanyi haya kwa maslai ya kisiasa na hii ilitokana na yeye kupewa huo mkanda na si polisi na hasa huyo kiongozi wa chadema!

Alisema kuwa anafanya hili kwa maslai ya taifa lakini siku zinvyo enda ukweli unaonekana hii ni case yenye maslai ya kisiasa!

Na kwenye hii case ninacho subiri ni hapo atakapo mtaja huyo kiongozi wa chadema amabye amesema ana kerwa na maovu ya viongozi wenzie!
Hapa ndio mzizi wacase hii ulipo kwenye huyo kiongozi wa chadema anaye tajwa na mh mwingulu!

Hii case ina maslai ya kisiasa!
 
Last edited by a moderator:
haswaaaa huyo spka namchukia mbaya

.
Huyu spika ni kirusi kibaya sana kwa mshikamano na amani ya Tanzania kama alivyokuwa Yezebel wakati ule kwa taifa la Israel. Nawaahakikishieni Makinda hayupo pale hivi hivi tu, ila kwa kuwa kuna mwisho kwa kila lenye mwanzo yeye amekuwepo kwa kusudi la mwisho wa walaghai fulani hivi ambao wamefanikiwa kudanganya kwa kipindi cha miaka 50.
Mwigulu afahamu kuwa Mungu hadhihakiwi. Yeye ni wa haki na haijalishi imechelewa kiasi gani ila ni sharti kwa wakati wake iachiliwe. Wakati ndio umefika na kila upande umeandaa mashuhuda wake.
.
 
Ccm ilijengwa na wenye akili, sasa inabomolewa na wagonjwa wa akili! Mwigulu sifa za mipasho unayotoa ni kuendelea kuididimiza ccm,k/katibu mkuu unatoa mipasho utadhani mwendawazimu fulani,eee?!!! Nashukuru kwamba umejitangaza kama wewe shahidi wa mkanda huo namba 1 hvyo tunategemea polis kukuhoji mapema iwezekanavyo not otherwise.
 
Mwigulu na CCM wako tayari kuivuruga hii nchi ili waendelee kutawala!
 
mwigulu anapoteza muda wake tu!! Mtu mdogo sana yule na hiki alichoingia ni choo cha wanawake!

Mwenzake Lowassa ametulia tu pamoja na kashfa zote zinazomwandama.
 
Wabunge wa TZ wanapoteza muda mwingi kujibizana kuliko kujadiri hoja.. Mh Nchemba amenisikitisha sana maana ameidharau mahakama na amevunja kanuni za bunge huku spika akisema "mkuki kwa nguruwe"😡

Tatizo sio wabunge bali spika kuruhusu hoja zisizo na mashiko kwa taifa huku akizizima hoja zenye mashiko kwa taifa. wanataka kusikia tu mipasho ya mwigulu
 

siasa za maji takaambazo CCM ni mabingwa!
 
Tuna kila sababu ya kukataa propaganda zinazo jaribu kutaka kuwaaminisha wananchi kwa kuwa tu jambo hili limesemwa bungeni na kwa kuwa tu mbunge ana kinga za kutoshitakiwa na mamlaka yeyote ikiwa jambo lenyewe limezungumzwa ndani ya bunge.Hali ya nchi ni tete lakini utete wa hali hii isiwe sababu ya mtu kuitumia kinga yake vibaya na kufitinisha watu,kinachofanyika ndani ya bunge letu ni bunge limegeuka kuwa jukwaa la kisiasa na kusahau utetezi wa wananchi juu ya maisha yao na raslimali za taifa na kuwa sehemu ya mashambulizi ya chama fulani dhidi ya chama kingine.

Lakini pia cha msingi,serikali kupitia vyombo vyake vya dola imezidi kudhihirisha udhaifu wa kiutendaji kiasi cha kupuuza majukumu yao kiutendaji.Toka Mh. Nchemba aseme ana mkanda wa mikakati ya CDM ya kigaidi dhidi ya kundi fulani la watu hatujasikia serikali wala vyombo vya dola vilivyosimama na kumhoji mheshimiwa huyu,lakini si vyombo vya dola tu hata mahakama kukemea suala hili kuzungumzwa nje ya mahakama ilihali kesi ipo mahakamani.Maanake nini,maanake serikali imelala usingizi na kukubali kumtumia kada wa chama cha CCM ambaye ni kiongozi wa chama tawala kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi.

Hali hii ikiachiwa kwa kumea kama ilivyofikia hivi sasa basi tujue ni hatari kama kundi lengwa likiamua kujibu mapigo kwa staili hiyo hiyo ya kulitumia bunge kama sehemu ya kujibu mashambulizi.Lakini ikumbukwe pia kuwa CDM ni chama cha kitaifa ambacho kilikidhi vigezo vyote na ndiyo maana msajili wa vyama vya siasa alikubali kukipa usajili wa kudumu baada ya kujiridhisha,kwa mantiki hiyo basi Mwigulu anataka kuliambia taifa kuwa CDM ni chama cha ugaidi na wanachama wake na wanayoisapoti ni magaidi pia.Nini hatari ya kuwaita Watanzania magaidi kwa minajili tu ya kukipa ridhaa CCM ya kuendelea kushika dola?Hatari yake ni mgawanyiko wa kitaifa ambao una kwenda kuvunja ngome ya umoja wa kitaifa na kujenga makundi ya kitabaka yaliyoasisiwa na mkakati wa CCM.

Haya yanayojaribu kupigiwa chapuo na makanjanja wa siasa athari yake ni sawa kabisa na yaliyokuwa yanapigiwa debe kuhusu udini katika kipindi cha uchaguzi wa 2010,kwakuwa chapuo lile lillipuuzwa matokeo yake leo watu wanachinjana kwa sababu ya kutafuta haki ya kuchinja ilihali miaka dahali waliishi kama ndugu.

Kuna mambo ya msingi kama kiongozi na mwakilishi wa wananchi ambayo yalihitaji umahiri wake kuyapigania na si muda wake muafaka wa kupiga propaganda ilihali ana changamoto nyingi zinazo kikabili chama chake katika utekelezaji wa ilani ya chama.Maisha bora kwa kila Mtanzania hayataweza kupatikana kwa kujenga uadui kati ya wananchi wa taifa moja ambao maisha yao ya kila siku ni bora na jana yao.Staili hii inayoonekana ni ya mkakati toka chama cha CCM kuwashughulisha CDM wajisahau na katiba mpya usipoangaliwa kwa umakini unaweza kuleta hatari kubwa najanga kubwa kwa taifa.

Videbe hivi vilivyonadiwa sana katika chaguzi mbalimbali ndiyo leo vimekuwa zao la message za kuwatenganisha Watanzania na kuhamasishana katika uchaguzi wa 2015 watu wasimame kwa misingi ya udini,lakinii hatari nyingine inayo kuja huko mbeleni serikali na chama chake isipokuwa makini inaweza kusababisha wimbi kubwa la wanyonge kuamua kushika hatamu za uongozi kwa nguvu bila kutumia demokrasia kutokana na kuchoka kugawanywa kwa misingi ya kichama.

Ni wakati sasa CCM kama chama kilichoshika dola kitumia nafasi yake vizuri katika kuimarisha demokrasia kuliko kuonyesha waliikubali kwa shingo upande ili kuwa ridhisha mabwana wakubwa kwa ajili ya njaa lakini kinyume chake kutenda pasi na maneno na makubaliano ya misingi ya demokrasi ya vyama vingi,viongozi wenye misimamo na dhana mbaya ya kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kigaidi ni chachu ya kuwataka Watanzania walio wengi wenye mapenzi mema na waliopigika kutokana na mfumo mimi kuamua kuingia msituni kutafuta njia mbadala ya kuikomboa nchi yao dhidi ya walafi wenye kutumia kila aina ya mbinu ili waendelee kushika dola.

I believe that unarmed truth and unconditional love will have the final word in reality. That is why right, temporarily defeated, is stronger than evil triumphant.
 

He, roho ya uchawi live!!
Zamani ukimgonga mwenzako Bahati mbaya Basi mzazi anayepractice uchawi anawaita, anamwambia yule aliyegongwa Bahati mbaya Amlabue bao la nguvu mwenzake Kama kulipiza kisasi, kisha anasema haya mmeshalipizana nendeni.. In the village ukiona mzazi anayewafundisha Watoto wake kulipizana lazima awe Mchawi ..naiona hii makitu Leo live..!!
 
Kwa hapa tulipofikia,vyama vya siasa Tanzania haviwezi tena kumkomboa mtanzania maskini zaidi ya kumtumia Kama daraja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…