Hivi huyu jamaa ana shida gani? Mbona anakua na kauli na vitendo vya kijinga kiasi hiki?
Sijasikiliza mchango wake huo alioutoa hapo bungeni lakini kwa jinsi ninavyomjua sina shaka ni yeye ndo aliyechangia hivyo katika hoja hiyo. Sasa anasema hotuba ya Mbowe ni malalamiko kwa kuwa haina mapendekezo yoyote, vipi kuhusu hotuba za Mwenyekiti wake wa Chama?
Juzi tu tumesikia Rais mzima analalamika kuhusiana na vurugu walizotengeneza wao na kuziita za kidini, na kuweka mstakabali wa Taifa letu mikononi mwa viongozi wa dini, kwanini hakumueleza mwenyekiti wake kuwa analalamika? Waziri Mkuu nae kwenye hotuba yake hivyo hivyo kama bosi wake, kwenye hotuba ya bajeti nae analalamika tu. Ipi afadhali kulalamika kwa kiongozi wa upinzani (kama ni kweli) ambaye hana serikali na dola au kulalamika viongozi walioko madarakani ambao kila kitu wanacho pamoja na kodi zetu. Ama kweli nyani ni mnyama mbaya sana.
Ujinga mwingine wa huyu mtu ni kwamba anadhani siasa ni kuisema CDM tu. Yaani kila anapopata nafasi ya kuongea au kuchangia, yeye ni kuwashambulia CDM tu. Sijui kwanini hakui huyu bwana. Kweli CCM imekua kama kokolo kwa kusomba hata ambao walipaswa kuwa hospitali za wagonjwa wa akili kama wagonjwa lakini wamechukuliwa kama ndo MAJEMBE ya chama.
LAKINI HATA HIVYO ASIPOWAZUNGUMZIA CDM ATATOA HOJA GANI NYINGINE ILI ASIKILIZWE!!!!?