Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?
Yaani Bora ninyamaze maana Hali niliyonayo naweza PATA kiharusi muda wowote
 
Kuna watu hata ujumbe wa nyumba 10 hauwafai Sasa kapataje ujasiri wa kutupangia fedha na matumizi...halafu ni doktaa...PESA zanawafanya waongee utumbo...
 
Walio mpa hiyo PhD inabidi sasa wachunguzwe kwa uhujumu wa elimu... Iweje muhitimu wao awe na mawazo finyu kama hayo na mawazo duni kwa level yake ya PhD? ni lini serikali ikawa na fedha zake? ina vitega uchumi gani vya kuongeza mapatol? imewekeweza wapi ? ni kodi za wananchi zitakazotumika kulipa deni, hizo kodi zinatokea wapi kama sio kwa wananchi na makampuni binafsi ? Huyi Nchemba siku marejesho yakifika sijui atakuwa yupo wapi na atakuja na sounds gani wakati huo...
 
Mwingulu asitudanganye, Deni la Taifa likiwa kubwa ....nchi itaingia kwenye mdororo wa kiuchumi..
Kwa Maana hatakuwa na back-up ya ku-bust uchumi wetu.... na ivyo ni-automatically wananchi tutaishi maisha magumu sana ..

Kwamba wananchi hawatalipa mkopo wa Taifa, siyo kweli. kwa maana bidhaa zitapanda..bei then na wananchi wa hali ya chini watashindwa ku- afford price directly ... mfano mzuri ni kenya last year wana nchi waliongezewa kodi kwenye bidhaa ili serikali ilipe madeni..

Mlipaji mkuu wadeni la Taifa ni mwananchi.
 
Eboo!! Huyu Myeramba vipi?
Kwani serikali itapata wapi fedha zaidi ya kutukamua wananchi,?
 
Huyu ndyo PHD holder????hakika hii nchi ina zaid ya matatizo
 
Siriazi, inachekesha kama wananchi wanalipa kwa kuambiwa na si kwa kununua na kuuza.
 
Mbatia alikuwa sahihi, tuna viongozi wasio wa uelewa wa mambo!! Kodi ni sehemu kubwa ya serikali kupata mapato na kulipia matumizi yake ikiwemo kulipa mikopo, na kodi hiyo hulipwa na mwananchi kupita manunuzi ya huduma na bidhaa, na shughuli nyingine kwa mujibu wa sheria! Hakuna wakati mwananchi aliwahi kugongewa na kulipishwa kodi nyumbani kwake - sijui atagongewaje kuhusu deni la taifa!!

Tuna viongozi walio katika nafasi hawapaswi kuwa!! Kweli huyu ndio aina ya kiongozi wa kutukwamua???

Ee Tanzania yangu!!!
 
Jinga Kama hili unalipa wizara ya pesa. Na linaongea ujinga likifikiri watanzania wote Ni wajinga kama waliompa kura kiomboi. Jitu lenye laana utalijua tu
 
Haya mambo ndo ilitakiwa wabunge wetu wayajadili bungeni.ila ndo hivyo tena.
Nadhani ndugai alishaliona hili na ndiko alikokua anaelekea,. Sema wasaka teuzi wakujikombakomba wamemkata upepo,.
 
Serikali huwa haina fedha! Fedha ni za wananchi. Waziri arekebishe kauli yake. Wananchi wasipokamuliwa Kodi serikali inapata wapi pesa?
N.b. Sina upande ktk ugomvi wa Samia na Ndugai.
 
Hii serikali ya vilaxa,kuna tofauti gani na MTU anayekopa halafu anarnda kujengea nyumba,au anasomeshea mtoto. Sisi wachumi tunahimiza kopa tia kwenye biashara ili biashara ndio i -generate cash flows itakayosaidia kulipa mkopo. Ndio maana nasema magufuri alikuwa ana akili sana,alikuwa anakopa anajenga bwawa LA umeme akijua fika umeme atauza hatΓ  nchi jirani, lakini sasa hii ya kukopa unajenga madarasa. Kwani tumeshindwa kujenga kwa fedha za ndani? Wanao shadidia hili in wazembe was kufikiri.
 
Wewe unasema nini mkuu, fungua biashara uone kama hautadaiwa binafsi, weka umeme kwenye mita yako uone kama haudaiwi binafsi, mtumie mtu pesa uone kama hizo tozo hujalipa wewe mwenyewe binafsi, kwenye hizo kodi sijaona anaalikwa jilani kusaidia.Unapolipa hayo makodi jua unalipa deni la taifa, kama ni hivyo kwanini useme sitadaiwa mimi binafsi??
 
Kwani TRA inapofungia watu biashara zao kwa sababu ya kutolipa kodi lengo lao ni nini ?? huyo waziri aombe radhi kwa kauli yake hiyo, inakera
 
Mkuu KODI unayolipa sio kodi ya MADENI. Unalipa kodi ya MAENDELEO ✍️
Madarasa ya kisasa, zahanati nk si ndio maendeleo? hiyo hela imetoka wapi? kama sio mikopo
 
Anaposema serkali italipa anamaanisha nini?
1. Kwamba Tozo si za wananchi
2. Kuwa kodi ya mwananchi
3. Kwamba maliasili si za wananchi
Hivi Serkali ina mapato tofauti na wananchi na maliasili zao?

Huyu ni Phd holder
Mpuuzi sana Mwigulu.......serikali inapata wapi pesa ? Zikitoka wanananchi kwenda serikali si zao tena ila za serikali ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…