TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Vifo vingine vinatokana na dhuruma kuiba wake za watu nk. Sidhani kama kufikiria serekali ya fisiemu inauwa hawa watu wote ni sahihi
let be reasonable guys. Serekali haiwezi kuuwa watu hovyo ikuuwe ww nani!!?? Yani serekali ije ikuuwe ww tigopesa kuweni na heshima kidogo basi
Kwann vifo vimekuwa vingi wakati huu? Kwann wanaoua hawakamatwi? Waliowahi kutekwa na kupigwa kisha wakasalimika walisema wametekwa na vyombo vya Dola wengine mpaka wakawataja na watekaji kwann tusihisi kwamba serikali ndio inahusika na unyama huu?
 
Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
Huyu ndio mwenye jina la kituo cha goba kwa ulomi?
 
mbaya sana

tusubiri uchunguzi..,MUNGU awape nguvu kipindi hiki kigumu familia na watu wa karibu kwa ujumla
 
Kwann vifo vimekuwa vingi wakati huu? Kwann wanaoua hawakamatwi? Waliowahi kutekwa na kupigwa kisha wakasalimika walisema wametekwa na vyombo vya Dola wengine mpaka wakawataja na watekaji kwann tusihisi kwamba serikali ndio inahusika na unyama huu?
Unahisi!!??
Umukuwa na hisia nyingi kama mtoto wa kike lete ushahidi
 
Kwann vifo vimekuwa vingi wakati huu? Kwann wanaoua hawakamatwi? Waliowahi kutekwa na kupigwa kisha wakasalimika walisema wametekwa na vyombo vya Dola wengine mpaka wakawataja na watekaji kwann tusihisi kwamba serikali ndio inahusika na unyama huu?
rejeeni kauli ya polisi juu ya jamaa harafu chagueni Moja
 
CCM ITAENDELEA , MNATUMIA VIFO KUPIGA KAMPENI KWA SABABU HAKUNA MLICHOFANYA MIAKA MLIYOKUWA BUNGENI. NATAMANI HILI LICHAMA LA CHADEMA LIFUNGIWE KUWE NA CHAMA KIMOJA. MAMA SIMPINGI AU KUMKOSOA ILA KUWAACHIA HAWA MAJAMAA WA CHADEMA KUFANYA KAMPENI NAHISI KWA UPANDE WANGU SIO JAMBO JEMA...
Binadamu asiye na uchungu na uhai na damu ya mtu ni muovu, mwehu, mwenye laana na shetani. Chama hakina mbadala kwa uhai. Tusifurahie kifo chochote kwa utetezi wa chama. Akifa wa ccm au serikali uchunguzi ni haraka. Haki ya kuishi ni ya msingi kwa wote. Kabla ya kushabikia U-ccm au u-chadema hujui kama chanzo cha kifo ni ajali, madeni, dhuluma, serikali au ugoni. Lakini kwa maneno yako unahitimisha kuwa ccm ndiyo imemuua kwa kushabikia. Wajane na yatima wanakupa furaha gani.
 
Back
Top Bottom