My week end is super crazy

Siwezi kuwarudisha hadi wazazi wao warudi,wamesafiri nje ya Tz na mimi mwenyewe ndo nilisema waletwe kwangu coz navipenda ila nimejua hawa inabidi mapenz ya mbalimbal,wakichukuliwa sitarudia tena kuvichukua
.
Poleee dear,
 
Hongera kwa kuwajali watoto wengine, kuhusu malezi tunatofautiana kuna wengine mtoto hajawahi kuguswa kabisa hata afanye kosa gani anachukuliwa mtoto

Sisi wengine, wazazi wetu walijua kutofautisha kati ya utoto na ujinga

Haiwezekani mtoto unampa chakula anajifanya kwenda kula chumbani afu anakimwaga kisa ugali au mboga ni kitu asichopenda au unaacha hela anapita nayo

Aisee nilichezea sana mikwaju kwa ujinga ila sijawahi kuadhibiwa kisa utoto

Vitu kama umeenda kucheza unarudi mavumbi mwili mzima, hizo nilikuwa natishiwa tu kisha adhabu nayopewa ni kwenda kuoga
 
Wanyooshe wakiwa kwako wajue namna ya kuishi bila vurugu.
 
🙏🏼🙏🏼 Asante mkuu.

Itakua mlivyoshuka watu waliwafanya mada.
Pole ila sio kosa lake masikini kwake ilikua vitu vigeni ila hongera kumfanya azoee sbb hatujui kesho yetu itakuaje.

Mimi wa kwangu keshazoea kupanda daladala.Hata mimi napandaga hasa nikiwa na mwanangu na nimemfundisha hadi kugombea siti😀Huwa namwambia we wa kiume gangamara tupate siti😀😀 na katapambana tutapata kweli siti na akija mtu mzima bila kumwambia atasimama na kumpisha na ninakua nimemlipia kukaa kama mtu mzima na kuna siku tulipanda nikamwambia sina hela ya kukulipia ukae kwa hiyo utasimama mpaka tufike na huwa hapendi kubebwa.

wa kwangu pia yuko la 5 kama wa kwako ila kwa upande wangu naona bado ni mdogo kutumia daladala akiwa peke yake kwenda shule.Mimi wa kwangu atatumia daladala kwendea shule akifika form one ila kwa sasa naona ni hatari sana
 
Mwisho wa siku ndo wanakuomba kitu unawaambia hauna, Wanajiongeza halafu mnakuja kulalamika watoto wanalawtiwa sana sikuhizi.
Ni kweli ila sio wa kwangu.
Nakubaliana na wewe hayo sio malezi wala upendo ndio maana nimelalamika.

Wa kwangu anajua hapana.
Anajua kuna siku mama hana hela na na kwamba sio kila atakachotaka atapata,anajua kuna watu wanalala
Njaa hivyo chochote kinachopikwa tunapaswa kula kwa furaha
 
KWA HIYO UKAENDA KUMNUNULIA KILA MMOJA TV YAKE 😁😂 MAISHA YA JF NITAAMBIWA SASA HIVI TAFUTA HELA
Why not mkuu?
Iam too old kusikiliza vilio na kesi za kupigana kila saa hadi niwe kama mkimbiz nyumban kwangu wakati laki 6 tu inatosha kutatua hilo tatizo
 
Akina junior hao.
Sawa pesa si zipo acha watumie.
Ila sie wengine hatujalelewa hivyo.
baba kila siku akirudi uwa anarudi na bakora ya dharura.anajua mwamba huko atakuwa kaharibu tu.
Na kweli akifika nyumbani mashitaka kwa mama wa kufikia.
Kabla ya kulala zinatembea kwanza bakora.
Kuna kitabu mpaka leo sikipendi. Kile cha "SOMA KWA HATUA"
KIMENILIZA SANA KILE
 
Honestly,nawaonea huruma sana hawa watoto.

Sijawahi ona watoto wamedekezwa kiasi hiki.
Sijui wazazi wenye haya malezi huwa wanawaza nini?
Ni ujinga kuwaendekeza watoto. Hawataweza ishi na mtu yeyote.
 
Umeongea vyema sana mkuu.

Ila pia naamini iko haja wazazi tupate mafunzo ya malezi maana wengine wanachukulia utoto kama ugonjwa.
Wengine wakiwa na vihela kidogo wanaona sifa kulea watoto kwa style ya what the kid wants the kid gets.

Wengi hawajui mtoto ni kama empty card na vile vitu vinavyoingizwa humo mwanzoni iwe vizuri au vibaya vikishaingia humo ni vigumu kuvifuta na wengi hawajui kuwa watoto sio wajinga.Ni binadamu wanaojifunza kwa kujaribu jaribu.Akigusa moto akiungua hatakaa tena maishan mwake aguse moto.

Akikataa kula ugali ataangalia nini kitatokea.Akiambiwa ukila utakua na nguvu kama baba na usipokula nakuchapa atakula na akikataa akichapwa kweli atajua hapa nikikataa ni viboko ila kakataa ugali anataka chips huyoo mbio unaagiza apikiwe chips siku nyingine ukimkatalia atasumbia sana sbb anajua nikikataa uwezekano wa kupata ninachotaka upo.

Na wazazi tunatakiwa wote tuwe na msimamo,baba akisema hapana na mama ni hapana.Sio baba kasema leo hawa wafue nguo zao akitoka mama unawaonea huruma unawasaidia.Au mama kasema hakuna hela wakienda kwa baba wanapewa.
 
Kina junia ni hatari.
Wazazi wao ndio wana hizo pesa za kudekezana mimi sina hela za kutumia kuharibu mtoto wangu.

Hapo kwa SOMA KWA HATUA nimekuonea huruma.
Nadhani ulikua mzito kusoma hivyo ikawa kila ukikosea unachapwa na ukweli ni kwamba haukua mzito ila aliyekua akikufundisha alikua hajui kufundisha.Zile fimbo zilifanya ukosee zaidi
 
Kosa lako la kwanza,hukuuliza hawa watoto wanapendelea nini kwao hizi taarifa unapata Kwa wazazi wake.
Pili ulifanya kosa sana kununua hizo tv kwakua zinawndeleza ubinafsi Kwa mtoto wako na hao wageni,ilitakiwa uwakalishe na kuwaelimisha suala la umoja and team work,wapeleke nje wakakate majani ya bustani mkiwa wote,osha vyombo nao as team.
Tatu,unaingia gharama bila kua mbunifu as long as unawaridhisha wote,all this are wrong and hata mwanao atakua na tabia ya Umimi and mother only.
Change unavyomlea mwanao mtoe nje acheze na wenzie aweze soma mazingira tofauti.
 
Kuna watu wana malezi utadhani wa na guarantee ya kuishi miaka 100 na kuwa na uchumi mkubwa hadi wafe.

Hayo ni malezi mabovu sana, mtu anayejitambua hawezi kuruhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…