Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

And when Our clear revelations are recited unto them, they who look not for the meeting with Us say: Bring a Lecture other than this, or change it. Say (O Muhammad): It is not for me to change it of my accord. I only follow that which is inspired in me. Lo! if I disobey my Lord I fear the retribution of an awful Day.

10:15
Ongezea tena fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na watu wengine ambao kipindi wanaandika walikuwa hawakufikirii wewe mmatumbi.
 
Ikifika Jumapili wewe zuga tu kwamba unaenda kanisani,ukiamka asubuhi jitayarishe Kisha chukua Biblia yako na utoke ujifanye unaenda kanisani...ukifika huko njiani fanya diversion uingie kijiweni ukapige story na Wana ama uende kwenye movie[emoji23]
Anataka tuwe tunaongozana mguu kwa mguu
 
Wala huna haja ya kumkaripia, labda kama alikwambia kwa njia ya kukushushia heshima ila kama aliongea politely wala huna haja ya kumkasirikia.
Mi nliona kama ni uchonganishi, alishindwa nini kuniambia privately mpaka aanze kusema eti namkaidi mama angu pale sebuleni?
 
Ndiyo maana nilisema hapo juu huyu kijana ni very knowledgeable, wengi humu hivyo vitabu, kama kweli umevisoma, hawajavigusa au wanesoma vichache sana, na sababu kubwa ni kutopenda kusoma na kujielimisha. Ndiyo maana kwenye arguments hapa utaambulia matusi, kejeli na mambo ya kufuata mkumbo tuuu..
Sad generation[emoji29]
 
Dah umeniharibia siku. Sikutegemea kusoma uzi wa kipumbavu kama huu. Miaka 24 ni mdogo na ubaya zaidi bado unaishi kwenu. Unajisikiaje unavyoona mama yako ananung'unika kwama hamfuati maelekezo yake? Wengi wetu huku town hatuendi kanisani ila tukifika nyumbani ili kumfurahisha mama ile siku ya ibada unabeba na biblia kabisa. Baada ya ibada lazima umsubiri asalimiane na watu wake kisha mrudi wote nyumbani. Mama akikunung'unikia ni mwanzo wa kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima. Uache upumbavu wewe. Kama hutaki usumbufu hama hapo kajitegemee.
Kwa hiyo mnaenda kanisani kumfurahisha mama na wala siyo Mungu?? [emoji12] [emoji12] Hii tabia ya unafiki wanayo wengi sana, ukikutana na mzazi anayejiongeza unakuta anaulizilia marafiki zake huko town " vipi vijana huko mjini huwa mnawaona makanisani au msikitini?" anajibiwa kila kitu. Sasa wewe siku ukienda home na kujifanya mtu wa dini kumfurahisha yeye anakuchora tuu.. [emoji23]
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Da nimekuonea huruma sana mdogo wangu.unayo haki ya kubehave hivyo.Inawezekana umepoteza iman na Mungu wako kwa kukosa matokeo ya kile ulichoamini kutokana na kuwa kwako karibu na Mungu.wewe umekuwa wazi lakini hili tatizo linawakumba wengi.Hasa wale wanaotegemea majibu ya haja zao kwa haraka halafu haiwi hivyo.

Ze botom line ni kwamba siyo uzushi,ni kweli Mungu ana exist.na ni kweli pia ukitenda dhambi utakula hukumu ya milele.na ni kweli pia usipowaheshimu wazazi siku zako za kuishi zitakuwa chache.na pia ukiwa umategemea mzazi kama hivyo ulivyo wewe ni miaka yako 24 bado uko home,ni vizuri kutii mashart ya mwenye nyumba.ujue inawezekana umelishwa matango pori ya mtandaoni au na wapinga dini na wewe ukaingia mzima mzima.savabu imani yoyote chanzo chake ni kusikia.sasa inategemea umesikia nini na kwa nani kuhusu Mungu

Tafakari badili tabia ingali bado mapema.Ila pia kila jambo lina wakati wake.Mimi ninauhakika hutaweza kupotelea huko kwenye uhasi maana Mungu ni wa Neema. Mungu wangu aliyehai akurehemu,akuondelee dhambi hii ya uasi
 
Kwa hiyo mnaenda kanisani kumfurahisha mama na wala siyo Mungu?? [emoji12] [emoji12] Hii tabia ya unafiki wanayo wengi sana, ukikutana na mzazi anayejiongeza unakuta anaulizilia marafiki zake huko town " vipi vijana huko mjini huwa mnawaona makanisani au msikitini?" anajibiwa kila kitu. Sasa wewe siku ukienda home na kujifanya mtu wa dini kumfurahisha yeye anakuchora tuu.. [emoji23]
Sasa bora kubishana nae? Bora akuone mnafiki ila awe na amani kwamba ukiwa mbele yake una adabu zote na sio kubishana. Utii kwa mzazi ni lazima.
 
Mzazi yupo sawa sababu we ni mtoto wake hataki uharibikiwe na kingine bado unaishi chini ya wazazi wako unatakiwa ufate kile wanachokwambia

Kijana mdogo ushaona dini uliyozaliwa ndani yake uiamini

Acha kujipa usahihi na mzazi wako mzazi huwa hakosei hata siku moja
Dini ni utumwa wa kipuuzi walioleta wazungu na waarabu
 
God could be there, Im not saying God is there.
Understand the differenece
Viashiria vipi sasa vinakufanya useme kuna uwezekano Mungu yupo? Nilichogundua we ni mbishi na hutaki uweke mind yako iwe free kupokea mawazo mapya, may be unahisi tupo kwenye ushindani wa who is right and who is wrong, hata nikikuuliza kwa nini unahisi kuna uwezekano wa uwepo wa Mungu kama unavyosema utaanza kuleta siasa... Kikubwa umeomba ushauri, ushauri wangu nenda kanisani kama mzazi wako anavyosema kuhusu kusikiliza neno nni juu yako, unaweza kumlazimisha farasi kwenda kwenye maji lakini huwezi mlazimisha anywe maji m
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Solution ni kuhama hapo nyumbani,
Ukiwa na maamuzi yako basi uwe na kwako ambapo unaweza kujipangia hama hapo na hayo unayosema ni usumbufu yataisha

Ila kama Mama yako ni mtu wa imani ya kweli ipo siku utakumbuka housegirl na Mama yako walipokuweka chini na kukuelekeza.
 
Afadhali wewe umekuwa muwazi .
Huo ndio umuhimu mkubwa wa dini kwa Africa hasa usipokuwa tajiri. Mahusiano ya kijamii.Ndoa, kusaidiwa katika shida kubwa na kuzikana.
Ni aina fulani ya uoga wa maisha pia.
😀😀😀 Hakuna tajiri ambae hana dini kacheki hata hao top 100.
Pili siendi kanisani wala msikitini, niliacha hayo mambo, even my father dont do that.
Lakini kwa uzoefu wangu mdogo, im above 35, i am educated. Nimeiona changamoto ya hiyo lifestyle.
To each his own, nilichotoa ni ushauri tu.
Sir Chande Freemason, lakini alizikwa kwa rituals za ki Hindu, Bob Marley na Jah wake mwishowe akarudi Roman Catholic akazikwa...Kingunge Ngombale Mwiru.
Kuna sehemu kasema wachina hawaamini Mungu, nikajua hata research simple tu hafanyi. Wachina na mambo spiritual ni wakongwe dunia hii, leo mtu anasema hawaamini uwepo wa Mungu/miungu🤗
 
Mnachekesha sana nyie watu lol
Sio tunachekesha. Hakuna hasara africa tunayo kama kubadili maisha yetu ya asili na kujifanya ni watu wa kisasa. Ukiangalia huyu wazazi walimchelewa. Hv hujiuliz kwanini ni watoto wachache wa kiarabu wanaishi tofauti na tamaduni zao? Sisi tumepoteana kuhc kila kitu ni usasa. Nina binti ana miaka 23 na ninakuhakikishia akiwa kwenye dari langu atafuata kila nilichoratibu aisee. Acha niendelee kuitwa mkuda tu.
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Imani ya kikristo inazalisha Aesheists wengi mno mna sio imani sahihi ndo mna wengi wasioamini Mungu wametokea huko kwenye ukristo

Am proud to be a Muslim
 
Kupungukiwa imani ni tatizo linaletwa na usasa! Mama yako anakuelekeza njia iliyo njema. Sali sana uondokane na hako kashetani ka-usasa kalikokukamata.
 
Back
Top Bottom