Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Hivi wewe sindo uncle fujo au nimekosea??
 
Mimi sina tatizo na mtoto kuwa boda boda au muuza chipsi. Kuna baadhi ya wauza chipsi wanatengeneza pesa nzuri kuliko wavaa tai wengi kwenye viyoyozi. Huenda hiyo elimu aliyosoma (hata kama ni unrelated) ndio imempa huo mwanga na hayo maono ya kuifanya hiyo biashara yake ya chipsi kwa namna anavyoifanya na kupelekea kupata faida anayoipata.


 
Hawa watu wa benki ndiko wanakotajirikia.

Unakuna mtu ana akaunti yake ya siri ambayo familia haijui.

Anapata majanga huko hakuna anayejua kama kuna mahali kaweka fedha zake na kiasi gani .

Basi wahusika baada ya kuona muda mrefu umepita hakuna anayejitokeza wanapita nazo.

Ubinafsi kupitiliza ni mbaya.
 
Hivi baba ako akikusomesha kwa gharama kubwa mpaka chuo kikuu then ukaishia kuwa bodaboda. Hivi baba ako akikukuta pale kijiweni mnakopaki pikipiki hivi cjui mnaangalianaje? Unajisikiaje akikuangalia usoni? Ukiwa unasubiria abiria HV baba ako unaweza kumwangalia usoni kweli?....

I can't imagine kichwa kinaniuma.
 
Poleni sana!
thisi timu nisingependa kuchangia sana ila ifikapo Februari kuna kitu nataka nijaribu kikifanikiwa nitakuja hapa kwa majibu mengine ambayo kwa imani yangu yaweza kuwa msaada!
binafsi nimechoka kulalamika natamani tufike sehemu tuamue nini cha kufanya hata kama itachukua muda mrefu au tutapata hasra lakini ifike wakati wa kutenda kwa kadri ya uwezo wetu.
miaka ya nyuma nilialikwa na kituo kimoja cha compassion nikawatie nguvu ili waweze kukusanya mtaji na waweze kukopeshana. lakini sura zilivyokuwa zimekata tamaa kidogo nishindwe pa kuanzia yaani choka mbaya!
lakini ghafla wazo likaja niwaulize matumizi ya sukari kwa watoto wao ni kiasi gani kwa kila wiki? kiukweli nilipata majibu ambayo sikuyategemea yakaonekana ni makubwa na kati yao wapo wanatumia zaidi ya tano ndani ya wiki mbili! nikagundua kuwa naongea na matajiri na sio kama ninavyofikiria.
hivyo tukaanzisha duka la dharura(bubu) ili kila mwanachama akihitaji sukari aje anunue kwenye kituo na jinsi unavyonunua kwa wingi ndivyo utarajie faida kubwa mwisho wa mwaka.
walifanya na wakagawana faida iliyowatosha na wengine ili waweze kuchukua sukari nyingi walianzisha biashara zinazoweza kuwasaidia kuongeza matumizi ya sukari kwa kupika vitafunwa na kuuza. siwakumbuki tena lakini wengi wao walishabadilika sana.
sasa nini nataka kusema kama hatuwezi kubadili mtazamo na kufanya tofauti hakuna jinsi ambavyo tutaweza kufanikiwa.
lazima tujitume na kwakweli ifike wakati tunaweza kugoma kuchukua bidhaa kwa hao matajiri na tukainuana wenyewe na wao wabaki kama wauzaji wa jumla.
 
Heshima yako mkuu Sean Paul

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Heshima kwetu sote mkuu.
Raia wanaona kuvaa tai ndio heshima na status. Halafu tukipita na magogo yetu toka porini tunakuja kuuza mbao mjini wanatuomba rushwa.
Anakagua vibali vyote vimetimia. Mzigo haujazidi hata nusu kilo, lakini anakuambia umpe hata ya maji........
Hiyo mil 20 ya kukopa unarudisha miaka 5. Sisi huku tunaitengeneza ndani ya miezi kadhaa.
Nakiri si kazi rahisi, businesses are full of chaos.
 
Iwapo wauza chipsi na bodaboda wote wataamua leo hii kuacha hizo kazi, trust me tutatamani warejee. Kila mmoja ana umuhimu wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…