TANZIA Mzee Said Mohamed (baba yake GSM) afariki dunia
Hivi hii tabia ya kurudia habari ile ile ambayo mwenzio kapost kitaalam inaitwaje?
 
Mimi binafsi naamini katika generational wealth creation.

Huyo kaanzisha biashara

Biashara ikapass kwa wanawe na wanawe wataipass kwa watoto hadi wajukuu

Tatizo sisi waafrika tunatimuliwa home mapema sana bila "mpango ukwasi"

Matokeo yake kila kizazi huanza moja mwisho wote hufaa masikini au masikini wenye afadhali

Au once wealth creator akifa hakuna successional plan ukwasi hupotea mazima wahuni huuza kila kitu

Cheki hio familia, halafa cheki dewji family halagu cheki mengi family halafu cheki bakhersa family ana wengine wengi especially asians

Ngozi nyeusi tuna la kujifunza
Uko sahihi iliniuma sana Tajiri mfanyabiashara mwenye biashara kibao ikiwemo Imalaseko supermarket mbunge wa Kahama mzee Kishimba akilalamika bungeni live kuwa mwanae amemaliza degree Serikali haijamwajiri!!! Inatisha msomi huyo mwanawe kashindwa kumpachika kwenye biashara zake?
 
Wanachofanya hawa jamaa hawagawanish mali baada ya mmiliki wa kwanza kuondoka,sasa sisi mmilik akifa tunataga tugawane kila mtu awe na chake mwisho wa siku tunashndwa kuendeleza
Una hoja nzito
 
sio kweli, utajiri wao umepatikana kwenye serikali ya kikwete na mke wake, they are affiliated to their wealth
Sawa...ila ukijiongeza utaielewa vzr comment yangu hiyo

Ova
 
Wanachofanya hawa jamaa hawagawanish mali baada ya mmiliki wa kwanza kuondoka,sasa sisi mmilik akifa tunataga tugawane kila mtu awe na chake mwisho wa siku tunashndwa kuendeleza
Ha ha ha nyumba ya kupangisha ya marehemu uswahilini unakuta wamegawana vyumba

Matengenezo ya jumla nyumba ikichoka hakuna wa kufanya kuchangia hawataki na maeneo ya jumla kama choo kikijaa hawataki kuvuta hadi wapangaji wanahama kwa hasira na nyumba kukosa wapangaji hadi inabomoka
 
Sio ndefu wala, huoni mzee katengeneza kizazi chake ndio kinafaidi
Ukizaliwa kwenye familia maskini ni bahati sana kuwa tajiri mkubwa ghafla isipokua inabidi tu utengeneze mazingira mazuri kwa kizazi chako kuwa matajiri wakubwa usiwe mbinafsi utafute mali na utengeneze mazingira mazuri kwa kizazi chako kijacho

Tatizo sisi wengi ni wabinafsi ukipata hela huwazi kuweka mazingira mazuri kwa kizazi chako ila unakula bata kwanza, mwsho wa siku kizazi chako kila siku kinaanza moja unamfukuza kwako aende akapangishe huko ili aanze sifuri Kama wewe

Hizo ni tabia za kimasikini
 
sio kweli, utajiri wao umepatikana kwenye serikali ya kikwete na mke wake, they are affiliated to their wealth
Mbona wewe serikali ya awamu ya 5,6 hazijakutajirisha ? Mkuu kwema lakini? 😂😂😂
 
Ukizaliwa kwenye familia maskini ni bahati sana kuwa tajiri mkubwa ghafla isipokua inabidi tu utengeneze mazingira mazuri kwa kizazi chako kuwa matajiri wakubwa usiwe mbinafsi utafute mali na utengeneze mazingira mazuri kwa kizazi chako kijacho

Tatizo sisi wengi ni wabinafsi ukipata hela huwazi kuweka mazingira mazuri kwa kizazi chako ila unakula bata kwanza, mwsho wa siku kizazi chako kila siku kinaanza moja unamfukuza kwako aende akapangishe huko ili aanze sifuri Kama wewe
Kifupi kupima mafanikio ya maisha ya mtu usimwangalie yeye mzazi angalia watoto wake
 
Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara

Hiyo ndio moja ya tafauti kubwa kati ya watu wa ngozi nyeupi na watu wa ngozi ya kiza. Yani mzee alistaafu miaka 25 nyuma akaachia wanawe waendeleze biashara. Mzee wa kiafrika mtoto hua anapata tabu sana hata baba akiwa na mkwanja. Yeye bado hujiona ndio anaakili nyingi hata kama zama zake zimeshapita.
 
Back
Top Bottom