Nilisoma mahali hii kesi mwanzoni ilikuwa na washtakiwa 6, DPP akawaondoa 3 wakabaki 3 ndio akaongezwa Mbowe. Sifahamu Kwa nini hili halisemwi sana, pengine kuna jambo ndani yake. Hawa watatu DPP alioamua hana nia ya kuendelea nao ndio wanaozungumziwa? Waliachiwa na DPP aliyepita au wa sasa? Kwa makubaliano gani?
Lingine nililoliona ni imani inayoendelezwa kwamba kuteua wapinzani kwenye serikali kusaidia kujenga taifa ndio suluhu. Kwamba majibu ya madai ya mabadiliko ya katiba, yatakayoleta chaguzi huru, kurudisha mamlaka kwa wananchi kuteua (na kutengua) wawakilishi wao, uhuru wa mahakama, jeshi la polisi lisiloingiliwa, kurudisha uwajibikaji wa viongozi, na mambo mengine yaendanayo na katiba inayopiganiwa, ni kuteua wapinzani kwenye serikali wasaidie kujenga nchi. Kwamba hata pale Rais atakapokutana nao, akiwaoffer vyeo mambo yatakuwa sawa. Pengine ndio maana Zanzibar wameishia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa bila kuonekana Kwa nia ya dhati ya mabadiliko ya kweli, na mapengo yameanza onekana.