Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mkuu umeniwahi tu.Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo.
Pamoja na mapungufu yake Magufuli alikuwa na watu wake (inner circle) aliowaamini waliokuwa wanampatia taarifa sahihi hasa za ndani, SSH hana anategemea watu wa system ambao wengi wao wana ajenda zao binafsi ikiwemo ya kumpata mrithi baada yake.
Kwamba Marekani wakimaliza uchaguzi hakuna mikutano ya hadhara wala maandamano, it’s wrong, hadi leo Trump anafanya mikutano, Marekani maandamano ni kila siku tumeona wakati wa ‘Black Lives Matters’ nk nk.
Kwamba yeye (Samia) hawezi kuingilia kesi iliyo mahakamani wakati huo huo anazungumzia maendeleo ya kesi iliyopo mahakamani, kuwa, wanaoshitakiwa kwa ugaidi pamoja na Mbowe kesi zao zimeshasikilizwa na wanatumikia vifungo kabaki Mbowe, hii ni kama keshamhukumu Mbowe anawajenga watu kisaikolojia kuwa kama wenzake wamehukumiwa lazima Mbowe naye atumikie kifungo, hii sio sahihi.
Kwamba, Mbowe alikimbilia Kenya akaanza kupanga ugaidi, kidiplomasia hili halina afya linaweza kusababisha mgogoro kuwa Kenya inahifadhi watuhumiwa wa kigaidi.
Kama Rais mwenyewe anaitangazia dunia kuwa kuna watu Tanzania wamehukumiwa kwa ugaidi anategemea investor gani ata invest kwenye nchi ya magaidi, it’s just a common sense kulitambua hilo.
Haya ni machache kati ya mengi niliyoyaona kuhusiana na uwezo wa Rais kuchambua mambo kwa hadhi ya urais. Kama ni wasaidizi wake wanampotosha ama yeye kwa makusudi anaamua kupotosha, basi yampasa awe na uwezo wa kugundua na kujua madhara yake.
Leo kuna watu wameanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa Samia (kiuongozi).
Ndio maana nikasema naanza kuwaelewa watu hasa ‘Sukuma Gang’ kina Gwajima, Polepole, Bashiru wanaoonyesha wazi kutofautiana na Mwenyekiti wao, pamoja na sababu kutosemwa lakini wana send message kuhusiana na uwezo wa rais.
Nami nimeanza kupata wasi wasi kuwa Rais Samia kawekwa mtu-kati na wahafidhina wa Mwenda zake.
Tukumbuke kesi ya Mbowe, Mama kakiri, kuwa ilianza kuasisiwa mwaka jana mwezi wa tisa.
Huu ulikuwa wakati wa Mwenda zake.
Mwenda zake anajulikana mahsusi kwa kubambika kesi ili kumfanyizia hasimu wake.
Hatujasahau alivyobambikwa kesi ya uhujumu mzee Shamte wa Mkonge Tanga na hatimae kufia gerezani.
Je tumesahau kesi 147 ambazo mama mwenyewe alizifuta kule TAKUKURU, makesi ya ubambikaji ambayo yalimg'oa Jenerali Mbung'o?
We can only draw one conclusion, Mam anazidiwa nguvu ya reforms, kuna watu wanampinga wazi wazi kwa kumpa juiced information.
Kwamba Polepole na Gwajima wako fore front kumpinga juu ya covid, si suala la coincidence.