wakati ndio nilikua naanza kujipata tu kimaisha,
siku moja dada yangu aliniomba nimsindikize kanisani kwa nabii ambae sikumfahamu kabla na mpka leo sijui jina lake, ila kwa sura ndiyo huyo muungwana hapo kwa video. Kwakua nilikua na usafiri wangu na dada alikua na watoto, basi nikakubali kumsindikiza mpaka hapo kanisani somewhere mbezi beach hapo katikati, na siku hiyo nami nikawa sehemua ya waamini wa kanisa hilo.
katikati ya ibada,
huyo muungwana ambae ni nabii wenu si akaniita mbele ya waamini kanisani!
akaanza mbwembwe sasa, mmemuona huyu kijana alikua na pesa mingi sana kabla ila sasa hivi amevaa vizuri amependeza na kitambi chake, unaweza ukadhani ana pesa na cheo kikubwa sana serikalini lakini kumbe hana hata kazi wala hata elfu2mfukoni
nikajisemea moyoni nimuwashe makofi huyu muhuni au nimuache kwanza anipandishe mori vizuri ili nimpige uppercut chembe la kidevu, nimkalishe chini ya madhabahu yake halafu niseme mapepo yalinipanda? maana anazingua sana.
akaendeleza ngonjera zake ya unabii uchwara,
eti ooh kuna mwananmke maji ya kunde jina lake linaanza na herufi A huyo hakufai na ndie anakula peasa zako. Wakati huo sina hata demu. Nikajisemea tena moyoni huyu fala kweli anawarubuni watu kindezi sana.
Akaja kuni kera zaidi.
alipokuja kuanza kunichonganisha na members wa familia yangu, kwamba eti hali ngumu ya kiuchumi niliyoku nayo japo si kweli, eti anaeitatiza kichawi ni mtu mwenye jina linaloanza na herufi J ndani ya ukoo wangu, eti na kuna mwingine jina lake linaanza na hefufi C, n.k
Nikajisemea moyoni this is nonsense.
apeleke utabiri wake kwa wajinga wengine huko but not me and other Tanzanians with constitutional mandate and responsibilities ya kuwatumikia na kuwaletea waTanzania maendeleo kijamii, kisiasa na kiuchumi.
