Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Hili ni jibu la swali lako hapo juu.
Una unganisha majibu ya maswali mawili tofauti.

Una unganisha majibu yangu ya maswali mawili tofauti kuleta Contradiction.

Hilo jibu la kwanza ni specific kwa binadamu.

Hilo jibu la pili ni la kuku (Broilers) ambao ni man made.
 
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu.
Tumia kichwa chako vizuri mzee,unauliza swali unajibiwa bado unauliza tena swali lile,husomi kilichoandikwa au huwezi digest!?
Nimeshakwambia kwamba unaweza kupima upepo kwa sababu upo.

Hatupimi upepo kwa kuangalia athari zake.

Upepo unapimwa kila siku kwenye vituo vya hali ya hewa kujua kasi yake na uelekeo wake.

Marubani na manahodha wa meli kila mara wanapewa updates za speed and direction za upepo, kwa sababu upo na unapimika.

Sasa wewe thibitisha uwepo wa huyo Mungu.
Vipimo vya upepo vinapima thrust/athari ya upepo,haviupimi upepo
 
Hilo jibu la pili ni la kuku (Broilers) ambao ni man made.
Binadamu hatengenezi chochote badala yake huwa anaweka/Sogeza/kuongeza favorable conditions za KITU kipya kujitengeneza chenyewe.

Hizi favorable conditions siyo lazima ziwekwe na binadamu sometime zipo tu kulingana na hali ya hewa.
Na ndicho kilichotokea kwenye evolution ya Binadamu, natural conditions ndizo zilifanya A-exist na awepo kwa rangi tofauti.
 
Tumia kichwa chako vizuri mzee,unauliza swali unajibiwa bado unauliza tena swali lile,husomi kilichoandikwa au huwezi digest!?
Thibitisha uwepo wa Mungu, yeye kama yeye.

Acha kuleta ufafanuzi uchwara na janja janja.

Usitumie vitu vilivyopo kufosi kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.

Mthibitishe huyo Mungu, yeye kama yeye.
Vipimo vya upepo vinapima thrust/athari ya upepo,haviupimi upepo
Una elewa maana ya neno athari?
 
Thibitisha uwepo wa Mungu, yeye kama yeye.

Acha kuleta ufafanuzi uchwara na janja janja.

Usitumie vitu vilivyopo kufosi kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.
Sijatumia upepo kusema umeundwa na huyo Mungu,najua huamini huyo mungu,nilitoa mfano wa umeme pia,hii inaonesha kiasi gani una kichwa kizito,rejea maelezo yangu ya mfano wa upepo,usome uelewe,kama umelewa subiri pakuche,pombe ziishe,ukasome tena
Mthibitishe huyo Mungu, yeye kama yeye.

Una elewa maana ya neno athari?
Athari ni neno la kiarabu, unadhani mimi muislam na wewe kafiri nani analielewa zaidi neno athari!?
 
Kajificha wee hatimaye kaamua kuweka hadharani kila kitu.

Huwezi ukawa mtumishi wa Mungu ukaacha kuyaamini maandiko matakatifu.
 
Binadamu hatengenezi chochote badala yake huwa anaweka/Sogeza/kuongeza favorable conditions za KITU kipya kujitengeneza chenyewe.
Kama binadamu hatengenezi chochote, nyumba🏠 huwa zina jitengeneza zenyewe?

Binadamu yeye anasogeza cement, mchanga, matofali na mabati kisha vinajiunda vyenyewe si ndivyo?
Hizi favorable conditions siyo lazima ziwekwe na binadamu sometime zipo tu kulingana na hali ya hewa.
Ndio maana nilikwambia mwanzoni, ndivyo asili ilivyo. Ukawa unabisha.
Na ndicho kilichotokea kwenye evolution ya Binadamu, natural conditions ndizo zilifanya A-exist na awepo kwa rangi tofauti.
 
1. Kama muandishi gani anaejulikana PASIPO SHAKA YOYOTE kwamba yeye ndio aliandika hicho kitabu?

2. Tuna uhakika gani kwamba hao walionakili: a) Walielewa kile walichokuwa wananakili b) Walinakili kwa usahihi c)Waliwakilisha kwa usahihi kile walicho nakili bila kupoteza maana?

3. a)Yeshua ina ugumu gani kutamkika mpaka watu waamue kutohoa?
b) Mungu sio jina, Allah ni jina, God sio jina. Mungu yoyote anaweza kuitwa Mungu/God ndio maana kuna miungu lukuki. Mungu wa wakristo ana jina lake, cha ajabu hakuna anaelitumia .

Hivi vitu vimefanywa kwa makusudi sio bahati mbaya.
1. Wewe una uhakika gani hilo jina la ukoo unalotumia ndio lilikuwa la babu za baba zako?

2. Kuhusu walionakili nafikiri kuna sehemu nimeandika waliongeza na kupunguza baadhi ya maneno. Na imegundulika baada ya kipatikana hati za kale zenye hivyo vitabu.

3. Ukibisha kuwa Mungu ni jina inaleta shida kidogo. Mwishowe utasema baba sio jina.

Kila jambo linafanywa kwa kusudi maalumu.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.

View attachment 3279501

MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.

Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.

Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?

Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?

Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?

Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.

Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.

Nawasilisha.
​
Huyu hajui anachosema. Anajidhihirisha tu kuwa ni nabii wa ibilisi.
 
Ndio maana nilikwambia mwanzoni, ndivyo asili ilivyo. Ukawa unabisha.
Lakini hii Asili haikuzalisha binadamu wa rangi tofauti bali binadamu wa Rangi moja ndio alianza Kisha asili hiyohiyo ikaendelea kuleta effect za kuzaliwa Rangi tofauti tofauti.

Na hapa nikiongelea Asili namaanisha Mazingira yanayokizunguka kiumbe husika.

Kulingana na Mazingira yaliyokuwa yanamzunguka bacteria miaka millions kadhaa iliyopita ndiyo yalipelekea uwepo wa Binadamu.
 
Kama binadamu hatengenezi chochote, nyumba🏠 huwa zina jitengeneza zenyewe?

Binadamu yeye anasogeza cement, mchanga, matofali na mabati kisha vinajiunda vyenyewe si ndivyo?
Nyumba siyo BADILIKO JIPYA. Kitu kipya nimemaanisha Chemical Changes
 
Lakini hii Asili haikuzalisha binadamu wa rangi tofauti bali binadamu wa Rangi moja ndio alianza Kisha asili hiyohiyo ikaendelea kuleta effect za kuzaliwa Rangi tofauti tofauti.
Binadamu mwenyewe ni sehemu ya asili hiyohiyo.

Ukisema binadamu wa rangi moja ndio alianza, Je ni binadamu wa rangi ipi?

Nyeupe au nyeusi?

Hapo tayari kutakuwa na maswali yenye utata.
Na hapa nikiongelea Asili namaanisha Mazingira yanayokizunguka kiumbe husika.

Kulingana na Mazingira yaliyokuwa yanamzunguka bacteria miaka millions kadhaa iliyopita ndiyo yalipelekea uwepo wa Binadamu.
Binadamu ni sehemu ya asili.

Binadamu tumekuwepo ulimwenguni milele.

Labda kama tuamue kujipoteza wenyewe, wote kabisa tufutike kwenye uso wa dunia.
 
Back
Top Bottom