Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Hili ni jibu la swali lako hapo juu.
Una unganisha majibu ya maswali mawili tofauti.

Una unganisha majibu yangu ya maswali mawili tofauti kuleta Contradiction.

Hilo jibu la kwanza ni specific kwa binadamu.

Hilo jibu la pili ni la kuku (Broilers) ambao ni man made.
 
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu.
Tumia kichwa chako vizuri mzee,unauliza swali unajibiwa bado unauliza tena swali lile,husomi kilichoandikwa au huwezi digest!?
Vipimo vya upepo vinapima thrust/athari ya upepo,haviupimi upepo
 
Hilo jibu la pili ni la kuku (Broilers) ambao ni man made.
Binadamu hatengenezi chochote badala yake huwa anaweka/Sogeza/kuongeza favorable conditions za KITU kipya kujitengeneza chenyewe.

Hizi favorable conditions siyo lazima ziwekwe na binadamu sometime zipo tu kulingana na hali ya hewa.
Na ndicho kilichotokea kwenye evolution ya Binadamu, natural conditions ndizo zilifanya A-exist na awepo kwa rangi tofauti.
 
Tumia kichwa chako vizuri mzee,unauliza swali unajibiwa bado unauliza tena swali lile,husomi kilichoandikwa au huwezi digest!?
Thibitisha uwepo wa Mungu, yeye kama yeye.

Acha kuleta ufafanuzi uchwara na janja janja.

Usitumie vitu vilivyopo kufosi kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.

Mthibitishe huyo Mungu, yeye kama yeye.
Vipimo vya upepo vinapima thrust/athari ya upepo,haviupimi upepo
Una elewa maana ya neno athari?
 
Thibitisha uwepo wa Mungu, yeye kama yeye.

Acha kuleta ufafanuzi uchwara na janja janja.

Usitumie vitu vilivyopo kufosi kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.
Sijatumia upepo kusema umeundwa na huyo Mungu,najua huamini huyo mungu,nilitoa mfano wa umeme pia,hii inaonesha kiasi gani una kichwa kizito,rejea maelezo yangu ya mfano wa upepo,usome uelewe,kama umelewa subiri pakuche,pombe ziishe,ukasome tena
Mthibitishe huyo Mungu, yeye kama yeye.

Una elewa maana ya neno athari?
Athari ni neno la kiarabu, unadhani mimi muislam na wewe kafiri nani analielewa zaidi neno athari!?
 
Kajificha wee hatimaye kaamua kuweka hadharani kila kitu.

Huwezi ukawa mtumishi wa Mungu ukaacha kuyaamini maandiko matakatifu.
 
Binadamu hatengenezi chochote badala yake huwa anaweka/Sogeza/kuongeza favorable conditions za KITU kipya kujitengeneza chenyewe.
Kama binadamu hatengenezi chochote, nyumba🏠 huwa zina jitengeneza zenyewe?

Binadamu yeye anasogeza cement, mchanga, matofali na mabati kisha vinajiunda vyenyewe si ndivyo?
Hizi favorable conditions siyo lazima ziwekwe na binadamu sometime zipo tu kulingana na hali ya hewa.
Ndio maana nilikwambia mwanzoni, ndivyo asili ilivyo. Ukawa unabisha.
Na ndicho kilichotokea kwenye evolution ya Binadamu, natural conditions ndizo zilifanya A-exist na awepo kwa rangi tofauti.
 
1. Wewe una uhakika gani hilo jina la ukoo unalotumia ndio lilikuwa la babu za baba zako?

2. Kuhusu walionakili nafikiri kuna sehemu nimeandika waliongeza na kupunguza baadhi ya maneno. Na imegundulika baada ya kipatikana hati za kale zenye hivyo vitabu.

3. Ukibisha kuwa Mungu ni jina inaleta shida kidogo. Mwishowe utasema baba sio jina.

Kila jambo linafanywa kwa kusudi maalumu.
 
Huyu hajui anachosema. Anajidhihirisha tu kuwa ni nabii wa ibilisi.
 
Ndio maana nilikwambia mwanzoni, ndivyo asili ilivyo. Ukawa unabisha.
Lakini hii Asili haikuzalisha binadamu wa rangi tofauti bali binadamu wa Rangi moja ndio alianza Kisha asili hiyohiyo ikaendelea kuleta effect za kuzaliwa Rangi tofauti tofauti.

Na hapa nikiongelea Asili namaanisha Mazingira yanayokizunguka kiumbe husika.

Kulingana na Mazingira yaliyokuwa yanamzunguka bacteria miaka millions kadhaa iliyopita ndiyo yalipelekea uwepo wa Binadamu.
 
Kama binadamu hatengenezi chochote, nyumba🏠 huwa zina jitengeneza zenyewe?

Binadamu yeye anasogeza cement, mchanga, matofali na mabati kisha vinajiunda vyenyewe si ndivyo?
Nyumba siyo BADILIKO JIPYA. Kitu kipya nimemaanisha Chemical Changes
 
Lakini hii Asili haikuzalisha binadamu wa rangi tofauti bali binadamu wa Rangi moja ndio alianza Kisha asili hiyohiyo ikaendelea kuleta effect za kuzaliwa Rangi tofauti tofauti.
Binadamu mwenyewe ni sehemu ya asili hiyohiyo.

Ukisema binadamu wa rangi moja ndio alianza, Je ni binadamu wa rangi ipi?

Nyeupe au nyeusi?

Hapo tayari kutakuwa na maswali yenye utata.
Na hapa nikiongelea Asili namaanisha Mazingira yanayokizunguka kiumbe husika.

Kulingana na Mazingira yaliyokuwa yanamzunguka bacteria miaka millions kadhaa iliyopita ndiyo yalipelekea uwepo wa Binadamu.
Binadamu ni sehemu ya asili.

Binadamu tumekuwepo ulimwenguni milele.

Labda kama tuamue kujipoteza wenyewe, wote kabisa tufutike kwenye uso wa dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…