Nabii Mwingira ni Ishara ya kukubalika kwa Rais Samia

Nabii Mwingira ni Ishara ya kukubalika kwa Rais Samia

Mama Samia Mitano tena
Na akimaliza aje Hussein Mwinyi na akimaliza Mwinyi aje Makame Mbarawa na amalizie Othman Masoud
Wanzanzibar hawana lawama kwenye hili wacha tu watawale, tuliwatafuta wenyewe. Nyerere aliwaleta wakaja, tulieni hapohapo. Hata katiba iliyomleta Rais Samia waliiandika watanganyika wenyewe kwa mikono yao. Wazanzibar tuliwachelewesha mambo mengi sana kwa kuwa kwenye muungano.
 
Kama awamu ni ileile mbona sasa hakuna wananchi wanaopotea? Mbona watu wasiojulikana wamepotea ghafla, mbona wanaharakati wa kujitegemea hawapo? Mbona wafanyabiashara hawanyang'anywi hela zao na TRA, mbona watumishi wamelipwa mafao yao, mbona rais hagawi hela ovyo mitaani?
Bado tupo awamu ya tano ndugu, hao wote waliopo madarakani waliingia madarakani kwa wizi wa kura ktk uchaguzi wa 2020, ukitaka kuifanya hii serikali itofautiane na ya JPM subiri uchaguzi ufanyike.

JPM alikuwa anagawa hela ila hakuwa mzurulaji wa kwenda kula bata nchi za nje

Mama hagawi hela, ila anatumia hela nyingi kwenda kuzurura huko nchi za nje akiwa na msafara wa kutisha. Kwa hiyo Samia ana matumizi mabaya ya kodi zetu kama ilivyo desturi ya watawala wote waliitoka CCM
 
Mwingira ni mwizi kama wezi wengine.Mcha Mungu hawezi kudhulumu ardhi ya watu kwa utajiri wake tena kwa dhulma ya wajinga.Kama anafikiri ana haki na mashamba arudi kuyachukua aone muziki wake.Biblia inakataza kuhukumu na kusingizia uongo.
Hebu tukumbushe namna alivyonyang'anya watu hayo mashamba yao. Na namna alivyowazuia watu wasiweze kwenda kudai haki yao kwenye vyombo vya sheria.
 
Ingia barabarani uandamane.

Samia ni Rais.

Na Mbowe na Lissu hawatakuwa rais wa Tanzania mpaka WANAKUFA.

Huo ndio UKWELI MCHUNGU hutaki JIUE.
Ungesema mwaka 2020 kuwa mama atakuwa Rais 2021 tungekuamini. Sasa unabii umeuanza Leo kwa sababu ya kumfurahisha.
 
Aisee umeongea point kubwa, bora tutawaliwe na wazanzibar, hii mitanganyika mingi ni miuaji na mijizi
Lazima tukubali, ustaarabu Zanzibar uliingia zamani sana kuliko Tanganyika ya kanda ya Ziwa na kati. Ndio maana hadi leo kuna wanaouana kwa uchawi wa macho mekundu.
 
chief hangaya awe makini sana na hizi sifa za kumpwaga....asisahau nae ni mshiriki wa awamu ya 5
Ile ilikuwa serikali ya magufuli tu baasi. Wengine walikuwepo tu kwa mujibu wa katiba yetu. Inawezekana Makonda alikuwa na sauti kuliko mama Samia kwenye serikali ile.
 
Yaani anasema Ikulu Yuko shetani na anayeongoza Ikulu ni mtoto wa shetani.
Halafu unasema anakubalika?mtamhadaa Hangaya mpaka lini?
Yaani kwa tozo,watu wanakataliwa huduma za matibabu mpaka wachanjwe,halafu unasema anapendwa?
Kuna watu hawana vyoo mpaka leo unafahamu? Je waachwe kwakuwa ni hiari yao kutumia au kuacha kutumia choo?
 
Huyu bibi acheni kumdanganya hakuna mtu wa bara anayemtaka wala kumpenda ni kwamba basi watu wamekaa kimya lakini hatumtaki
Hizo takwimu za watu wa bara wanaomchukia Samia umezipataje? Yaani ukivimbiwa makande na wanao ndipo mnajiona ndiyo Tanzania bara??

Kwa taarifa yako viongozi WAISLAMU wanaleta utulivu wa nchi kuliko Wakristu. Tutegemee makubwa kwa Samia
 
Hizo takwimu za watu wa bara wanaomchukia Samia umezipataje? Yaani ukivimbiwa makande na wanao ndipo mnajiona ndiyo Tanzania bara??

Kwa taarifa yako viongozi WAISLAMU wanaleta utulivu wa nchi kuliko Wakristu. Tutegemee makubwa kwa Samia
Nendeni huko kwenu mbona hampataki? Kwani bara hakuna waislamu?
 
Madai ya Askofu Jesephat Mwingira wa kanisa la EFATHA aliyoyatoa kwenye sherehe za Christmas aliyatoa sasa baada ya kuwa na Imani na serikali ya mama Samia. Aliona utu, uchaMungu wa dhati na utukufu ndani ya Rais Samia hivyo kuuona wakati wa kuyabwaga yote wakati huu ya moyoni mwake aliyofanyiwa kwenye awamu zilizopita. Hii ni sawa na watoto wanaoshitaki kwa mama yoote waliyofanyiwa na house girl wao wakati mama hayuko nyumbani.

Ni malalamiko ya hope kwa serikali yao ya awamu ya sita. Hii ni kusema kuwa Mama ana kazi kubwa sana ya kuliunganisha taifa kuliko anavyofikiria. Mwingira sio mjinga kwa kiasi hiki anachofikiria Mh. Simbachewene. Mimi ninaiona dhamira safi ndani ya Nabii Mwingira, na wako wengi wenye shida kama ya Mwingira. Asichukuliwe poa au kukegeliwa.

Angekuwa mimi ndiye Rais Samia ningeanzia kwa Nabii Mwingira kuelekea kuwatambua wengine wenye malalamiko genuine kama haya. Wasitishwe bali wapewe moyo wayafichue yote.
Wewe umewezaje kumuelewa Mwingira ukashindwa kumuelewa Simbachawene?
Iko hivi, Simbachawene amemuelewa Mwingira kama ulivyomuelewa wewe - tofauti ni wewe huna cha kufanya baada ya kumuelewa Mwingira! Ila Simbachawene ameamuru Mwingira ahojiwe kwa undani ili hata yale ambayo hakuweza kuyataja pale Kanisani yajulikane aweze kusaidiwa!
 
Hizo takwimu za watu wa bara wanaomchukia Samia umezipataje? Yaani ukivimbiwa makande na wanao ndipo mnajiona ndiyo Tanzania bara??

Kwa taarifa yako viongozi WAISLAMU wanaleta utulivu wa nchi kuliko Wakristu. Tutegemee makubwa kwa Samia
Awamu iliyopita ilikuwa ya giza. Hata akina dudubaya walijiita conc master. Sitamani inikute tena awamu ya aina ile.
 
Wewe umewezaje kumuelewa Mwingira ukashindwa kumuelewa Simbachawene?
Iko hivi, Simbachawene amemuelewa Mwingira kama ulivyomuelewa wewe - tofauti ni wewe huna cha kufanya baada ya kumuelewa Mwingira! Ila Simbachawene ameamuru Mwingira ahojiwe kwa undani ili hata yale ambayo hakuweza kuyataja pale Kanisani yajulikane aweze kusaidiwa!
Awamu hii ya sita lazima itoe suluhisho la jumla kwakuwa walioumizwa na awamu ya tano ni wengi sana sana sana sana. Fikiria tu mfano wa watumishi woooote wakiwemo polisi hawakuongezewa mshahara kwa miaka 6. Suppliers na makandarasi hawakulipwa fedha zao. Kuna saupplier mmoja aliilisha taasisi ya umma huko Morogoro, hakulipwa hadi akishindwa kulipa ada ya mwanawe chuo kikuu hadi mtoto akakosa mitihani mpaka leo anahangaika na kurudia masomo mwaka mzima.

Akina Mwingira ni kipande kidogo tu kinachoonekana cha meli iliyozama majini. Suluhu ya jumla lazima ifanyike pamoja na kuwalipa wanaoidai saerikali
 
Ingia barabarani uandamane.

Samia ni Rais.

Na Mbowe na Lissu hawatakuwa rais wa Tanzania mpaka WANAKUFA.

Huo ndio UKWELI MCHUNGU hutaki JIUE.
Mbowe na Lissu wameingiaje kwenye hoja hii?????
 
Back
Top Bottom