NAFASI YA AJIRA: Kijana Mwenzangu Chukua Mkopo wa Kusambaza Nishati Safi ya Kupikia mijini na vijijini (Ni fursa kubwa sana hii)

NAFASI YA AJIRA: Kijana Mwenzangu Chukua Mkopo wa Kusambaza Nishati Safi ya Kupikia mijini na vijijini (Ni fursa kubwa sana hii)

Zinafanana kwa kiasi fulani ila ni tofauti.

Reducing Balance Interest: Riba inatozwa kila mwezi kulingana na salio linalobaki. Kadri unavyolipa deni, kiasi cha riba kinapungua kwa sababu msingi wa hesabu unapungua.

Compound Interest: Riba inayozalishwa huongezwa kwenye mkopo wa awali (principal), na riba mpya huhesabiwa juu ya jumla hiyo (interest on interest).
Hivyo, Reducing Balance haiwezi kuitwa Compound Interest kwa sababu haiongezi riba kwenye riba iliyopita; inahesabu tu riba kwa salio linalobaki.

Ukilipa Mkopo Wote kwa Miezi 12 kwa mkupuo, Je Riba Itakuwa 12%?

Kwa kawaida, reducing balance inahesabu riba ya kila mwezi kulingana na kiasi kilichobaki. Ukilipa kidogo kidogo, riba inapungua. Lakini ukilipa kwa mkupuo baada ya miezi 12, bado utakuwa umelipa riba kwa kila mwezi uliopita.

Ikiwa hakuna penalty ya kulipa mapema, basi utalipa riba halisi iliyokusanywa hadi mwezi huo wa 12. Kwa hiyo, huwezi kulipa 12% ya mkopo mzima kama kwenye flat rate. Badala yake, utalipa kiasi kidogo kwa sababu riba ilihesabiwa kwa salio linalopungua kila mwezi.

Lakini... taasisi nyingi za kifedha zinaweza kuwa na early repayment penalty au ada za kufunga mkopo mapema. Hii inaweza kukufanya ulipie ada ya ziada ili kufidia mapato ambayo wangepata kama ungeendelea kulipa kwa miezi yote.

Mfano Mdogo

Uchukue mkopo wa TSh 1,000,000 kwa 12% kwa mwaka (reducing balance):

Ukilipa kidogo kidogo kila mwezi, unaweza kulipa riba ya jumla inayofikia karibu TSh 66,000 kwa mwaka.

Ukisubiri hadi mwisho wa miezi 12 na ulipie mkopo wote, hautalipa 12% ya TSh 1,000,000 (ambayo ingekuwa TSh 120,000). Badala yake, utalipa kiasi kilichokusanywa kwa miezi 12, ambacho ni kidogo kwa sababu riba ilihesabiwa kwa kiasi kilichobaki kila mwezi.
Grest! Simple and clear. Kweli wewe ni manager wa makampuni.

Sasa fungua kampuni yako uache kuandikia makampuni ya watu( jokes)
😃😃😃
 
FURSA KUBWA KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA!

View attachment 3220855

Benki ya NMB imetenga Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya Mikopo ya Miradi na Biashara za kusambaza Nishati Safi ya Kupikia kwa Watanzania.

SIFA ZA MKOPO:

Riba nafuu ya 1% kwa mwezi (12% kwa mwaka, reducing balance hivyo effective interest rate ni 6.6%).
Mkopo wa hadi Shilingi Bilioni 1 kwa mfanyabiashara mmoja.
Muda wa mkopo hadi miaka 2 – unachagua muda wa kulipa usiozidi miaka 2.

Fursa hii ni kwa Wasambazaji wa Mitungi na Majiko ya Gesi!

UUzinduzi wa mkopo ulifanyika mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akiongozana na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na uongozi wa Benki ya NMB.

Usikose fursa hii! Tembelea NMB kupata maelezo zaidi.
Wewe ndio meneja wa NMB?
 
Dhamana ya mkopo ni Hati ya nyumba!
Vijana hawana hati Wala nyumba!
Ni muda wa kujiongeza sasa, kununua viwanja vya serikali (halmashauri). Hapo jiji la Tanga wanauza viwanja vilivyopimwa kwa gharama ndogo tu ya kuanzia shilingi milioni 1. Mnaweza jichanga hata watatu mkapata kiwanja chenye hati na mkajenga nyumba ndogo tu mkaipaka rangi na kuweka alluminium ili kupandisha thamani, mkampooza na valuer aipandishe thamani, mpate mkopo kwa lengo la kuufanyia biashara na kuulipa. Ni njia ya kujiongeza kukidhi masharti ya kukopesheka.

Mnadanganya kwa faida, sio kukopa hela na kutolipa.

Jiangalizie viwanja hapo palipoandikwa LAND SALES, chagua Tanga jiji, Tunduru au Misungwi, ndio zipo plot za bei nafuu. Mbeya jiji vipo vya milioni 2 na kuendelea, mnajichanga hata 4
 
Nashukuru kwa ushauri mzuri !
Tatizo unanunua kiwanja cha Halmashauri Tsh 2m, ndio dhamani yake.
Kiwanja hicho unaweza kukutumia kukopea Tsh 100 m?
 
Aya mambo yaliwah kuja na hapo nyuma et kweny wilaya hela zimetolewa vijana mkakope daaah qumamae kbs, hakuna cha mama wazee ni usengeusenge mwingi kama wa airtel kukupa elfu ishirini kwenye account yako hahahahahah.
 
Kwenye gesi mambo hayapo hivyo. Limiti ya mkopo ni billioni mbili.
 
Back
Top Bottom