NAFASI YA AJIRA: Kijana Mwenzangu Chukua Mkopo wa Kusambaza Nishati Safi ya Kupikia mijini na vijijini (Ni fursa kubwa sana hii)

NAFASI YA AJIRA: Kijana Mwenzangu Chukua Mkopo wa Kusambaza Nishati Safi ya Kupikia mijini na vijijini (Ni fursa kubwa sana hii)

FURSA KUBWA KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA!

View attachment 3220855


Benki ya NMB imetenga Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya Mikopo ya Miradi na Biashara za kusambaza Nishati Safi ya Kupikia kwa Watanzania.

SIFA ZA MKOPO:

Riba nafuu ya 1% kwa mwezi (12% kwa mwaka, reducing balance hivyo effective interest rate ni 6.6%).
Mkopo wa hadi Shilingi Bilioni 1 kwa mfanyabiashara mmoja.
Muda wa mkopo hadi miaka 2 – unachagua muda wa kulipa usiozidi miaka 2.

Fursa hii ni kwa Wasambazaji wa Mitungi na Majiko ya Gesi!

UUzinduzi wa mkopo ulifanyika mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akiongozana na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na uongozi wa Benki ya NMB.

Usikose fursa hii! Tembelea NMB kupata maelezo zaidi.
Issue colateral...au wanatoa kwa mali kauli tu
 
Nashukuru kwa ushauri mzuri !
Tatizo unanunua kiwanja cha Halmashauri Tsh 2m, ndio dhamani yake.
Kiwanja hicho unaweza kukutumia kukopea Tsh 100 m?
Unaweza kukopea milioni 100, Inategemea akili yako umeichangamsha kiasi gani. Ndio nikaongeza na mawazo ya kujenga nyumba, na kuwapooza maafisa mikopo na mavaluer.

Ila katika hali ya kawaida, kama huna fedha ya kununua kiwanja cha milioni 2 unaanzaje kukomaa kukopa milioni 100!! Yaani ukiwa umechoka kabisa huna hela, huwezi kusema biashara ya milioni 5 kuwa ni ya kipuuzi na hivyo hukopi!!

Unaanza na fedha ndogo ili upate mtaji wako na kusonga mbele. Malalamiko ni vijana kutokuwa na hati za viwanja, sasa viwanja hivyo vinauzwa bei chee wanunue na viwasaidie kukopesheka. Ishu ni amount na sio tena ishu ya qualification
 
Back
Top Bottom