Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Bwana ametoa mabinti wametwaaaa jina la adamu lisimuliwe
loh!!!!!!!


Hapa nimetoka kapa.. Bwana ni JK au Malima Sr.?
 
Maelezo ya meneja wa hoteli mbele ya waandishi wa habari yamepindishwa kujaribu kumuokoa mzinzi yule, lakini yamechelewa! Wenye hoteli hawako tayari kuharibu biashara kumtetea mzinzi! Never on earth!
 

naambiwa aliona mabinti wanamekuja na pombe y kienyeji kwenye chupa ya uhai wakaomba aonje
huku amemwaga kwenye glass jack daniel loh ikawa jack malima
teeheeeteeehhhhhh wacha bana muulizeni mama rwakatare ile pombe yetu inaitwaje na heshima gani sio kipata ama kitochi ...ashazoea kuomba kuria mbege kili akajua iko the same loh ..ashukuru awakumshikakunani maana kuna wengine wakiona umelewa unakuta asbh suruali imelowa harufu
loh..ila mlichofanyamadada nyie amtosahaulika na familia ya malima kwa kweli kama si wana ......
 

Stuxnet, hivi ni kweli huoni what is special kwa huyu waziri, in this case?
 

Usiongee bila kuwa na data, tutaonekana kama Wazushi. Mimi sikubaliani na uchafu wowote , lakini nina tatizo na ukweli wa hilo tukio.
Polisi wamasema dirisha lilivunjwa na meneja wa Hoteli alikubaliana na maelezo hayo. Wewe ni nani hata upingane na taarifa ya kitaalamu iliyothibitishwa na meneja?
Sina hisa na mtu mkuu, bali sipendi uzushi.
 

kama kulala tu anatumia laki nne kwa siku?,je matumizi mengine inaweza kuwa milioni moja anatumia kwa siku?.na kama ndyo hivyo yeye anaingiza sh ngapi kwa siku?,na kwa hizo pesa kwa mwaka anatumia sh ngapi?,je matumizi yake na mapato yake vinaendana?.kupitia yeye serikali inapata sh ngapi ?au anazalisha sh ngapi? ili awe na uhalali wa kutumia hicho kiwango kwa siku.Je watanzania wanafaidikaje na uwepo wake katika utumishi wa umma?.Au watanzania tunaumia kiasi gani tukiwa na viongozi kama huyu? NISAIDIENI MAJIBU JAMANI
 

Ishu siyo Malima. Ishu ni kwamba thread imegusa mahala pake! Ukizingatia kwamba mwanamke akipewa nafasi Anaweza!
 
Kutokuwa mwaminifu katika familia siyo sehemu ya maadili ya viongozi wa Taifa la Tanzania? Mbona nchi kama Ujerman au Italy tukio kama hili linampotezea mtu sifa za kuwa kiongozi?
Nchi hii imeendelea sana kiasi utamaduni wa kuwajibika kwa skendo ni ishu iliyopitwa mno na wakati! Ndo maana unaona hata akina Mponda wanapeta!
 
Wana JF niambieni kuna nini special kuhusu Adam Malima? Maana mada imeanza sa 7.13 na kufika saa hizi ni saa 4 .11 za usiku lakini kuna wchangiaji 481... Je Adam ana maadui wengi kiasi hicho? Naomba jibu

Muulize yeye iweje atembee na AK 47 na bastola, kama hana maadui wengi kihivyo! Uliona wapi AK 47 inalinda dola 4,000 $ tu?
 
Alilala hoteli ya laki 4 kwa siku??????
Si ajabu mama watoto hakumwachia hata hela ya "mchicha", kwa kisingizio cha hali ngumu.
Nampongeza huyo dada aliyejihudumia hizo hela zisizo na kazi;
utalalaje hoteli ya laki 4 Moro kwa kutumia kodi za mlala hoi ambaye hajui kesho atakula nini?
Siku tatu tu malazi 1.2m. Afu eti bi kiroboto Makinda anadai hali ngumu wabunge wengi wako mbioni kuacha kazi. Thubutu! Hizo hela za kutanua nazo bila kutolea jasho watazitoa wapi?
 
hakuna siku ambayo magazeti ya udaku yanafurahia hiii thread maana jumatatu ndiyo habari kuu.
 


mkuu si afadhali ameibiwa? angekuwa ameuliwa au kunyeshwa sumu tungesemaje??

mpaka ulinzi anaotembelea Kikwete sisi tuliozoea CSI scenes nyingi unaona kabisa unampata pale, unammaliza hapa

nenda mabenki yetu hakuna ulinzi kabisa

as life getting tougher watch out! usiamini kila kitu mpaka chupi yako mwenyewe!
 
Binafsi huwa nafurahi na kusherehekea wanapoibiwa wakubwa kwani mfumo unaowaibua wezi na majambazi umejengwa na hao hao wakubwa. Hongereni wezi kwa kumwonjesha machungu ya kuibiwa. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea na tabia hiyo kwa wakubwa wengine. Mbarikiwe sana.
 

Ritz nasemaje haya mambo ya kawaida kabisa!! tena jamaa ashukuru ni waziri hivyo serikali itagharamia kila kitu pale

kuna story nyingi mno za wenzangu wahandisi wa ujenzi, ,migodi, masurveyor, ma geologist

kuna mahali unabanwa, unaingia na mtoto chumbani unaona kabisa itakuwa short time..mara una extend muda na huku ukilia na

kujuta kwa nini umeoa yule wakati raha ziko huku

kutahamaki huna michoro, simu, laptop na tender documents!!! achilia mbali theodolite na GPS!

kuna wanawake balaa acha kabisa

humu wengi wanasema kwa zile mila za kinafiki za ki-afrika as if they are 100% innocent kumbe ni vice versa kwa sababu ni Malima!

Huyu malima kama alikuwa na kamchezo haka tangu kabla hajawa waziri kuna mechanism gani au nguvu gani ya kuwa ukiwa waziri unaacha haka kamchezo?? kama sio kuwa ukiwa waziri ndio kanaongezeka

kwanza anatabia nzuri kwa dollar 4000? unakuwa na watatu unawachukua sehemu mbali mbali...mbona mshikaji yuko normal tu!! mmoja tu!

pole dume la mbegu
 
Reactions: ral
Kutokuwa mwaminifu katika familia siyo sehemu ya maadili ya viongozi wa Taifa la Tanzania? Mbona nchi kama Ujerman au Italy tukio kama hili linampotezea mtu sifa za kuwa kiongozi?

sasa huko si ni Ujerumani na Italy??

mbona na sense kama unakataa asili yako??
 
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 1"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Adam Kighoma Malima[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima amekombwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.


Taarifa za kipolisi zilizopatikana kutoka mjini Morogoro zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema ulitokea usiku wa kuamkia leo.


Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea wakati waziri huyo alipokuwa amejipumzisha kwenye sebule ya chumba chake kwenye hoteli hiyo hadi mida ya 10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani.


Kwa mujibu wa polisi zimeibwa fedha taslimu Dola 4000 za Marekani na Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh. milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.


Polisi wanasema dirisha la aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu kigumu.


Habari zinasema nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za mwizi.


Kufuatia wizi huo, walinzi watatu wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa vimepatikana, ingawa havikutajwa.


Posted by: ByBBashir Nkoromo
 
Hivi kweli Waziri Mzima Safari ya Morogoro unahitaji kuwa na Dola 4,000 mfukoni, ni za nini?

Yaani Mawaziri wa Awamu ya Nne ni Matajiri haswa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…