Naibu Waziri Mkuu majukumu yake Kikatiba ni yapi? Wafahamu waliowahi kuwa Manaibu Waziri Wakuu nchini

Kanda ya ziwa na kama maji tu, usipoyanywa utayaoga!
 
Hata Sasa hiki cheo kimetolewa kwasababu maalumu Ili kudhoofisha utendaji wa Majaliwa, maana alikuwa haungi mkono uwekezaji wa bandari
Pongezi sana kwa Majaliwa.
Kimya yake ni jibu kwa utawala huu wa hovyoo
 
Ndo nimeskia leo kuna nafasi ya naibu waziri mkuu
 
Walowahi kupewa.

1. Salm A Salim
2. Lyatonga Mrema
3. Ernest Nyanda. Huyu alikuwa mbunge wa Magu/ Busega

4. Doto Biteko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho cheo hakipo kisheria! Kwenye katiba yetu pendwa hicho cheo hakipo!
Cheo hakipo ila katiba inamruhusu prizidenti kuanzisha cheo chochote nakufuta cheo chochote,, tukililia katiba mpya tuwe tunaeleweka
 
Kipara ngwidu Kila sehemu anayo wekwa hatoshi, hii ni hasara nyingine kwa jamuhuri ya uswahilini
 
Aha
Like fadher like a daughter
 

Agosti 30, 2023, Rais Samia alimteua aliyekuwa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu, nafasi ya Uongozi ambayo mara ya mwisho ilitumikiwa mwaka 1994 na Hayati Augustino Mrema.


Pia, Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye amewahi kuwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alihudumu katika nafasi hiyo mwaka 1986 hadi 1989 chini ya Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Ikumbukwe, Katiba ya Tanzania Ibara ya 36(1) imempa Rais Mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya aina mbalimbali katika Utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Cheo cha Waziri mkuu hakina tija kama makamu wa Rais yupo.

Kuwa na VP pamoja na PM kwa nchi masikini kama Tanzania ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi walalahoi.
 
Nilikuwa sioni upungufu wowote kwenye UTATU wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu

Na hata sasa sioni upungufu wowote kwenye UTATU ni kwamba Kazi zote zinakwenda sawia

Anyway Siasa ni Sayansi 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…