Manjagata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 13,942
- 15,371
Ndiye waziri mkuu wa 2025-2030Biteko hata uwaziri mkuu na uraisi kabisa anafit ...Jamaa ni snart sana.!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiye waziri mkuu wa 2025-2030Biteko hata uwaziri mkuu na uraisi kabisa anafit ...Jamaa ni snart sana.!
Rubbish...Anaruhusiwa...View attachment 2733336
Mkuu inawezekana kabisa🤣🤣🤣🪑Ni njia ya kisiasa ya kummaliza waziri mkuu bila kuvunja serikali.
Pongezi sana kwa Majaliwa.Hata Sasa hiki cheo kimetolewa kwasababu maalumu Ili kudhoofisha utendaji wa Majaliwa, maana alikuwa haungi mkono uwekezaji wa bandari
Soma ibara ya 36 (1 - 4)Hii nchi katiba inavunjwa hakuna wa kuhoji, hicho cheo hakipo kikatiba ndiyo maana hata Jaji Mkuu muda wake ulishapita lakini yupo kwa kuvunja katiba
Walowahi kupewa.Hapa staki kuongea sana kwa sabu sielewi mambo ya Kisheria
Naongelea hii nafasi aliyopewa na kuteuliwa mh Dotto Biteko kuwa Naibu waziri mkuu, sjawahi kuisikia na wala kuona tangu nchi yangu ipate uhuru
Hii inamaana gani? Ni mh Rais kuogopa kulivunja bunge kwa kutokumtengua waziri mkuu?
Au lipo kikatiba?
Tafadharini Waheshimiwa sana viongozi wetu meza kuu Maadimin wetu Jf
Msiunganishe huu uzi
Cheo hakipo ila katiba inamruhusu prizidenti kuanzisha cheo chochote nakufuta cheo chochote,, tukililia katiba mpya tuwe tunaelewekaHicho cheo hakipo kisheria! Kwenye katiba yetu pendwa hicho cheo hakipo!
Tangu lini CCM ikapenda wenye akili? Angalia wenye akili na wafia nchi wanavyonyanyaswa na kubagazwa ndani ya CCM!!!!!?Biteko akili nyingi na dhamira ya kweli
Like fadher like a daughterMpaka leo hii, hiki cheo kiliwahi kushikiliwa na watu 2 tuu tena kwa sababu maalumu sana na nyeti, na zenye maslahi mapana kwa taifa.
1. Dr. Salim Ahmed Salim.
Salim alipewa cheo hiki 1986 mpaka 1990, kwasababu aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja enzi za Mwalimu Nyerere (Baada ya Kifo cha Sokoine), hivyo baada ya Rais Mwinyi kuingia akaona ni Busara Waziri Mkuu wake aliyemteua Joseph Sinde Warioba awe na Naibu ambaye ni Salim.
2. Augustino Lyatonga Mrema
Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema alitumia ujuzi wake kama KACHERO WA USALAMA WA TAIFA, kudadisi na kukamata wezi na wala rushwa katika kila wizara ya Serikali aliyogundua mambo si shwari.
Hali hiyo ikawaudhi baadhi ya mawaziri wenzake serikalini. Wakamwambia "MREMA USIVUKE MIPAKA YAKO, Wewe ni waziri kama sisi na huwezi kuingilia mambo ya ndani kwenye wizara zetu bila kujadiliana nasi kwanza." Mrema anasema alikomaa nao, na ndipo Rais Mwinyi akagundua dhamira yake njema.
Rais Mwinyi mnamo mwaka 1992 akamuongezea cheo kipya Mrema. Akamteua kuwa NAIBU WAZIRI MKUU.
1993, Mrema alipopewa Unaibu Waziri Mkuu anasema "wenzangu walianza kuniogopa na kuniheshimu. Hata kama wanaenda sehemu walikuwa wanalazimika kusimama kwanza ili kupisha msafara wenye ving'ora wa Naibu Waziri Mkuu."
Akiwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu alishughulika na kila aina ya ubadhirifu, wizi na magendo kwa kadri alivyopata taarifa. Akawa waziri maarufu sana kwa wananchi mijini na Vijijini.
"Rais Mwinyi kila akirudi kutoka mikoani alikua akiniita na kuniambia Mrema nimetoka kwenye ziara, wananchi wanakusalimia sana. Unafanya kazi nzuri," alinisimulia Mzee Mrema katika mahojiano hayo ya MSUMARI WA MOTO.
Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu Mrema zama hizo za uwaziri wake wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu ilikua ni kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi kwa nguvu za wananchi ili kuimarisha ulinzi lakini pia "Tajirika na Mrema" - UTOAJI WA ZAWADI KWA WATU WANAOFICHUA WAHALIFU.
Nani angekubali kukaa na taarifa za mwizi au muhalifu wakati ana uhakika akimfichua atapewa zawadi?
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Swali ni je, Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kwa merits alizonazo, ama ameteuliwa kwa sababu Majaliwa ameonekana anapwaya kwenye u Waziri Mkuu?
Ukizingatia wasukuma ni wengi kuliko kabila lolote Tanzania hii.Zinatafutwa kura za Wasukuma hapo 2025
Ernest Nyanda ni lini alikuwa naibu waziri mkuu?Walowahi kupewa.
1. Salm A Salim
2. Lyatonga Mrema
3. Ernest Nyanda. Huyu alikuwa mbunge wa Magu/ Busega
4. Doto Biteko
Sent using Jamii Forums mobile app