Naibu Waziri Mkuu majukumu yake Kikatiba ni yapi? Wafahamu waliowahi kuwa Manaibu Waziri Wakuu nchini

Mpaka leo hii, hiki cheo kiliwahi kushikiliwa na watu 2 tuu tena kwa sababu maalumu sana na nyeti, na zenye maslahi mapana kwa taifa.

1. Dr. Salim Ahmed Salim.

Salim alipewa cheo hiki 1986 mpaka 1990, kwasababu aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja enzi za Mwalimu Nyerere (Baada ya Kifo cha Sokoine), hivyo baada ya Rais Mwinyi kuingia akaona ni Busara Waziri Mkuu wake aliyemteua Joseph Sinde Warioba awe na Naibu ambaye ni Salim.

2. Augustino Lyatonga Mrema

Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema alitumia ujuzi wake kama KACHERO WA USALAMA WA TAIFA, kudadisi na kukamata wezi na wala rushwa katika kila wizara ya Serikali aliyogundua mambo si shwari.

Hali hiyo ikawaudhi baadhi ya mawaziri wenzake serikalini. Wakamwambia "MREMA USIVUKE MIPAKA YAKO, Wewe ni waziri kama sisi na huwezi kuingilia mambo ya ndani kwenye wizara zetu bila kujadiliana nasi kwanza." Mrema anasema alikomaa nao, na ndipo Rais Mwinyi akagundua dhamira yake njema.

Rais Mwinyi mnamo mwaka 1992 akamuongezea cheo kipya Mrema. Akamteua kuwa NAIBU WAZIRI MKUU.

1993, Mrema alipopewa Unaibu Waziri Mkuu anasema "wenzangu walianza kuniogopa na kuniheshimu. Hata kama wanaenda sehemu walikuwa wanalazimika kusimama kwanza ili kupisha msafara wenye ving'ora wa Naibu Waziri Mkuu."

Akiwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu alishughulika na kila aina ya ubadhirifu, wizi na magendo kwa kadri alivyopata taarifa. Akawa waziri maarufu sana kwa wananchi mijini na Vijijini.

"Rais Mwinyi kila akirudi kutoka mikoani alikua akiniita na kuniambia Mrema nimetoka kwenye ziara, wananchi wanakusalimia sana. Unafanya kazi nzuri," alinisimulia Mzee Mrema katika mahojiano hayo ya MSUMARI WA MOTO.

Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu Mrema zama hizo za uwaziri wake wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu ilikua ni kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi kwa nguvu za wananchi ili kuimarisha ulinzi lakini pia "Tajirika na Mrema" - UTOAJI WA ZAWADI KWA WATU WANAOFICHUA WAHALIFU.

Nani angekubali kukaa na taarifa za mwizi au muhalifu wakati ana uhakika akimfichua atapewa zawadi?
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Swali ni je, Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kwa merits alizonazo, ama ameteuliwa kwa sababu Majaliwa ameonekana anapwaya kwenye u Waziri Mkuu?
Safi,mtu akishindwa mtafutie msaidizi ambae ataheshimika ,hiki hakina tofauti na Waziri wa Mambo maalumu
 
Tunamtaka Makonda
 
Naibu waziri mkuu kaja kubalance influence ya kanda ya Ziwa!! Lissu na Mbowe wameivuruga lake zone mbaya kabisa CCM inapumulia mashimo
Hii ni applicable Kenya, Tanzania hatuna hayo mambo, Lowasa alikuwa na nguvu Monduli kwake na sio kanda ya kaskazini, Yule Mmilikibwa StarTv alisha kuwa Waziri kama sikosea je alikuwa na uungwaki mkono kwa kanda ya ziwa? Kenya haya yanawezekana ila sio Tanzania
 
Jamani hili Taifa letu tunaendaje? Vyeo vinakuwa vingi Sana. Ina maana ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa kubwa sana mpaka utendaji unakuwa Mdogo na kuamua kuiongeza nguvu kumpa msaidizi vipi? Vipi wizara zilizo chini yake?

Ningependa kujua majukumu ya Naibu Waziri Mkuu yatakuwa yapi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri na Muungano wa Tanzania.

Pia soma - "Naibu Waziri Mkuu" ni Cheo Nyeti Sana, huwa hakitolewi ovyo ovyo
Soma hii hapa 👇
 
Kipindi kile Makamu wa Rais alikuwa ni Waziri Mkuu pia. Kwa hiyo, kwa sasa ni kama utaratibu mpya na pengine lengo ni kumpunguzia majukumu WM
 
Hapa staki kuongea sana kwa sabu sielewi mambo ya Kisheria

Naongelea hii nafasi aliyopewa na kuteuliwa mh Dotto Biteko kuwa Naibu waziri mkuu, sjawahi kuisikia na wala kuona tangu nchi yangu ipate uhuru

Hii inamaana gani? Ni mh Rais kuogopa kulivunja bunge kwa kutokumtengua waziri mkuu?

Au lipo kikatiba?

Tafadharini Waheshimiwa sana viongozi wetu meza kuu Maadimin wetu Jf

Msiunganishe huu uzi
Hapa Tanzania iliwahi tokea mtu akateuliwa cheo hicho...Hilo litakuwa jambo geni huko kwenu Burundi!
 
Jamani hili Taifa letu tunaendaje? Vyeo vinakuwa vingi Sana. Ina maana ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa kubwa sana mpaka utendaji unakuwa Mdogo na kuamua kuiongeza nguvu kumpa msaidizi vipi? Vipi wizara zilizo chini yake?

Ningependa kujua majukumu ya Naibu Waziri Mkuu yatakuwa yapi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri na Muungano wa Tanzania.

Pia soma - "Naibu Waziri Mkuu" ni Cheo Nyeti Sana, huwa hakitolewi ovyo ovyo
Majukumu yake makuu yatakuwa ni KUMDHIBITI Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ili ASIFURUKUTE kama ilivyo kwa cheo cha Makamu wa Pili wa Rais kule Zanzibar ambaye anamdhibiti Kikamilifu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kutoka chama cha ACT-Wazalendo.
 
Mama aliposema yaani mpaka PM aende halafu aambiwe ndio aje kuniambia kuwa huyo hafai
Basi nikajua kuna kitu
Sasa naona jipu limelata mkunaji
 
Mpaka leo hii, hiki cheo kiliwahi kushikiliwa na watu 2 tuu tena kwa sababu maalumu sana na nyeti, na zenye maslahi mapana kwa taifa.

1. Dr. Salim Ahmed Salim.

Salim alipewa cheo hiki 1986 mpaka 1990, kwasababu aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja enzi za Mwalimu Nyerere (Baada ya Kifo cha Sokoine), hivyo baada ya Rais Mwinyi kuingia akaona ni Busara Waziri Mkuu wake aliyemteua Joseph Sinde Warioba awe na Naibu ambaye ni Salim.

2. Augustino Lyatonga Mrema

Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema alitumia ujuzi wake kama KACHERO WA USALAMA WA TAIFA, kudadisi na kukamata wezi na wala rushwa katika kila wizara ya Serikali aliyogundua mambo si shwari.

Hali hiyo ikawaudhi baadhi ya mawaziri wenzake serikalini. Wakamwambia "MREMA USIVUKE MIPAKA YAKO, Wewe ni waziri kama sisi na huwezi kuingilia mambo ya ndani kwenye wizara zetu bila kujadiliana nasi kwanza." Mrema anasema alikomaa nao, na ndipo Rais Mwinyi akagundua dhamira yake njema.

Rais Mwinyi mnamo mwaka 1992 akamuongezea cheo kipya Mrema. Akamteua kuwa NAIBU WAZIRI MKUU.

1993, Mrema alipopewa Unaibu Waziri Mkuu anasema "wenzangu walianza kuniogopa na kuniheshimu. Hata kama wanaenda sehemu walikuwa wanalazimika kusimama kwanza ili kupisha msafara wenye ving'ora wa Naibu Waziri Mkuu."

Akiwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu alishughulika na kila aina ya ubadhirifu, wizi na magendo kwa kadri alivyopata taarifa. Akawa waziri maarufu sana kwa wananchi mijini na Vijijini.

"Rais Mwinyi kila akirudi kutoka mikoani alikua akiniita na kuniambia Mrema nimetoka kwenye ziara, wananchi wanakusalimia sana. Unafanya kazi nzuri," alinisimulia Mzee Mrema katika mahojiano hayo ya MSUMARI WA MOTO.

Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu Mrema zama hizo za uwaziri wake wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu ilikua ni kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi kwa nguvu za wananchi ili kuimarisha ulinzi lakini pia "Tajirika na Mrema" - UTOAJI WA ZAWADI KWA WATU WANAOFICHUA WAHALIFU.

Nani angekubali kukaa na taarifa za mwizi au muhalifu wakati ana uhakika akimfichua atapewa zawadi?
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Swali ni je, Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kwa merits alizonazo, ama ameteuliwa kwa sababu Majaliwa ameonekana anapwaya kwenye u Waziri Mkuu?
JE KATIBA INASEMAJE KUHUSU CHEO HIKI?
 
Back
Top Bottom