Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Kule kwao ndipo moshi wa Ruangwa ulimzimisha magufuli siku 3 hoi kuna watu hawakulizika na uteuzi wake kule jimboni kwake wanandai pesa zao za kufanikisha uchakachuaji hajawalipa
Atakuwa naape hyo.
 
Acha uongo why yeye tu
 
Unashangaa kwa sababu labda huna utu kama huyo unayemjibu. Nini cha ajabu kumuonea huruma mtu aliyekuzidi mafanikio akipata matatizo?
 
Unashangaa kwa sababu labda huna utu kama huyo unayemjibu. Nini cha ajabu kumuonea huruma mtu aliyekuzidi mafanikio akipata matatizo?
ila kweli sisi magorilla...yani Watu wanatunyonya wanakula keki ya nchi wanagawana vyeo na ulaji..Bado tunawahurumia wakati hawapotezi kitu..Bado hapo ana sehemu kuendelea kula

Sisi ndo tunaowahurumia wao hata hawatujali wananunua magari ya mill400

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka yule binti kutoka Lindi UVCCM alishindwa kujinadi kwa wajumbe akapata kigugumizi cha ukubwani,,,Hata huyu naibu waziri ni uchawi tu...watu wa Lindi acheni mimoshi yenu khaaa
 
Mi najiuliza zile fomu walizijazaje hata wapinzani wakashindwa kujaza
 
Inasemekana kwamba maandishi yalikua yanaonekana kama hivyo
 
Kuna kitu hapo hakiko sawa kwenye uteuzi wake, hofu yake inatokana na siri alizonazo mwenyewe!. Inawezekana kuwa hakutarajia kupata uteuzi, lakini alikuwa na muda wa kujiandaa angalau kukariri kiapo alichotakiwa kuapa.
Kwani kiapo kile wanakariri?
 
Huo ndio utu na hata maandiko yanatuongoza hivyo.
 
Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.

Ngoja niwakumbushe;

Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.

Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.

Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.

Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…