Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Kwa nini tena kuhoji elimu yake na kumtumbua? Kwa nini asipewe muda ili aape tena?
Nimesema sisi tunapoteza muda kwa kujadili hili..ni suala la mteule na mteuliwa. Sana Sana sisi kiubinadam tunamuonea huruma tu tungemuomba mheshimiwa Rais ampe nafasi zaidi.

Masuala haya huwa mengi yanapita na wakati binadamu wengine huko wanaweza kuwa wametengeneza yao ili tu kumkwamisha katika Hilo.

Kwa elimu aliyonayo namshauri Mh Rais aendelee kumtumia Kama alivyokuwa amepanga...inawezekana Ni sauti ya Mungu kwayeye kupewa nafasi ile...Mh.Rais ampime kwa utendaji wake wa mbeleni..
 
Ameshatenguliwa tayari,waallah uchawi upo,hicho kipapai alichopigwa ni kiboko
Hiyo aibu najaribu kuvaa viatu vyake naona havienei kabisa.Ndugu jamaa na familia utawatizama vipi.
Unawaza hao? Mkeo utamuambia nini akuelewe?
Alishajua anaenda kuwa mke wa naibu waziri.

Ukijaribu kumla mate hii ndio picha atayokuwa anaiona machoni pake: Ng'ombe
giphy.gif
 
Nimesema sisi tunapoteza muda kwa kujadili hili..ni suala la mteule na mteuliwa. Sana Sana sisi kiubinadam tunamuonea huruma tu tungemuomba mheshimiwa Rais ampe nafasi zaidi..masuala haya huwa mengi yanapita na wakati binadamu wengine huko wanaweza kuwa wametengeneza yao ili tu kumkwamisha katika Hilo..kea elimu aliyonayo namshauri Mh Rais aendelee kumtumia Kama alivyokuwa amepanga...inawezekana Ni sauti ya Mungu kwayeye kupewa nafasi ile...Mh.Rais ampime kwa utendaji wake wa mbeleni..
Sijakuelewa.
 
Nasikia wateule wa rais huwa wanafanyiwa vetting ya hali ha juu.

Nani huwa anamfanyia rais vetting? Mpaka anampa majina ya watu ambayo hawawezi hata kusoma kiapo na kutamka!

Hawa watu mbona kama wamemtia doa mkuu wa nchi, maana sinawahi kushuhudia mtu akitumbuliwa kwa kushindwa kusoma kiapo na kutamka!

Hii inaleta picha gani? Kuwa kama ni kweli kwamba watu wanaomfanyia vetting mkuu wa nchi hawako makini mpaka wanampa majina ya watu ambao wanashindwa kuapa!

Au ni mambo ya kijamii yameitawala Tanzania,ndio maana watu wengi wenye IQ kubwa huwezi kuwakuta kuwa ni viongozi?

Inasikitisha sana kwa Taifa ambalo linajinasibu kuwa ni moja ya taifa kubwa hapa Afrika mashariki, waziri mdogo anashindwa hata kusoma na kula kiapo. Nafikiri maneno aliyosema Askofu Rashid kuwa wengi wa wabunge wa CCM walipita kwa mgongo wa kiongozi wao wa chama,sababu 70% walikuwa hawana uwezo na hata kukubalika ilikuwa ni kwa mashaka

Kwa ujumla aliyeshindwa kuapa na aliyemtumbua wote wameaibika.
Urais ni taasisi na hateui mtu mmoja pekee. Rais atashauriana na waziri mkuu...
 
WaTZ wengi hawajazoezwa mashuleni na vyuoni kujiamini. Hata wanachuo wa University more than 70% hawawezi kabisa kujieleza. Hata akiulizwa swali na mwalimu, hawezi kujieleza;b tena kama ndiyo kwa lugha ya malkia, Ni msiba atatafuta pa kukimbilia akajifiche. Ila kujieleza kwa maandishi, hawajambo.
Somo la kujiamini litiliwe mkazo mashuleni na vyuoni.
 
Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
Hilo ni jambo la kawaida hutokea kwa wanadamu wengi, kuna rais wa Marekani ilimtokea miaka ya nyuma
 
Dah aisee uchawi upo, unaona maandishi yamepandana mpaka unashikwa kigugumizi. Walimwengu washafanya yao.
Serikalini katika nyadhifa za juu usipokuwa mtu wa kimila hutoboi!
Ndio uchawi wanaotumia wanasiasa wa Lindi kuna mwingine wa UVCCM toka Lindi yalimtokea


 
Sijakuelewa.
Nasemaaa suala la mteule na mteuliwa sisi hatuwez lijadili.. sanasana tunamuonea huruma bwana waziri mteule kwa yaliyotokea.. na sanasana kiubinadam tunamuombea kwa mhe. Rais ampe second chance,.

Masuala haya ya viapo wakati mwingine yanaweza kukwamishwa na midomo ya wanadam kwa chuki tu na wivu.. unakuta wanachez mchezo kumkwamisha mwingine...

Nina imani na uzoefu wake na elimu yake inaweza saidia kule ambapo Rais alipanga kumuweka... sisi wananchi ambao tuko nyuma ya mhe. Rais tungemshauri aendelee nae amuapishe then apige kazi.. aendelee na vetting zaidi mbeleni ili kuondoa doubt yoyote inayokuwepo.. natumai Mhe.Rais atasoma ujumbe huu Kama ushauri na inawezekana Ni maono na sauti ya Mungu pia..

God bless our president..
 
Back
Top Bottom