Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.
Ngoja niwakumbushe;
Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.
Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.
Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.
Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.
Mungu wa mbinguni awabariki nyote.
Maendeleo hayana vyama!