Sasa huku kwenye frem wanazochezesha ps huwa wanalipia pesa kwahiyo dogo kaanza kuiba Hela nyumbani Ili aende kucheza, kukiwa hakuna pesa anaweza kuuza vitu vidogo vidogo, baba yake alipogundua alimtembezea kipigo cha haja lakini bado hasikii.
Wale Old-Timers, sio kwa umri bali old timers kwa haya mambo bado wanaikumbuka Dangerous Dave back in 1990's and early 2000's!!
Wakati ule nilikuwa kijana mdogo, lakini nilikuwa Nusu Zombie Nusu Mtu! Ningeweza kukaa kwenye PC siku mzima, hata kula sili.
Nakumbuka PC yangu ilikuwa na ROM 1GB na RAM 576MB....
Thanks God nikaenda chuo, na karibu mwaka mzima sikuwa na access to PC. Baada ya kuanza kuisahau Dangerous Dave nikaapa kukaa mbali na games za aina yoyote ile manake nafahamu jinsi zilivyo too addictive!!
Leo hii, thanks God... nasikia tu mara Play kufanya nini, mara Play Station... zote hizo sijawahi hata kuzigusa na naziogopa kama ukoma!!
Kama upo poor kwenye time management, video and pc games ni msiba wako! Na ukishakuwa addictive, hakuna cha kuwa poor kwenye time management wala good...
Anyway, naona siku hizi nimeanza taratibu kurudi kwenye huo ufa'la manake simu yangu ina games 200 kidogo, na nimeshaanza uboya kwamba wakati wa kulala LAZIMA nipige round kadhaa za some games!