Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Aisee, mda mwingine na mimi napata haya mawazo.....

nimekuelewa sana, pole

jua tu kwamba mbali na yote hayo, mama yako hajutii uwepo wako kwenye maisha yake


Mimi huwa nasema tushukuru kwa hii mechanism ya ku adapt mambo ambayo tumeumbwa nayo otherwise mambo mengine katika maisha ni majuto makuu.

Yes, anaweza kuwa anajivunia uwepo wake kwenye maisha yake lakini hiyo haifuti ukweli mchungu kuwa kupitia yeye maisha yake yameharibika mno.
Na maybe kila akiwaona wenzake waliko husikitika sana.

Kuna mwanamke mmoja namfahamu niliwahi pewa stori yake kuwa alikuwa na akili sana darasanie. Alifanya mitihani yake na kufaulu vizuri sana
Kumbuka ni zamani sana miaka ya 80 huko.
Sasa ile anatakiwa aende chuo baada ya matokeo mazuri,ikagundulika kuwa ana ujauzito.
Shule ikawa basi. Leo classmates wenzake wana magari na kazi nzuri lakini yeye yupo tu with no hope. And the sad thing ni kwamba wapo within the same city.
She saw them ride as she conduct her entrepreneurship activities by the side of the road.
 
Thread yote hii hujamzungumzia baba kabisa.

Watoto wa mama mnapenda sana kudeka.

Ndio nyie mnapaswa kuitwa JUNIA.
Kuna muda wa kina baba Huwa wanakosea sana. Hivyo kwakuwa nimeamua kujilaumu mwenyewe sijapenda sana kumzungumzia baba kwasababu ingepelekea Mimi kumlaumu.

Itoshe TU kusema kuwa Kuna vitabia vya kiarabu ambayo vimekuja kututia UMASIKINI sana sisi waafrika. Yani hatujaona jambo jema kuliiga Zaidi ya kuoa wake wengi. Mwisho wa siku familia inamshinda😭😭😭

Mkuu Nina mengi ya kuzungumza ila Leo nilitaka kujilaumu mwenyewe ili nisinge mbele.​
 
Mimi nadhani vijana mliozaliwa 90s muwashukuru sana wazazi wenu, hasa mliozaliwa kwa "bahati mbaya", ni kipindi ambacho vijana wengi walichoropoa mimba hatari. So mama yako aheshimiwe sana.

Don't dwell in the past, pambana.
 
Mimi nadhani vijana mliozaliwa 90s muwashukuru sana wazazi wenu, hasa waliozaliwa kwa "bahati mbaya", ni kipindi ambacho vijana wengi walichoropoa mimba hatari. So mama yako aheshimiwe sana.

Don't dwell in the past, pambana.
Shukrani sana boss.
 
Nitajitahidi sana. Asante boss
 
Amesema wamesoma darasa moja na ni wa kijiji kimoja.
Mama anatakiwa amlilie Mtendaji msaada kama itawezekana. Kijana ana cheti, sio ngumu sana kumsaidia ikiwa tu ana moyo wa kusaidia
 
Nashukuru sana. Hata hivyo najivunia kuwa na mzazi. Ila najutia kuwa nashindwa kutatua matatizo ya mzazi wangu badala yake yeye ndio ananitatulia matatizo yangu. Hii kwangu ni aibu sana.​
Aibu bila kuikwepa itafuatia fedhea,sasa wewe endelea kulalamika wakati hata kubeba deli la vitumbua alivyo choma mama yako ukauze hutaki eti kisa wewe ni msomi mjinga.
 
Wapende wazazi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…